Mfumo wa TEHAMA watetereka dunia nzima baada ya Kampuni ya Microsoft kupata changamoto kwenye mifumo yako

Na waliomshangaa mleta mada pia wana akili ndogo, au skuli walienda kukariri.
1) Amelenga kuweka utayari wa kumsikiliza yeye kwa atakachotaka kukiwasilisha.
2)ameamua tu kwa makusudi kutumia ile kauli ya if you fail to convince them confuse them.
3) Amelenga kuwasumbua kwa makusudi ili mtoe ya moyoni.

Na hamna zaidi ya hapo
 
Aah! Hii inanikumbusha watch Dogs. Humu kwetu hata serikali inatumia cracked windows kutoka getintopc. Ukichangia bei za bando, means hakuna mtu mwenye ubavu wa kufanya updates za Bill Gates.

We cool out here!
 
Hiyo ndo yaitwa digital pandemic na imeathiri mifumo yote ya tehama inotumia software za Windows khasa Operating Systems na 365 Apps..

Hiyo kampuni ya Crowdstrike ndo yenye mikataba na makampuni mengi duniani na leo wamekiri kusababisha tatizo la kiufundi pale walipokuwa wakifanya updates.

Crowdstrike wana makao makuu mjini Austin katika jimbo la Texas na kwa bahati mbaya makampuni na mashirika makubwa ya ndege kama la American Airline leo ilibidi wasirushe ndege zao.

Crowdstrike ina mikataba na makampuni zaidi ya 24,000 duniani kote ikiwemo Microsoft wenyewe na kazi yao kubwa ni kufanya analysis kwenye mifumo ya Tehama kubaini matatizo yoyote yanosababishwa na mashambulizi ya kwenye mitandao au "Cyber Attacks".

Si tu mifumo ya tehama pia wazingalia simu za mikononi khasa Apple, Samsung na vifaa vingine vya kieletroniki.

Kwenye soko la hisa leo Crowdstrike imefungua soko ikiwa asilimia 15 chini na tayari imepoteza dola bilioni 12.5.

Kwa kuwa Windows yatumiwa duniani kote hili tatizo limeathiri kwa kiwango kikubwa uchumi wa Dunia.

Sasa nini kimetokea?

CrowdStrike ambao wana wajibu wa kulinda mifumo ya tehama waliingiza App moja ili ifanye kazi kwenye mifumo hiyo lakini App hiyo haikuwa sawa (au twasema ilikuwa Corrupted) hivyo ikazua tatizo jingine la kusimamisha mifumo ya tehama iliyopo kwenye majumba ya kuhifadhia mfumo ya tehama au "Crowd Computing".

Hivyo mhandisi alieandika "Code" moja kwenye kufanya update akakosea maandishi ya Code hiyo na ndipo balaa lilipozuka na hiyo huitwa "Faulty Update".

Hivyo hapa ndipo kwa wataalam wa IT khasa katika nchi zetu kuangalia faida na hasara ya mifumo ya Cloud Computing ya SaaS na PaaS.

SaaS (Software as a Service) ni pale unapoingia mkataba na watu kama wa Crowdstrike lakini weye watumia tu Software zao na wao ndo wafanyao Updates na software zote bado ni zao. Mfano wa Software hizo ni Office 365 ambayo kwa sasa Microsoft hukuazima na weye kulipa kwa mwezi au mwaka lakini huimiliki software hiyo.

PaaS (Platform as a Service) ni pale wanapokupatia software na hardware zote na weye hulipa fee tu kwa kutumia mali zao.

Hivyo kongole kwa makampuni ambayo yapo hata Tanzania na yanalipa kila kitu kuwa ni chao.
 
Mifumo ya kibank ndo imepata hyo kadhia
Mifumo ya banks, maduka, viwanja vya ndege, mahospitali, migahawa khasa Mac Di, Apps za kufanyia malipo, Payroll systems, maduka ya kubeti na taxis khasa za New York, pamoja na supermarkets.
 
Dunia bila mifumo, tunarudi ujima fasta...
 
Dunia bila mifumo, tunarudi ujima fasta...
Ni lazima kuwepo Resilience and Continuity.

Crowdstrike ndo wategemewa kufix tatizo hili.

Ila Mac na Linux ndo mifumo bora kwa sasa ingawa ni ghali sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…