KERO Mfumo wa SOMA wa DIT ni kero kwa wanafunzi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mwanafunzi wa DIT, tunatumia mfumo unaitwa SOMA katika usajili na ufatiliaji wa matokeo.

Kwa zaidi ya mwezi sasa mfumo umekuwa na changamoto, Huku baadhi ya wanafunzi wakiwa NOT PROMOTED
baada ya kufuatilia ADMISSION OFFICE tulipewa Ticket Number ili kuhudumiwa na SOMA hata hivyo Ofisi za SOMA hufungwa kila siku, Huku mmoja wao akituelekeza wao hawahusiki na Changamoto za wanafunzi, TURUDI TUFUATILIE KWA ALIYETUPA TICKET NUMBER.

Hatuelewi ni Ofis ipi tuende maana tayari taasisi imetoa NOTCE wale wote ambao bado hawako registered wapostpond mitihani au masomo, Kwa jambo ambalo ilikiwa ni Tatizo la kimfumo.

Taraehe 9, Mitihani ya UE inaanza, wengine hatujui hata itakuaje maana mifumo haifanyi kazi.


 
elimu ya bongo kichomi sana. yani chuo cha teknolojia kinashindwa kufanya mambo madogomadogo ya teknolojia husika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…