DOKEZO Mfumo wa NEST sasa umekuwa ni jipu, ulianza vizuri lakini sasa kuna dalili za upendeleo

DOKEZO Mfumo wa NEST sasa umekuwa ni jipu, ulianza vizuri lakini sasa kuna dalili za upendeleo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni tenderer kwenye Mfumo wa Kielektroniki wa Manunuzi ya Umma (National - e - Procurement Systemwa - NEST) ambao mwanzoni ulikuwa mzuri kabisa.

Na kama kijana nilihamasika ku-comply ili niweze kuwa naomba kazi za Serikali, ni fani ya Ushauri Mazingira lakini kwa sasa pamekuwa pagumu sana.

Hakuna kazi na hata kazi ikitangazwa anatafutwa mtu, then huyo mtu ana tafuta wa kumsindikiza. Kwa maana ya kwamba wanakuwa invited kwa hiyo wengine hata kama wana uwezo hamuwezi kuiona.

Wataiona wale tu waliokuwa invited wewe utaiona ishakuwa opened na unakuta mtu mmoja ndo ka-apply.

Fuatilia tender nyingi za Consultancy kiukweli zinakatisha tamaa lakini pia, kuna Watu wanachukuwa kazi na hawana vigezo mfano kampuni inatakiwa iwe registered NEMC na pia iwe na practicing license lakini haiwi hivyo.

NEST haiwezi kuitambua kwamba hiyo kampuni iko valid wanatoa tu kazi. Inakatisha tamaa hasa kwa makampuni ambayo yana-comply na kusubiri kufanya kazi kwa weledi.

Asante.

Pia soma
~
PPRA: Inapotokea kuna changamoto ya Mtandao katika Mfumo wa NeST huwa tunasogeza mbele muda wa Tenda
~ PPRA Mtandao wa Manunuzi (NEST) una changamoto sana
 
  • Thanks
Reactions: Nus
Ongeza na maimprest yanasumbua sana kwenye manunuzi kwa sasa kila mtu ni afsa manunuzi, serikali inapigwa vya hatari.
 
Back
Top Bottom