Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MFUNGO WA RAMADHANI KATIKA MJI WA HARARE ZIMBABWE
Zamani ilikuwa ukiwa na safari unahitaji vibali kadhaa ili uweze kusafiri, iwe safari ya kikazi au vinginevyo.
Kwanza utahitaji kibali cha Benki Kuu ili uweze kupata fedha za kigeni.
Naamini kuna wasomaji wangu hawajapatapo kusikia kitu kinaitwa Thomas Cooke Travellers Cheque.
Hii ni hundi ambayo msafiri alikuwa anapewa na afikapo safari yake atavunja kupata dollars, pounds nk.
Kulikuwa na kibali cha Wizara husika, kibali cha Ikulu nk. nk. kiasi kuwa hadi umemaliza kupata vibali vyote hivyo mtu unakuwa taaban kwa kuchoka.
Ukiingia tu kwenye ndege hata kabla haijaruka umeshalala kwa uchovu na si kama natia chumvi mimi mwenyewe yamenitokea mara nyingi tu.
Kusafiri ilikuwa shughuli pevu.
Nasafiri kwenda Harare Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ndege Air Tanzania Corporation (ATC) wenyewe ndege hii tukiipa majina kadha wa kadha lakini mimi nililipenda jina la Twiga.
Ndege ya alfajir saa 12 kwa hiyo nimefika uwanjani kumi ya usiku.
Tumetua Harare na haukupita muda niko nje ya uwanja na ndani ya teksi inanipeleka mjini.
Madereva wa taxi wanajua mengi sana kuanzia ''rate,'' ya ''dollar black market,'' hadi hoteli nzuri kwa malazi na chakula.
Dereva wa taxi namuuliza kuhusu msikiti uliopo mjini jirani na hoteli yangu ''Ambassador Hotel.''
Mimi na dereva wa taxi tunazungumza Kiingereza na natumia neno. ''mosque,'' neno hili halipo katika msamiati wake wa Kiingereza.
Nimejitahidi sana kumuelewesha lakini hakunielewa.
Mwisho nikamwambia, ''the place where Muslims pray.''
''Oh! You mean Muslim church I will show you!''
Nikapumua na kweli akanipitisha kwenye huo msikiti nikauona.
Niko Ambassador Hotel, katikati ya mji.
Tarweh nikawa nasali kwenye huu msikiti lakini wengi wa waumini ni Wahindi na Waafrika wachache kutoka kabila la Wayao.
Meneja wa hoteli akawa hanioni kwenye chai asubuhi akanitafuta kutaka kujua kwa nini siendi kunywa chai kwenye dining room ya hoteli.
Kaniuliza tena kwa masikitiko.
Nikamfahamisha kuwa nimefunga Mwezi wa Ramadhani.
Yule Bwana Meneja wala hajui Ramadhani ni kitu gani lakini akaniambia kuwa kuanzia siku hiyo atamfahamisha ''Chef,'' yaani mpishi wa hoteli anitayarishie futari jioni kama fidia ya ya chai ya asubuhi na itakuwa, ''Room Service,'' futari italetwa chumbani kwangu tena, "on the house,'' yaani hawatanitoza chochote.
Furaha yangu haisemeki.
Jioni ile ulipotimu muda wa kufungua nikapiga simu,''Room Service,'' na haukupita muda mlango ukagongwa na futari ikaletwa imefunikwa vizuri sana.
Ikafunuliwa na kwa hakika ule muonekano wake ulinivutia kupita kiasi.
Chakula na vinjywaji vilikuwa vimepangika vyema.
Lakini katika kutupa jicho nikaona kuna nyama ina rangi nyeupe inayokwenda kwenye wekundu na imekatwa ''slice,'' nyembamba iliyoviringika.
Yule bint aliyeleta futari ile alikuwa bado hajatoka mle chumbani kasimama ananiangalia ninavyokitazama chakula kile.
Nikamuuliza kuhusu ile nyama kuwa ni nyama gani?
Jibu alilonipa lilinishtua.
''This is pork sir.''
Kanifahamisha kuwa ile nyama ilikuwa nguruwe.
Futari ya nguruwe.
Kwa utaratibu nilimuomba aondoe chakula chote kile akirudishe jikoni.
Nilihama siku ya pili nikahamia hoteli nyingine inaitwa Holiday Inn.
Kusafiri hakika ni elimu tosha.