Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 7,093
- 10,469
Hakuna kingine communism inafanya isipokuwa kuwahudumia politiburo, mfumo wa Tanzania haukuundwa kujali mtu wa kawaida bali ni kwa ajili ya wale walio juu na hilo ni kuanzia Serikalini, Mashirika mpaka Polisi na Jeshini, ukiwa mkubwa matatizo hayakuhusu, na na ndiyo maana Ujamaa au moja kati ya sababu za Ujamaa kushindwa.
Watu wengi hujiuliza kwa nini Mashirika ya Tanzania yalikufa? Sababu ni corruption na kingine kuhudumia wakubwa na familia zao, kuna wakati kila bosi alikuwa na magari ya Shirika 2/3 moja la kwake, lingine la mke wake kumpeleka saluni na lingine kupeleka watoto shuleni yote haya yalilipiwa na Shirika, na ndio maana Watoto wao wanafanya wanavyotaka.
Kama ulishawahi kuwa na Mzazi au hata ndugu wa karibu mwenye Cheo Serikalini au Shirika la Umma utaelewa ninachokiongelea. Fikiria raisi mstaafu bado anajengewa Villa na Serikali pamoja na yote anayopewa, ukiona pension wanazolipana wakubwa baada ya kustaafu utashangaa, achilia mbali magari na mpaka nyumba wanapeana zawadi, sasa ukijumlisha idadi yao na ndugu zao hakuna hela itabakia kwa wengine.
Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo Wananchi wanasubiri Serikali itangaze ajira!