Mfumuko wa bei ni utekelezaji wa ilani ya CCM?

Mfumuko wa bei ni utekelezaji wa ilani ya CCM?

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Shaka anazungumza kwa uwazi kwamba Mwenyekiti wa CCM Taifa ameifungua nchi.

Anazunguka duniani kuipaisha Tanzania.

Ziara za Rais zimetuzawadia deni la Taifa kufikia Trillion 71+ mpaka sasa.

Shaka anataja mafanikio mengi yatokanayo na utekelezwaji wa ilani ya CCM.

Sasa hivi bidhaa muhimu hazishikiki sokoni. Bei imepanda na inaendelea kupanda maradufu.

Je, hili la mfumuko wa bei ni utekelezaji wa ilani ya CCM?

Uoga wetu
 
Hili deni mmeanza kumtwisha Samia?

Aliekopa hela nyinyi kimyaa kimyaa hamumjui?Samia ndo kaleta deni la trilioni 71?...hamnaga aibu mkiamua kumchafua mtu?
 
Kumjadili Shaka ni kupoteza mda tu, ni bahati mbaya Sana kwamba ccm ndo wanachama iliyowatengeneza, watu wanasifia mpaka ujinga.

Tunasemaga sio KILA mtu anaweza kuwa rais, nafikili mnaona ni namna gani uyu mama Mambo yanavyomwendea, ni kama mifumo ya nchi imecolapse, watu wanajiibia tu, yeye ni kusafili tu, na wahuni Sio watu wazuri wanajua kusifia Sana, hii ni mbaya sana.
 
Wamefikia ukomo namna ya kuongoza kwa ueledi kilichobaki kwao ni mipango ya kuendelea kutawala .

Hawana jipya mbaya zaidi na sisi wananchi tumekuwa kama makalia yanayotumiwa na mafundi kwenye ujenzi ,fundi akimaliza kazi hana habali nalo.

Yaani tupotupo wenye utambuzi na wenyewe wamekubwa ni woga tena uwoga kwelikweli. Hatujui hatma itakuwaje,maana nionavyo mimi nafikili labda mkazo waongeze .

Kila kitu gharama zake ziongezeke mara mbili Ili utayari wa kusema hapana uwepo kwetu sote na kama kuandamana kushinkiza kiongozi fulani awajibike wataweza maana watakuwa hawana namna
 
Wameshashindwa kuongoza nchi hawa viumbe...wamebaki wanapiga tu propaganda
Watanzania wamemezeshwa viza la kuhofia wasioyajua.

Hata kuwang'oa kwa kura tunapgopa

Angalia drama za Bungeni kana kwamba wana nia njema.

Ni mbunge wa chama gani alisema Bungeni kuwa Watanzania wanapostaafu wakipewa mafao yao kwa mkupuo wanaenda kuongeza wake?

Je, wanaostaafu ni wanaume pekee?

Je, walitumia takwimu za NBS kuongea upuuzi huo? Hatimaye wakapitisha sheria ya kuwaminya wazalendo wanaovuja jasho kila siku huku wakilipwa kiduchu na kodi kubwa

Shame
 
Hili deni mmeanza kumtwisha Samia?
Aliekopa hela nyinyi kimyaa kimyaa hamumjui?Samia ndo kaleta deni la trilioni 71?...hamnaga aibu mkiamua kumchafua mtu?
Twende taratibu, per year average za yule wa kimya kimya ngapi na mama zake ngapi...
 
Back
Top Bottom