Mfumo wa Mawasiliano wa Korea Kaskazini na Sababu za Vikwazo vya Kimataifa

Ozon

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2024
Posts
2,910
Reaction score
4,711
Luhaga Mpina, katika bandiko lake kwenye ukurasa wa X (zamani Twitter), mbunge huyo ameandika: "Miaka 8 nyuma nchi yetu ilishtumiwa na UN kuwa na uhusiano wa kibiashara na kiulinzi na usalama wa NORTH Korea unaohusisha mkataba wa \$12.5m. Tulikanusha! UN haikutoa ripoti ya uchunguzi, ikashia hivyo. Nani anaujua mfumo wa N.Korea wa kusisimamia mawasiliano? Sijasema TCRA wanao." Swali linalozuka ni: je, ni mfumo gani huo wa Korea Kaskazini wa kusimamia mawasiliano ambao umewekewa vikwazo na jumuiya za kimataifa?

Korea Kaskazini inafahamika duniani kwa kuwa na mfumo mkali wa udhibiti wa mawasiliano, unaotumika ndani ya nchi hiyo kwa ajili ya upelelezi wa ndani (surveillance), udhibiti wa taarifa, na matumizi ya kijeshi. Mfumo huu hauishii tu kwenye intaneti na simu bali unajumuisha pia vifaa vya mawasiliano ya kijeshi, teknolojia za kudhibiti mitambo ya anga na makombora, pamoja na matumizi ya satelaiti kwa ujasusi.

Kwa mujibu wa maazimio kadhaa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kama vile 1718, 1874, 2094 na mengine yaliyofuata, Korea Kaskazini imewekewa vikwazo vya wazi dhidi ya usafirishaji au upokeaji wa vifaa vya mawasiliano ya kijeshi, mitambo ya kudukua (interception), na teknolojia zinazoweza kutumika kwa ukandamizaji wa haki za binadamu au kutengeneza silaha. Jumuiya ya kimataifa imeweka vikwazo hivyo ili kuzuia Korea Kaskazini kutumia teknolojia hizo kuimarisha mifumo ya kiimla na programu zake za nyuklia au makombora.

Ushirikiano wowote wa kiteknolojia, hasa unaohusisha mawasiliano, kati ya nchi yoyote na Korea Kaskazini unachukuliwa kuwa ukiukaji wa maazimio hayo. Hii ni kwa sababu teknolojia ya mawasiliano ina matumizi mawili (dual-use): inaweza kusaidia maendeleo ya kiraia lakini pia inaweza kutumika kwa madhumuni ya kijeshi au ukandamizaji.

Mfumo wa Korea Kaskazini wa kusimamia mawasiliano si mfumo wa kawaida wa kiutawala au kibiashara, bali ni chombo cha kimkakati kinachotumiwa na serikali hiyo kwa ajili ya ulinzi, upelelezi, na udhibiti mkali wa raia wake. Hii ndiyo sababu kuu iliyowasukuma wahusika wa kimataifa, wakiwemo Umoja wa Mataifa, kuweka vikwazo dhidi ya mifumo hiyo, na kwa nchi yoyote inayodhaniwa kushirikiana na Korea Kaskazini katika maeneo hayo, tahadhari ya juu hutumika, hata kama hakuna ushahidi wa wazi uliowasilishwa hadharani.
 
Mara nyingine makatazo yanawekwa sio kwasababu ya haki za binadamu bali mikakati ya kibiashara.

Waulize Lesotho walichofanyiwa na Mmarekani kisa biashara anayofanya na Mchina.
Hakuna biashara kati ya Nchi maskini na nchi za kidikteta hakuna braza. Lesotho na China?
 
Comment ipo tu general.

Hizi tarrifs ulizoziskia hazikuja kwa bahati mbaya. Lesotho ni mmoja wa supply wakubwa wa Textiles Marekani. Hizi jeans kama Levi's unazovàa material yakatoka Lesotho.

Marekani baada ya kuona pua ya mchina Lesotho alilimwa tarrifs ambayo hakuna nchi ya Africa ililimwa.

Haya matamko si ya bahati mbaya kama wengi tudhaniavyo.
 
China imemsaidia nani kibiashara hapa afrika zaidi ya madeni tu?
 
Unakosea sana bro.
Embu FANYA tafiti vizuri.
Afrika aliyefanya iendelee kimiundombinu ni CHINA.
Tanzania yako reli barabara na miundombinu mingi hadi viwanda baadhi ambavyo vingine mmeshindwa kuviendesha ikiwemo Urafiki Textile ni Mchina.
Afrika isingekua na maendeleo kama sio urafiki na China.
Hili halipingiki usijitie upofu kaka.
 
Nitalifanyia kazi hili
 
Nchi zilizokua za Kikominist zina shida sana yaani; utakuta wanajifanya kuzua mambo eti ya kiulinzi wakati viongozi wao wezi wakubwa na matajiri wa kutupwa; look at Iran as well, Korea hi inayozungumzwa hapa, viongozi wao ni mabilionea wa kutupwa yaani. Nchi za Kiafrica na zenyewe sasa; ubaya wa black countries, pesa wakiiba wanakwenda kuficha nje ya bara letu, badala basi hata ya kuweka nchini mwao walau basi watengeneze ajira kwa wananchi wao, wao wapeleka oversees, stupid
 
Huwezi kuwa bilionea Korea ya kim, Iran haijawahi kuwa nchi ya kijamaa...get your facts right kabla hujatoka nje
 
Nilivyo kuelewa ni kwamba waendelee kuiba ila wawekeze nchini mwao Africa, asante kwahilo ila tusisikie hoo kiongozi fulani ni fisadi lakini 🙏🙏
 
Nitajie wamiliki wa visima vya mafuta wa Iran, nitajie wafanyabiashara wakubwa na mabilionea wa Iran kaka.
Ukimaliza, jiulize hivi, "ujamaa ni neno au matendo, ubepari hali kadhalika"

So yale maneno "...kibaya zaidi..." hayana maana yoyote kwako? Kanisome tena kaka, usifanye tu hitimisho haraka.
 
Mafuta ya saudia humilikiwa na nani?.. kwamba Iran mfumo wake wa uchumi ni kama ujamaa wa tanganyika,soviet,china?
 
Back
Top Bottom