Ndugu wana JF habari za sku.
Imenilazimu kuandika Mada hi baada ya kuona mengi yanayojitokeza nchini kwetu.
Raisi wetu mama Samia Suluh Hassan anapofanya teuzi zake hutuhumiwa na baadhi ya watu kuwa anaupendeleo kwa Zanzibar wenzake.
Uteuzi wa Mkurugenzi wa TPDC inatuhumiwa eti ni mzanzibari na inaonekana haistahiki kwa shirika la Muungano.
ilitakiwa amchague Mtanganyika. kwakuwa Zanzibar eti wanashirika lao linaitwa ZPDC.
Mitafaruku ya aina hii ya mambo ya kimuungano imeshajitokeza sana kwa maraisi waliotangulia.
OIC ilifika kuleta mtafaruku wa kuvunjika Muungano.
Suala la Benki kuu na A/C ya pamoja bado ni kitendawili tokea miaka ya 80 HAKIJATEGULIWA.
Kuna tume kadhaa zimeundwa na kutumia fedha nyingi za Watanzania hatimae mapendekezo yao yametupwa.
Moja ya mapendekezo ni lile la serikali 3. liiwa limependekezwa na tume zaidi ya 3.
Kuna vikao vya mawaziri wakuu na waziri kiongozi(Makamu wa pili wa raisi kwa sasa) Zanzibar kuhusu kujadili,na kuyatatua machangamoto ya kimuungano. Lakini ukweli hadi leo bado ni kioja , na fedha zinaliwa katika kamati na vikao mbali mbali.
Zanzibar ilitaka Kujenga Bandari ya Mpiga duri ,Mkopo wa pesa umezuiwa na waziri wa Mungano na kufanya mradi ule ufe.
Zazibar walianza mchakato wa kuchimba mafuta na Gesi wakati wa Dr.Sheni, lakini Wataalamu walipewa masa 24 kuondoka Tanzania na mchakato wa kampuni ya Ras el khema petroleum, ukafia pale nungwi.
Takriban Miradi mingi ya Zanzibar imelalamikiwa kukwamishwa na Muungano kwa zanzibar kuzuiwa kukopa fedha nje.
Leo Zanzibar wana ZRB ambayo ni mbadala wa TRA ambayo ni ya Muungano. Kuna ZBS ambayo ni mbadala wa TBS na
SUMATRA ya Muungano na Zanzibar wana Sumatra ya kwao.
Hii ni kuonesha kuwa Kuna mvutano ya kimuungano ambayo CCM wenyewe wameshindwa kuitatua.
Munajua sababu nini?
Mimi nadhani ni Mfumo wa MUUNGANO waliojiwekea hauruhusu mabadiliko, kwahiyo CCM wamekwama.
Nadhani sasa ni wakati muafaka kabla ya kuandika kwa katiba mpya Pajadiliwe mfumo muafaka wa Muungano kwanza.
Kuna hatari kuwa endapo chama kingine kisichokuwa CCM kukamata upande mmoja wa Muungano na upande wa pili kuwepo CCM hali itakuwa ni ya Minyukano zaidi. Zanzibar wanataka MAMLAKA KAMILI
Natoa tahadhari. MUUNGANO WETU NI TUNU, LAKINI UNAPASWA UENDANE NA MATAKWA YA WAKATI NA MBADILIKO YA KIFIKRA ZA WADAU NA MAHITAJI.
Nawakilisha
karibuni kwa mjadala