Mfumo wa PEPMIS, Utumishi mmekurupuka kuuleta

Mfumo wa PEPMIS, Utumishi mmekurupuka kuuleta

Kila Jambo linakuwa na nukta ya kuanzia.Naamini wamefanya tathmini ya kina na kuona kwamba sasa ni wakati sahihi kwenda hewani.Changamoto zilizojitokeza naamini wahusika watazifanyia kazi.

Tuwapongeze wenzetu kwa ubunifu wenye lengo la kuongeza ufanisi wa kushughulikia masuala ya kiutumishi kwa Watumishi wa Umma.

Nawasilisha,

Article.
Hakuna kitu pale, siku serikali ikiwekeza kwa dhati kwenye soft infrastructure na kupunguza ubinafsi wataweza. Dunia ya leo hakuna kitu kipya, hakuna ubunifu wowote hapo kwani hii mifumo tayari ipo nchi kadhaa. Hii ni dalili ya upigaji na kwa hulka hii ni lazima hadi Yesu akirudi.
 
Mbona kila kitu walimu wana hali ngumu, ondoa hiyo kitu kwa ubongo wako. Huu ni mfumo kwa watumishi wote wa umma na umeonyesha mapungufu makubwa kama mleta mada alivyosema, hata kwa wahadhiri wa vyuo vikuu imekuwa ni changamoto sana. Msiwafanye walimu kuwa ni sehemu ya kutupia kila taka taka.

Pole sana ToD
 
Huu mfumo unawataka viongozi wawajibike lakini hao mabosi hamna kitu mimi nimejiunga ila sioni kitu maana ilitakiwa nishushiwe task na kiiongozi wangu ila sijui kama hata anajua unafafanaje
Binafsi nawatetea viongozi wa vituo. Utumishi wamewakosea sana na huenda kwa baadhi yao watawasababishia fedheha kwa wafanyakazi wa chini

Baadhi ya watu wakishakuwa viongozi wanapenda kuonekana wao wanajua kila kitu.

Walitakiwa wawape mafunzo ya uhakika wahakikishe wameelewa kabla hata mfumo haujatambulishwa angalau wao wawe tayari na ufahamu nao. Lakini imekuwa kinyume. Yaani wanatakiwa kujifunza kuutumia ukiwa umeshaanza kufanya kazi na hapo hapo wawaelekeze walioko chini yao

Katika hili serikali inaonekana ndio mambo yake. Hebu angalia kinachoendelea kwenye hii ngoma inayoitwa mtaala mpya wa elimu

Wakati walimu bado hawaelewi dubwana la competence based, tayari wanasikia mtaala mpya na hapo nao wanasikia kwenye media kama wananchi wengine

Serikali yetu inaandaa vitu vizuri sana kwenye makaratasi lakini wanakuja kufeli kufikisha kwa implimentazi!

Wao wanajifungia mahali miezi kadhaa wakielimishana (top leaders) inapofika kuleta kwa wanaohusika huku field wanapiga bla bla za hapa na pale wanaenda kwenye media kulipablishi na kazi inakuwa imeishia hapo hapo baada ya siku kadhaa jambo linakosa morali kwa wanaotakiwa kulitekeleza sio kwasababu ni baya ila tu kwasababu hawakulielewa vizuri jambo lenyewe ili waweze kulimiliki kama lao
 
Mfumo wa PEPMIS aka PEPSI ni mzuri kwa nchi zilizoendelea ambako kuna internet ya kumwaga kila kona. Lakini pia watumiaji wanatakiwa wawe na uelewa mkubwa kwenye TEHAMA na computer applications kwa ujumla.
Nchi yetu ina shida kwenye suala la upatikanaji wa mtandao na uelewa kwenye matumizi ya computer na smartphones upo chini. Kwa sababu hizi basi, PEPMIS ni shida tu.
 
Teacher on duty
Nyie vijana mna tabu sana, ningekuwa Mwl ningejisikia fahari sana. Sasa home of great thinkers wao kila kitu ni Mwl, huu mfumo wa PEPMIS umeleta usumbufu kwa watumishi wote.
 
Mfumo wa PEPMIS aka PEPSI ni mzuri kwa nchi zilizoendelea ambako kuna internet ya kumwaga kila kona. Lakini pia watumiaji wanatakiwa wawe na uelewa mkubwa kwenye TEHAMA na computer applications kwa ujumla.
Nchi yetu ina shida kwenye suala la upatikanaji wa mtandao na uelewa kwenye matumizi ya computer na smartphones upo chini. Kwa sababu hizi basi, PEPMIS ni shida tu.
Waruhusu Elon musk alete star link tz mtandao unasumbua sana
 
Serikali ilipiga hesabu kama kishikwambi kilituma taarifa za sensa na ni kijiji lazima na ww mwalimu utatuma tu wanasahau mawakala wa sensa walikuwa wanaenda sehemu yenye mtandao ndo wanatuma
Vishikwambi vipi tena??? Vishkwambi vililetwa kwa ajili ya sensa na kazi ilivyoisha vingi vilikufa kibudu... Nenda katika shule moja yoyote katika walimu 10 wenye vidhikwambi ni vishkwambi viwili au kimoja ndio vizima
 
Back
Top Bottom