Mfumo wa ufundishaji wa masomo ya Tehama kwa Vyuo Vikuu ubadilishwe

Mfumo wa ufundishaji wa masomo ya Tehama kwa Vyuo Vikuu ubadilishwe

kelvin bayona

Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
16
Reaction score
8
Nchi yangu ya Tanzania kama inatamani kupiga hatua zaidi kwenye maendeleo ya tekinologia inapaswa kuangalia zaidi suala la elimu inayotolewa na vyuo haswa vya umma.

Unakuta mwanafunzi anamaliza shahada yake ya masomo akiwa anachukua masomo ya tehama lakini hakuna kitu alichotoka nacho kichwani ambacho anaweza kukifanya kwa vitendo, vyuo vingi vinafundisha kwa maneno tu nakupewa vitabu vya kwenda kupitia lakini hakuna vitendo.

Kama tunavyojua kuna wakati vyuo utoa nafasi kwa wanafunzi wake kwenda kufanya kazi kwa vitendo kile walichokisomea darasani(filidi) unakuta mwanafunzi kaletewa pale kompyuta aiunganishe labda ni mpya anashindwa pakuanzia, mimi binafsi na marafiki zangu tumepeta nafasi ya kwenda kufanya kazi kwa vitendo lakini kwenye hiyo taasisi tulipoenda kipindi chote hatukufanya kazi ya maana kwa sababu tulikuwa tunaulizwa mnaweza kufanya hiki tunajibu hapana lakini tunakumbuka mwalimu alitufundisha ubaoni na akatupa notisi zakwenda kusoma lakini hatukufanya kwa vitendo.

Hili tatizo litapelekea vyuo kukosa sifa za kuwa vyuo na vitajikuta vinatoa elimu kama wanayopata wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa sababu wanakeremishwa tu.

USHAURI
1. Serikali ione haja ya kuanzisha vyuo vitakavyokuwa vinatoa mafundisho yanayohusu tehema tu visichanganye na masomo mengine na hivyo vyuo viwe na kila dhana mfani kompyuta, upatikanaji wa mtandao, kila mwanafunzi kuwa na compyuta yake binafsi etc, hili litasaidia mwanafunzi kuwasa swala analolisomea tu tofauti na saizi unakuta mwanafunzi anasomea tehama lakini humo humo anafundishwa masomo ya biashara humo humo anafundishwa mambo ya sheria.

2. Hili litalenga vyuo husika kuweka mitaara yake vizuri. Mfano unakuta kuna somo limegawanywa mara 2, (Networking 1 na networking 2) hapa ilo la (networking 1) mwanafunzi atafundishwa muhura wa kwanza, hilo la (networking 2) atakuja kufundishwa muhura wa tatu lakini ukija kuangalia haya masomo yanategemeana kwamba ulipoishia (networking 1) ndipo mwendelezo wa (networking 2) huyu mwanafunzi lazima aferi sababu itabidi akumbuke alipoishia (networking 1) huko muhura wa kwanza. Kwahiyo vyuo viwe vinaunganisha masomo kam hayo kwamba ukifunguq tu muhura wa pili uendeleze pale pale ulipoishia.

3. Pia kila chuo kinachotoa elimu ya tehama kuhakikisha kila madarasa maalumu kwa ajiri ya wanafunzi kusoma kwa vitendo wakati wanafundishwa au kwa mda wao wenyewe, hili litaongeza ubunifu kwa hawa wanafunzi ambao wanakuwa wanafanya kwa vitendo mara kwa mara, kwa sababu naamini masomo ya tehama hayana utafauti na masomo ya udaktari lazima mwanafunzi afundishwe kwa vitendo ndipo ataelewa kitu gana anapaswa akifanye kwa wakati gani.
 
Back
Top Bottom