Mzawa_G
JF-Expert Member
- Feb 27, 2014
- 669
- 1,475
Mawasiliano na vyombo mbalimbali vya anga za mbali ni kitu muhimu sana ndio maana mamlaka husika imekuwa ikiweka mifumo imara itakayoweza kuwasiliana na vyombo mbalimbali vinavyoenda katika anga za juu kufanya chunguzi.
Mengi yaliyojificha yapo juu angani kwa kuchukulia vile tunavyoweza kutazama sisi wanadamu, mifumo mbalimbali ya nyota tunaitazama angani yaani juu yetu kabisa hapo moja kwa moja hata vifaa vyetu vya kupokea na kutuma taarifa mbalimbali zinabidi zitazame angani juu kwakuwa ndipo kwenye yale yaliyojificha.
Mifumo ya aina hii ya mawasiliano huwa inafanya kazi kwa nguvu na kwa haraka sana bila kusahau inaweza kubeba rundo la taarifa kubwa kwa wakati mmoja tofauti na baadhi ya mifumo mbalimbali ya mawasiliano hapa duniani kwetu.
Mara ya mwisho NASA walisema kuwa mfumo wao wa mawasiliano hufikia mpaka kiasi cha kasi ya 90 Gb kwa sekunde moja, unaweza ukaona ni jinsi gani mfumo huu unavyokwenda kwa kasi sana.
Kitaalamu mfumo huu ujulikana kama Deep Space Network ambao huweza kufanya mawasiliano na chombo katika eneo lolote la ulimwengu.
[emoji625]Moudyswema
[emoji625]Gerald
[emoji625]geraldchristopher1@gmail.com