Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 525
- 2,950
Dahhhh
Hizi not selected zinachanganya mnoMi naona wangewaboreshea pia kujua kama upo kwenye hiyo Database au bank
Umefatilia na kuona hawajafanya hvy?Mi naona wangewaboreshea pia kujua kama upo kwenye hiyo Database au bank
Huoni databank isipokuwa na expire date itakuwa tatizo zaidi, wahitimu wapya hawatapata fulsa ya kuingia kwenye usaili watakuwa wanachukuliwa wale waliohifadhiwa kwenye database tu hadi waishe sio leo.THE VICIOUS CYCLE OF YOUTH UNEMPLOYABILITY.
Naomba leo nizungumze na mamlaka ya Serikali Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma chini ya Waziri Mhe. Ridhiwani Kikwete, pia Sekretarieti Ya Ajira.
Kuna mfumo upo kwenye Ajira Portal unaitwa "Data Bank". Mfumo huu upo kwa mujibu wa kanuni (Principal Rule) GN 322 ya 2021 kanuni ya 22(1),(2),(3),(4) na Kanuni (Amended Rule )GN 579 ya 2022 Kanuni ya 22(5).
Ajira zinapotangazwa huwa kuna idadi ya nafasi zinazohitajika,ila kulingana na tatizo la ukosefu wa Ajira kuwa kubwa, Vijana wengi hujitokeza kwenye usaili na hatimaye wengi wanafaulu (Both Written and Oral Interviews) ukilinganisha na uchache wa nafasi.
Kama nafasi ni 200, unakuta waliojitokeza ni 1000 na waliofaulu ni 350, hivyo kinachofanyika katika hao 350 wanachukuliwa 200 na 150 wanahifadhiwa kwenye Data Bank (Passed and Stored into Data bank) kwa ajili ya kuajiriwa moja kwa moja bila usaili ikiwa nafasi zitajitokeza.
Changamoto ipo hapo kwa Vijana waliofaulu na kuwekwa kwenye Data Bank, Kanuni(Amended Rule )GN 579 ya 2022 kanuni ya 22(5)inasema watadumu kwa muda wa Mwaka mmoja tuu kama hakuna nafasi zilizotangazwa Data bank ina expire kama bidhaa sokoni.
Hivyo, watatakiwa kufanya usaili tena. Mfumo huu ni mzuri ila una changamoto kadhaa.
Moja, hakuna haja ya Data Bank ku expire sababu maarifa na uwezo wa mtu hauwezi ku expire kama bidhaa sokoni.
Ninapendekeza kanuni ziondoe expire au iwe miaka 2, nchi kama Canada na nchi nyingi wana huu mfumo wanaita Reserve Pools/Qualified pools hawana expire bali wanawaajiri muda wowote nafasi za taaluma zao zinapojitokeza.
Mfano, Nchini kwetu Septemba 2024 nafasi za kada ya Afya na Elimu zilitangazwa,wapo Vijana waliofaulu wakawekwa Data-Bank ila ilipofika Septemba 2025 wakaambiwa wame expire ila mwezi uliofuata Oktoba 2025 nafasi za kada ya Afya na Ualimu zikatangazwa, Vijana wale wa Data Bank wakaomba tena wakakosa na kutupwa nje wakiambiwa wamefeli.
Ni kama kuna kuviziana na kukomoana, jambo ambalo si sahihi na kinachotokea ni kama huo mchoro wa circle juu.
Mfumo huu uangaliwe upya na jina libadilishwe isiitwe DATABANK, uitwe"RESERVE POOLS" labda itasaidia badili mindset za wenye mamlaka.
Mwisho, Serikali iweke kipaumbele kuajiri Vijana na itengeneze mazingira bora kwa sekta binafsi ili kusaidia kuajiri, na mazingira bora ya uwezeshaji Vijana kujiajiri.
Kwani hali ni mbaya, kwa takwimu nchini kwetu Tanzania kwa mujibu wa ILFS (Integrated Labour Force Survey, 2021) na sera ya Maendeleo ya Vijana ya 2007 toleo la 2024 inasema kwa Mwaka Vijana Milioni Moja huingia kwenye soko la ajira ila ni Vijana laki mbili tuu ndio hupata ajira sekta rasmi aidha sekta ya umma au binafsi.
Huku Vijana laki 8 wakiachwa nje na kwa taarifa ya TCU kila mwaka wahitimu takribani elfu 60 wanamaliza vyuo vikuu, mfano Nchini kwetu hadi sasa tuna uhaba wa walimu 279,202 huku Mtaani kukiwa na Vijana wahitimu walimu wengi sana bila ajira, huku ajira za Serikali za Serikali zikiwa chache sana.
Changamoto hii huongeza Vijana Mtaani, na kupanua ukuaji wa shughuli zisizo rasmi kwa Vijana. Hadi sasa nchini kwetu shughuli siziso rasmi ni 80%. Ni muhimu mambo haya kuangaliwa vyema.
View attachment 3682453
Abdul Nondo.
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa -ACT Wazalendo .
02/Oktoba/2026.
Gharama walizotumia utawarudishia wewe au ndio unaleta mambo ya Kamali unabet na Maisha ya watu sio?Huoni databank isipokuwa na expire date itakuwa tatizo zaidi, wahitimu wapya hawatapata fulsa ya kuingia kwenye usaili watakuwa wanachukuliwa wale waliohifadhiwa kwenye database tu hadi waishe sio leo.
Ni vyema databank iendelee kuwa ya mwaka mmoja hivyohivyo ili kutoa fulsa kwa wahitimu wapya kupambania fulsa ya ajira.
Ww n mpumbavu na huna akili, unachojua n kulalamika bila kufatilia mambo.Gharama walizotumia utawarudishia wewe au ndio unaleta mambo ya Kamali unabet na Maisha ya watu sio? Yaan watu hawajijui km wapo kwenye hio databank hilo tatizo la kwanza ukituma maombi unapata notification ipo pale inasoma "application received" ukipasua written inasoma "selected for Practical/Oral" ukipasua Oral kwanini haiandiki km umepasua na haujui chochote mpaka pdf itoke na ikitoka hujui chochote tena km upo kwenye databank au upo wapi maana hakuna notification yoyote pale inayokuonyesha kwamba "your in a databank" ili vijana wapumue. Na hio muda ya miezi 12 ni mfupi saana ilibidi iwe hata miaka 3½ angalau kidogo, hakuna kuwazuia wengine ila kuna kua na huakika wa vijana kupata ajira kuliko kurudia rudia jambo lile kila baada ya miezi 12 na wakati ulishafaulu inakua km unacheza Kamali
Upo sahihi mzeeGharama walizotumia utawarudishia wewe au ndio unaleta mambo ya Kamali unabet na Maisha ya watu sio?
Yaan watu hawajijui km wapo kwenye hio databank hilo tatizo la kwanza, mfano rahisi ukituma maombi unapata notification ipo pale inasoma "application received" ukipasua written inasoma "selected for Practical/Oral" ukipasua Oral kwanini haiandiki chochote inakua tu kimya km umepasua na haujui chochote mpaka pdf itoke na ikitoka na jina lako halipo hujui chochote tena km upo kwenye databank au upo wapi maana hakuna notification yoyote pale inayokuonyesha kwamba "your in a databank" ili vijana wapumue.
Hilo ni tatizo kubwa sana ambalo hao jamaa wa ajira aidha wanalijua na wanafanya makusudi kutokulifanyia kazi au wanalijua ila hawataki kulifanyia kazi kwa maslahi yao binafsi.
Na hilo suala la muda ya miezi 12 hili ni tatizo la pili kwa sababu muda ni mfupi saana ilibidi iwe hata miaka 3½ angalau kidogo, hakuna kuwazuia wengine ila kuna kua na uhakika wa vijana kupata ajira kuliko kurudia rudia jambo lile kila baada ya miezi 12 na wakati ulishafaulu inakua km unacheza Kamali
Sio kulalamika, watu wametoa pesa kuenda sehemu za kufanyia usahili, wengine wakakodi vyumba, kula na muda, iweje isiwe sababu ya msingi wao kuendelea kutambulika kwenye mfumo!!?Ww n mpumbavu na huna akili, unachojua n kulalamika bila kufatilia mambo.
Upo nyuma sana.Gharama walizotumia utawarudishia wewe au ndio unaleta mambo ya Kamali unabet na Maisha ya watu sio?
Yaan watu hawajijui km wapo kwenye hio databank hilo tatizo la kwanza, mfano rahisi ukituma maombi unapata notification ipo pale inasoma "application received" ukipasua written inasoma "selected for Practical/Oral" ukipasua Oral kwanini haiandiki chochote inakua tu kimya km umepasua na haujui chochote mpaka pdf itoke na ikitoka na jina lako halipo hujui chochote tena km upo kwenye databank au upo wapi maana hakuna notification yoyote pale inayokuonyesha kwamba "your in a databank" ili vijana wapumue.
Hilo ni tatizo kubwa sana ambalo hao jamaa wa ajira aidha wanalijua na wanafanya makusudi kutokulifanyia kazi au wanalijua ila hawataki kulifanyia kazi kwa maslahi yao binafsi.
Na hilo suala la muda ya miezi 12 hili ni tatizo la pili kwa sababu muda ni mfupi saana ilibidi iwe hata miaka 3½ angalau kidogo, hakuna kuwazuia wengine ila kuna kua na uhakika wa vijana kupata ajira kuliko kurudia rudia jambo lile kila baada ya miezi 12 na wakati ulishafaulu inakua km unacheza Kamali
Siwezi kufuatilia mi sasa hivi nafikiria retirementUmefatilia na kuona hawajafanya hvy?
Bc Tulia acha wenge, subir mafao ule.Siwezi kufuatilia mi sasa hivi nafikiria retirement
Mwenye Wenge anayetembeza bahasha mtaani siyo mimi mi Principal sasa nimeshamaliza rank zote kwenye utumishi wa ummaBc Tulia acha wenge, subir mafao ule.