Mfungo wa Ramadhani katika Mji wa Harare Zimbabwe

MFUNGO WA RAMADHANI KATIKA MJI WA HARARE ZIMBABWE

Zamani ilikuwa ukiwa na safari unahitaji vibali kadhaa ili uweze kusafiri, iwe safari ya kikazi au vinginevyo.

Kwanza utahitaji kibali cha Benki Kuu ili uweze kupata fedha za kigeni.

Naamini kuna wasomaji wangu hawajapatapo kusikia kitu kinaitwa Thomas Cooke Travellers Cheque.

Hii ni hundi ambayo msafiri alikuwa anapewa na afikapo safari yake atavunja kupata dollars, pounds nk.

Kulikuwa na kibali cha Wizara husika, kibali cha Ikulu nk. nk. kiasi kuwa hadi umemaliza kupata vibali vyote hivyo mtu unakuwa taaban kwa kuchoka.

Ukiingia tu kwenye ndege hata kabla haijaruka umeshalala kwa uchovu na si kama natia chumvi mimi mwenyewe yamenitokea mara nyingi tu.

Kusafiri ilikuwa shughuli pevu.

Nasafiri kwenda Harare Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ndege Air Tanzania Corporation (ATC) wenyewe ndege hii tukiipa majina kadha wa kadha lakini mimi nililipenda jina la Twiga.

Ndege ya alfajir saa 12 kwa hiyo nimefika uwanjani kumi ya usiku.

Tumetua Harare na haukupita muda niko nje ya uwanja na ndani ya teksi inanipeleka mjini.

Madereva wa taxi wanajua mengi sana kuanzia ''rate,'' ya ''dollar black market,'' hadi hoteli nzuri kwa malazi na chakula.

Dereva wa taxi namuuliza kuhusu msikiti uliopo mjini jirani na hoteli yangu ''Ambassador Hotel.''

Mimi na dereva wa taxi tunazungumza Kiingereza na natumia neno. ''mosque,'' neno hili halipo katika msamiati wake wa Kiingereza.

Nimejitahidi sana kumuelewesha lakini hakunielewa.
Mwisho nikamwambia, ''the place where Muslims pray.''

''Oh! You mean Muslim church I will show you!''

Nikapumua na kweli akanipitisha kwenye huo msikiti nikauona.

Niko Ambassador Hotel, katikati ya mji.

Tarweh nikawa nasali kwenye huu msikiti lakini wengi wa waumini ni Wahindi na Waafrika wachache kutoka kabila la Wayao.

Meneja wa hoteli akawa hanioni kwenye chai asubuhi akanitafuta kutaka kujua kwa nini siendi kunywa chai kwenye dining room ya hoteli.

Kaniuliza tena kwa masikitiko.
Nikamfahamisha kuwa nimefunga Mwezi wa Ramadhani.

Yule Bwana Meneja wala hajui Ramadhani ni kitu gani lakini akaniambia kuwa kuanzia siku hiyo atamfahamisha ''Chef,'' yaani mpishi wa hoteli anitayarishie futari jioni kama fidia ya ya chai ya asubuhi na itakuwa, ''Room Service,'' futari italetwa chumbani kwangu tena, "on the house,'' yaani hawatanitoza chochote.

Furaha yangu haisemeki.

Jioni ile ulipotimu muda wa kufungua nikapiga simu,''Room Service,'' na haukupita muda mlango ukagongwa na futari ikaletwa imefunikwa vizuri sana.

Ikafunuliwa na kwa hakika ule muonekano wake ulinivutia kupita kiasi.

Chakula na vinjywaji vilikuwa vimepangika vyema.

Lakini katika kutupa jicho nikaona kuna nyama ina rangi nyeupe inayokwenda kwenye wekundu na imekatwa ''slice,'' nyembamba iliyoviringika.

Yule bint aliyeleta futari ile alikuwa bado hajatoka mle chumbani kasimama ananiangalia ninavyokitazama chakula kile.

Nikamuuliza kuhusu ile nyama kuwa ni nyama gani?

Jibu alilonipa lilinishtua.

''This is pork sir.''

Kanifahamisha kuwa ile nyama ilikuwa nguruwe.

Futari ya nguruwe.

Kwa utaratibu nilimuomba aondoe chakula chote kile akirudishe jikoni.

Nilihama siku ya pili nikahamia hoteli nyingine inaitwa Holiday Inn.

Kusafiri hakika ni elimu tosha.
Umeona ukarimu wa wahudumu wa Kikristu!
 
Ume overreact kwa kuhama hoteli utadhani waliku serve hiyo nguruwe kwa makusudi. Ulivyofanya kuhama hoteli siyo ustaarabu. Kwani huko Holiday Inn hawapiki nguruwe jikoni? Be practical and open-minded. Unaishi karne ya 21.
 
Ningependa kupewa elimu kupitia uzi wako kuwa uharamu wa kula nguruwe ni upi? Je, ukila nguruwe katika amri kumi za Mungu unakuwa umevunja ipi?
 
Mokaze,
Naam.

Unajua Sheikh,watu wengi hasa katika nchi za huko kusini ya Afrika ni walaji wakubwa wa Nguruwe, huwa wanashangaa sana wanaposikia kwamba kuna mtu hali nyama ya nguruwe.

Mimi nadhani ungechukua nafasi hiyo kuwafahamisha kwamba wewe ni Muislamu na kulingana na mafundisho ya Uislamu nguruwe ni haramu kuliwa kwa sababu nyama yake inayo madhara makubwa katika mwili wa binadamu, pi
Mokaze,
Naam.

Ungechukua nafasi hiyo kuwajulisha kwamba hata ndani ya Biblia Nyama ya nguruwe ni haramu kula.
 
Amri kumi za Mungu kwa mujibu wa Imani yako sio kila mtu anaamini hizo Amri

Yeye kwake Nguruwe ni haram kwa mujibu wa mafundisho anayoamini ambayo ni Qur an na si lazima wewe kuamini au kukubali
 
Ume overreact kwa kuhama hoteli utadhani waliku serve hiyo nguruwe kwa makusudi. Ulivyofanya kuhama hoteli siyo ustaarabu. Kwani huko Holiday Inn hawapiki nguruwe jikoni? Be practical and open-minded. Unaishi karne ya 21.
Ndjabu...
Hakika hawakunipa nguruwe kwa makusudi.
Nilihama kwa sababu walikuwa na nguruwe katika menu.

Hukumu ya nguruwe ni kuwa hata vyombo vinavyotumika
kupikia na kupakulia nguruwe huwa vimenasijika.

Njia salama kwangu ilikuwa ni kuhama hoteli.

Holiday Inn hapakuwa na nguruwe katika menu yao.

Ukiwa msafiri wa mara kwa mara vitu hivi unavijua na unajifunza
namna ya kuvishughulikia.

Nilikaa katika moja ya hotel Durban.
Durban hotel zote ziko beach wanaita Golden Mile.

Kwenye chai nilikuta nguruwe.
Sikuhama hoteli ila nilikuwa nakula restaurant ya jirani kwa Wahindi.

Huku ndiko kuwa, ''open minded,'' na ''practical.''
 
Unajua Sheikh,watu wengi hasa katika nchi za huko kusini ya Afrika ni walaji wakubwa wa Nguruwe, huwa wanashangaa sana wanaposikia kwamba kuna mtu hali nyama ya nguruwe.

Mimi nadhani ungechukua nafasi hiyo kuwafahamisha kwamba wewe ni Muislamu na kulingana na mafundisho ya Uislamu nguruwe ni haramu kuliwa kwa sababu nyama yake inayo madhara makubwa katika mwili wa binadamu, pi

Ungechukua nafasi hiyo kuwajulisha kwamba hata ndani ya Biblia Nyama ya nguruwe ni haramu kula.
Mokaze,
Umesema maneno mazuri sana.
 
Mohamed Said uliwakosea fadhila. Kama ulivyomvumilia dereva taxi hadi akasema ''muslim church'' ndivyo hivyo ungewaambia waondoe chakula na kuwaeleza ni kwanini

Kufanya hivyo kungemsaidia Meneja siku nyingine ya ugeni aelewe nini cha kufanya au kuuliza

Nia na dhamira yao ilikuwa njema kabisa, mapungufu ya uelewa hayawafanyi wawe na makosa

Hiyo ilikuwa fursa ya kutoa darsa na si kuhamia hoteli nyingine
Nguruvi3,
Ushauri mwema.
Ahsante.
 
MFUNGO WA RAMADHANI KATIKA MJI WA HARARE ZIMBABWE

Zamani ilikuwa ukiwa na safari unahitaji vibali kadhaa ili uweze kusafiri, iwe safari ya kikazi au vinginevyo.

Kwanza utahitaji kibali cha Benki Kuu ili uweze kupata fedha za kigeni.

Naamini kuna wasomaji wangu hawajapatapo kusikia kitu kinaitwa Thomas Cooke Travellers Cheque.

Hii ni hundi ambayo msafiri alikuwa anapewa na afikapo safari yake atavunja kupata dollars, pounds nk.

Kulikuwa na kibali cha Wizara husika, kibali cha Ikulu nk. nk. kiasi kuwa hadi umemaliza kupata vibali vyote hivyo mtu unakuwa taaban kwa kuchoka.

Ukiingia tu kwenye ndege hata kabla haijaruka umeshalala kwa uchovu na si kama natia chumvi mimi mwenyewe yamenitokea mara nyingi tu.

Kusafiri ilikuwa shughuli pevu.

Nasafiri kwenda Harare Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ndege Air Tanzania Corporation (ATC) wenyewe ndege hii tukiipa majina kadha wa kadha lakini mimi nililipenda jina la Twiga.

Ndege ya alfajir saa 12 kwa hiyo nimefika uwanjani kumi ya usiku.

Tumetua Harare na haukupita muda niko nje ya uwanja na ndani ya teksi inanipeleka mjini.

Madereva wa taxi wanajua mengi sana kuanzia ''rate,'' ya ''dollar black market,'' hadi hoteli nzuri kwa malazi na chakula.

Dereva wa taxi namuuliza kuhusu msikiti uliopo mjini jirani na hoteli yangu ''Ambassador Hotel.''

Mimi na dereva wa taxi tunazungumza Kiingereza na natumia neno. ''mosque,'' neno hili halipo katika msamiati wake wa Kiingereza.

Nimejitahidi sana kumuelewesha lakini hakunielewa.
Mwisho nikamwambia, ''the place where Muslims pray.''

''Oh! You mean Muslim church I will show you!''

Nikapumua na kweli akanipitisha kwenye huo msikiti nikauona.

Niko Ambassador Hotel, katikati ya mji.

Tarweh nikawa nasali kwenye huu msikiti lakini wengi wa waumini ni Wahindi na Waafrika wachache kutoka kabila la Wayao.

Meneja wa hoteli akawa hanioni kwenye chai asubuhi akanitafuta kutaka kujua kwa nini siendi kunywa chai kwenye dining room ya hoteli.

Kaniuliza tena kwa masikitiko.
Nikamfahamisha kuwa nimefunga Mwezi wa Ramadhani.

Yule Bwana Meneja wala hajui Ramadhani ni kitu gani lakini akaniambia kuwa kuanzia siku hiyo atamfahamisha ''Chef,'' yaani mpishi wa hoteli anitayarishie futari jioni kama fidia ya ya chai ya asubuhi na itakuwa, ''Room Service,'' futari italetwa chumbani kwangu tena, "on the house,'' yaani hawatanitoza chochote.

Furaha yangu haisemeki.

Jioni ile ulipotimu muda wa kufungua nikapiga simu,''Room Service,'' na haukupita muda mlango ukagongwa na futari ikaletwa imefunikwa vizuri sana.

Ikafunuliwa na kwa hakika ule muonekano wake ulinivutia kupita kiasi.

Chakula na vinjywaji vilikuwa vimepangika vyema.

Lakini katika kutupa jicho nikaona kuna nyama ina rangi nyeupe inayokwenda kwenye wekundu na imekatwa ''slice,'' nyembamba iliyoviringika.

Yule bint aliyeleta futari ile alikuwa bado hajatoka mle chumbani kasimama ananiangalia ninavyokitazama chakula kile.

Nikamuuliza kuhusu ile nyama kuwa ni nyama gani?

Jibu alilonipa lilinishtua.

''This is pork sir.''

Kanifahamisha kuwa ile nyama ilikuwa nguruwe.

Futari ya nguruwe.

Kwa utaratibu nilimuomba aondoe chakula chote kile akirudishe jikoni.

Nilihama siku ya pili nikahamia hoteli nyingine inaitwa Holiday Inn.

Kusafiri hakika ni elimu tosha.
Mkuu acha uvivu wa kuandika, story yako is very intersting ila hujaimalizia.
 
hahahahahaaa
nafkir utakuwa uliomba namba ya simu ya yule binti. ukishafungulia unamwita lodge mwenyeji wako Binti mzungumze vizur amewezaje kupika chakula kizur vile ila tu akakosea kuweka Pork
 
Back
Top Bottom