TheForgotten Genious
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 2,087
- 3,156
Utangulizi
Dunia ya sasa teknolojia haikwepeki. Afrika ina watu wengi ila wenye weledi ni wachache, tuna watu wanaojiibia wenyewe kitu kinachopelekea sekta nyingi kuwa shagala bagala sababu ya utendaji mbovu.
Ni ngumu sana kupambana na rushwa kwa askari wa usalama barabarani kwa kutumia TAKUKURU (japo TAKUKURU wanafanya kazi nzuri) na tukafanikiwa. Dawa ni kutumia mifumo ambayo haiwezi kuomba ama kupokea RUSHWA.
Mf. katika mfumo huu ASKARI hawatahusika ktk suala zima la kusimamia sheria za barabarani hivyo hivyo inamtengenezea mipaka ya kuomba RUSHWA.
Huu mfumo ni complex ndio lakini kama tutakuwa serious unatekelezeka ndani ya miaka 5 tu maana ni vifaa vichache ambavyo vinahitaji kuundwa, vingi vipo sokoni na programming ndio inatumika kutoa muongozo kwa system nzima.
Kielelezo.1: Ajali kati ya basi la mwendo kasi na bodaboda . Chanzo: Daily News Digital
Mfumo unalenga kutatua changamoto zote za kiusalama na weledi barabarani kama vile;
Huusisha mifumo miwili ambayo ni Gridi na dharura (jua) mifumo hii itabadirishana kupitia swichi maalumu kutoka gridi kwenda jua na jua kurudi gridi pale unapokatika na kurejea, Lengo ni kuhakikisha nishati inapatikana muda wote.
Mfumo simamizi wa mwendokasi
Utapima mwendo kasi wa kifaa cha moto,utaundwa na kamera za kutambua mwendo kasi zitwazo “Speed Camera”(SC) na kutuma taarifa katika mfumo wa kati kwa ajili ya uchakataji.
SC Zitafungwa katika makutano ya barabara na katika Intelligent Car Monitoring kit (ICMK).
kielelezo.2: Mpangilio wa mfumo katika mzunguko wa Barabara.
Mfumo tambuzi wa foleni
utakabiliana na foleni za magari kwa kutambua idadi ya magari katika kila barabara kuanzia kwenye makutano ya barabara.
Utaundwa na “Traffic Sensor Camera(TSC)” ambazo zitatambua uwepo wa gari katika kila barabara iliko elekezwa,idadi itategemea idadi ya barabara zilizo kutana.
Pia itatumika kama swichi ya RF MODULE katika mfumo wa makutano ya barabara kwa ajili ya uzalishaji wa mawimbi ya redio yatakayowezesha kutambua idadi ya magari katika kila barabara,pia itatumika kama muongozo wa muelekeo wa mawimbi yaliyozalishwa.
“Transmitter” itazalisha na kutuma mawimbi kwa msaada ya antenna na kupokelewa na “Receiver” ya RF Module iliyopo kwenye ICMK ya chombo cha moto na kusababisha RF module katika makutano ya barabara kuzima na transmitter ya RF MODULE katika ICMK kuzalisha mawimbi na kutuma ambayo yatapokelewa na “Receiver” ya RF MODULE katika ICMK ya gari nyingine,mzunguko kamili ni kati ya “Receive (R)” na “Transmit (T)” katika RF Module,ambapo RF Module ya ICMK moja ikipokea na kutuma mawimbi iCPU itatambua “1” huku mfumo ukijumlisha kila hatua.
Mawimbi yatasetiwa kusafiri umbali flani ambao yakifikia umbali huo bila kupokelewa, iCPU itatambua “0” na kujumlisha “1” zote,kisha kuoanisha na idadi za magari katika barabara nyingine na kuruhusu barabara yenye idadi kubwa ya magari kwa mtiririko kwa kuwasha taa ya kijani.
Kielelezo.3: Mpangilio wa mfumo katika makutano ya njia nne.
Taa za usalama barababarani.
Zitaongoza vyombo vya moto na waenda kwa miguu katika maeneo ya makutano ya barabara na vivuko, zitakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na mfumo tambuzi wa foleni barabarani nawa dharura.
Mfumo wa dharura.
Utatumika pale tukio maalumu lisilohitaji muingiliano wowote kama vile misafara ya viongozi,na gari za wagonjwa.
kutakuwa na kioo kitakacho onesha tukio na muda ambao litadumu ambacho kitafungwa katika makutano ya barabara(Tazama kielelezo .3 ,sehemu "E").
Polisi watawasiliana na wasimamizi wa msafara juu ya njia watakayo itumia na kupitia mfumo wa kompyuta wataseti muda utakaotumika kukamilisha msafara huo na mfumo utaruhusu taa za barabara zote kuwaka nyekundu isipokuwa barabara ambayo itatumiwa itawaka kijani,muda ukiisha mfumo utaendelea na majukumu yake katika sehemu zote ambazo njia zilifungwa.
Taarifa hii itaonekana pia katika programu ya simu ili kuwezesha kila mtu kujua.
Mfumo tambuzi wa alama za barabarani.
utaundwa na Red light camera (RLC), Automated number plate recognition (ANPR).
RLC ni kamera zinazotumia akili mnemba kusoma alama za barabarani na kuzichakata kwa kuoanisha kanuni na sheria za barabarani,ikitokea dereva kakosea kamera hii itapiga picha na kuchakatwa na iCPU na mfumo wa malipo utatengeneza stakabadhi ambayo muhusika atapata ujumbe wa maandishi kwa njia ya simu na katika programu ya simu.
ANPR itafanya kazi ya kuzisoma nambari za gari punde baada ya RLC kugundua kosa na kabla ya kupiga picha.
Kielelezo.4: Jinsi ambavyo RLC inafanya kazi.
Chanzo: Road Safety ,By Chequanlaosi
“Intelligent car monitoring kit”
Hiki ni kifaa maalumu kwa ajili ya kufuatailia mwenendo wa vifaa vya moto na mwenendo wa dereva,kitafungwa katika magari na pikipiki.
Itaundwa na Speed Camera(SC),Red light Camera(RLC) na Driver monitoring Camera (DMC) kwa upande wa magari na SC na RLC kwa pikipiki,Sensa ya kutambua kileo kwa dereva, na iCPU ambayo itachakata taarifa zote zinazoingia na kutoka katika kiti
SC na RLC zitafanya kazi kama ilivyoelezwa hapo awali DMC itachunguza mwenendo wa dereva kama vile kutumia simu wakati anaendesha gari na uivei,itaunganishwa na "Alcohol Sensor"pamoja na "Buzzer" na itapachikwa kwenye kioo cha mbele cha gari ikimtazama dereva.
Kielelezo.5
Itakuwa na “RF module” kwa ajili ya kupokea na kutuma mawimbi ya Redio ili kugundua idadi ya magari ili kukabiliana na foleni kama ilivyo elezwa hapo awali, na kutambua uwepo wa gari upande wa pili wa barabara hasa katika maeneo yenye kona kali ambapo mawimbi yatatumwa na kupokelewa,iCPU itachakata muda uliotumika na mawimbi kusafiri na kupokelewa upande wa pili kisha kutambua umbali kati ya gari na gari.
kutakuwa na muda ambao utasetiwa utakaotambuliwa kama “Safe time” ambao ikitokea muda uliotumika na mawimbi kusafiri na kupokelewa ukawa chini ya huo muda buzzer itatoa sauti kumtahadharisha dereva.
Itakuwa na GPS Module kwa ajili ya kuonesha maeneo ambayo kifaa cha moto kipo,hii itasaidia kuzuia uhalifu unaohusisha vyombo vya moto,kuwapata wahalifu pamoja na wale walio kwepa faini,kuonesha ni wapi chombo cha moto kimesababisha ajari au kupata ajari,na kujua ni eneo gani dereva alifanya kosa lililopelekea mfumo umtoze faini.
Programu ya simu
Itatumiwa na madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kupata na kutoa taarifa muhimu kama vile faini,uwepo wa foleni mbele au kufungwa kwa barabara kutokana na sababu mbalimbali pia kufanya malipo mbalimbali.
Pia itatumiwa na madereva kuripoti ajali.
Mfumo endeshi wa kompyuta
Ni mfumo ongozi wa mifumo mingine.Mfumo huu ndio utakao tumiwa na polisi wa usalama barabarani kujua mambo mbalimbali yanayoripotiwa na mifumo mingine.
Kanzi data
Ita hifadhi taarifa zote zinazohusiana na mwenendo wa usalama barabara,taarifa za vyombo vya moto kama vile bili ambazo hazijalipiwa,usajiri,bima nk.
Mfumo wa malipo
utatumika kufanya malipo mbalimbali kama vile faini za makosa yaliyogunduliwa.Utaruhusu mtu kufanya malipo kwa njia Zote.
Chumba ongozi cha mfumo wa usalama barabarani.
Ni chumba cha mawasiliano kikionesha sehemu za mifumo ya usalama barabarani na utendaji kazi wake ili kutambua na kutatua tatizo pale linapotokea,kitaongozwa na wataalamu wa mifumo ya mawasiliano kutoka jeshi la polisi.
Kielelezo.6
Polisi hawataruhusiwa kutekeleza majukumu yanayotekelezwa na mfumo.
Dunia ya sasa teknolojia haikwepeki. Afrika ina watu wengi ila wenye weledi ni wachache, tuna watu wanaojiibia wenyewe kitu kinachopelekea sekta nyingi kuwa shagala bagala sababu ya utendaji mbovu.
Ni ngumu sana kupambana na rushwa kwa askari wa usalama barabarani kwa kutumia TAKUKURU (japo TAKUKURU wanafanya kazi nzuri) na tukafanikiwa. Dawa ni kutumia mifumo ambayo haiwezi kuomba ama kupokea RUSHWA.
Mf. katika mfumo huu ASKARI hawatahusika ktk suala zima la kusimamia sheria za barabarani hivyo hivyo inamtengenezea mipaka ya kuomba RUSHWA.
Huu mfumo ni complex ndio lakini kama tutakuwa serious unatekelezeka ndani ya miaka 5 tu maana ni vifaa vichache ambavyo vinahitaji kuundwa, vingi vipo sokoni na programming ndio inatumika kutoa muongozo kwa system nzima.
Kielelezo.1: Ajali kati ya basi la mwendo kasi na bodaboda . Chanzo: Daily News Digital
Mfumo unalenga kutatua changamoto zote za kiusalama na weledi barabarani kama vile;
- Foleni
- Rushwa.
- Ajali.
MUUNDO NA UTENDAJI KAZI WA MFUMO.
Mfumo wa umeme.Huusisha mifumo miwili ambayo ni Gridi na dharura (jua) mifumo hii itabadirishana kupitia swichi maalumu kutoka gridi kwenda jua na jua kurudi gridi pale unapokatika na kurejea, Lengo ni kuhakikisha nishati inapatikana muda wote.

Upvote
2