Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Unajua kuwa leseni yako ya udereva ina pointi 15, ambazo zinaweza kupunguzwa kutokana na makosa ya barabarani?
Hapa Advocate Witness Manase anaeleza zaidi namna unavyofanya kazi
Kwa mujibu wa The Road Traffic (Drivers Licence Point System) Regulations, 2014, G.N. No. 109 of 2014, zilizofanyiwa marekebisho kupitia G.N. No. 420 of 2025, dereva anaweza kupunguziwa pointi 1 au 3, kulingana na aina ya kosa alilofanya.
Kwa mujibu wa Kanuni hizo, endapo pointi za dereva zitafikia sifuri, leseni yake inaweza kusimamishwa kwa kipindi cha miezi sita. Kukatwa pointi hakumuondolei dereva faini au adhabu nyingine inayotokana na kosa husika.
Hata hivyo, mfumo huo haujaanza kutekelezwa rasmi. Tarehe 29 Septemba 2026, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alielekeza mfumo huo usitishwe kwa muda ili kufanyiwa tathmini ya kina.
Tathmini hiyo itahusisha madereva kupitia viongozi wao pamoja na wadau wengine. Pia itazingatia elimu na uhamasishaji wa umma, maoni ya wadau, pamoja na namna mifumo ya usalama barabarani inavyotekelezwa katika nchi nyingine, kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi.