bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 1,213
- 2,938
MFUMO MPYA UNAOLINDA KOREA KASKAZINI DHIDI YA MAADUI ZAKE.
Ulimwengu unajua vyema kuwa katika mikakati ya kijeshi, zipo mbinu maarufu kama "mpango maalum wa kushambulia na kumwondoa kiongozi mkuu wa nchi kwa makombora ya usahihi wa hali ya juu kabla hajapata nafasi ya kutoa amri ya vita.
Katika miaka ya hivi karibuni, sote tulishuhudia jinsi mashambulio hayo yanayo walenga viongozi wa ngazi za juu (precision strikes) yanavyoweza kutekelezwa kwa kasi na shabaha kubwa. Tumeshuhudia Marekani ikifanya kwa Iran, na Israel ikifanya kwa wanamgambo huko palestina na Lebanon.
Lakini je, kwa nini Marekani na washirika wake wanachukua tahadhari kubwa mno wanapoitazama Pyongyang?
Jibu ni rahisi lakini linatisha: Kiduku ametengeneza mfumo ambao pigo lolote dhidi yake linaweza kuweka ulimwengu mzima kwenye hatari kubwa ndani ya dakika chache!
Mwezi Septemba mwaka 2022, Bunge la korea kaskazini lilipitisha rasmi sheria mpya na nzito ya silaha za nyuklia (Law on DPRK Nuclear Forces). Sheria hii iliziba kabisa mwanya wa adui kufanya shambulio la ghafla la kumng'oa kiongozi mkuu:
Sheria hiyo inasema wazi kuwa, ikiwa mfumo wa uongozi mkuu (Command & Control) utashambuliwa, au ikiwa Kim Jong Un atamalizwa, au hata mawasiliano yake yakikatwa ghafla... mifumo ya nyuklia itajiendesha yenyewe kurusha makombora mara moja!
: Kim Jong Un ameshagawa namba za siri za makombora (launch codes) kwa makamanda wa kijeshi wa ngazi za chini waliopo kwenye vituo vya siri vya makombora. Wakibaini uongozi mkuu haupatikani au mawasiliano yamekatika, hawahitaji kibali kingine—mifumo hiyo inaamuru urushaji wa makombora hayo moja kwa moja.
Hii ina maana kwamba shambulio lolote la kumwangusha kiongozi huyu halitazua vita vya nyuklia, bali LITAHAKIKISHA VITA VYENYE MAANGAMIZI MAKUBWA NDIO VINAANZA BILA KUZUILIKA!
Kwa maneno mengine, tofauti na mataifa mengine ambapo kuondoa uongozi mkuu kunavuruga jeshi na kumaliza vita, (Mfano Libya, Iraq
, hata Ivory Coast) huko North Korea, shambulio dhidi ya Kim Jong Un ni sawa na kubonyeza batani ya kujilipua.
Korea kaskazini imeweka uzio wa mwisho wa kijiografia: Mfumo ambao hata ukimshinda mmiliki wake, bado una uwezo wa kukamilisha kazi yake bila yeye kuwepo.