NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Naomba nisieleweke vibaya nashare tu mtazamo wangu ili kuboresha na kuwa na taifa bora zaidi lenye uwezo wa kutatua matatizo yake kwa kutumia wataalamu wake.
Mfumo wetu wa elimu huko hivi unamchukua samaki na ndege aina ya tai alafu unawapa mtihani mmoja. Yaani unampima samaki kwa kupaa juu na tai unamuingiza baharini ili aogelee. Mwisho wa siku wote wanafeli alafu unahisi hawana akili kumbe umetumia vipimo visivyo sahihi.
Mfumo wetu wa elimu unatulazimisha tuwe watu wa kukariri zaidi kuliko kuelewa.
Tunapokuwa watu wa kukariri tunajikuta tunasoma kwa ajili ya kufaulu mitihani na sio kuelewa. Ukishafanya mtihani kila ulichokariri kinafutika.
Mtihani mwingine ukija inakubidi ukariri tena. Basi huo mzunguko unaendelea tena na tena na tena.
Tuna uwezo wa kuwa wavumbuzi lakini sasa unakuwaje mvumbuzi wakati elimu yako yote toka msingi mpaka ngazi uliyopo sasa umefaulu vema sio kwa sababu ulikuwa ukielewa sana lakini kwa sababu ulikuwa unakariri vema.
Kukariri kunakuwezesha kutoa copy ya ulichofundishwa.
Kuelewa kunakuwezesha kutumia ulichofundishwa kuleta mabadiliko. Huwezi kuapply kile ambacho hujaelewa.
Huwezi kufanya innovation kwa maarifa uliyokariri. Innovation inafanywa na maarifa uliyoyaelewa.
Huwezi kuwa creative wakati elimu yako ni elimu kariri.
Creativity inazaliwa kutoka kwenye elimu uliyoelewa.
Mungu tusaidie tuelewe sio tukariri. Mungu ibariki Tanzania.