Pragmatist
Member
- Sep 21, 2012
- 18
- 1
Inatisha! Aliyefungwa miaka 15 kukutwa uraiani tena akiwa na silaha za kivita. Magereza wanafanya nini? Haya ndiyo makandokando ya rushwa. Kama kawaida yetu Watanzania hakuna atakayewajibika! Serikali mpo?
==========
MFUNGWA anayetumikia kifungo cha miaka 15 jela alichohukumiwa mwaka 2010, Masanja Maguzu (42), amekuwa akiishi uraiani baada ya kutoka gerezani katika mazingira ya kutatanisha.
Akisimulia mkasa huo jana, Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Salum Msangi alisema awali wa Polisi ilikuwa ikimchunguza mke wa Maguzu, Holo Mabuga (30) ambaye alipatikana akimiliki silaha ya kivita kinyume cha sheria.
Mwanamke huyo kwa mujibu wa Kamanda Msangi, alikamatwa Novemba 6 mwaka huu akiwa na silaha ya kivita aina ya G 3 ikiwa na risasi zake 36 na risasi zingine 96 za bunduki aina ya SMG.
Baada ya kumkamata mwanamke huyo, Kamanda Msangi alisema waligundua kuwa hakuwa peke yake katika matumizi ya silaha nzito na ya kivita kama hiyo, bali nyuma yake kulikuwa na mtandao au kundi la watu waliokuwa wakishirikiana naye kuzitumia silaha hizo katika matukio ya ujangili na uporaji wa kutumia silaha bila kujua ni mumewe.
Kamanda Msangi alisema, kutokana na hali hiyo polisi waliandaa mtego ili kubaini mtu au watu waliokuwa kwenye mtandao huo wa uhalifu waliokuwa wakishirikiana na mwanamke huyo.
Kutokana na mtego huo, siku kumi baada ya kumkamata mke wa mfungwa huyo, polisi walimkamata Maguzu akiwa nyumbani kwake katika Kijiji cha Ng'wang'wali wilayani Itilima katika Mkoa wa Simiyu.
Maguzu alikutwa na silaha ya kivita aina ya SMG, risasi 31 na magazine tatu ambazo moja ya magazine hizo ni ya bunduki aina ya Uzi Gun ya Israel.
Kamanda Msangi alisema kupatika kwa magazine hiyo kunathibitisha kwamba kuna bunduki nyingine aina ya Uzi Gun ambayo matumizi yake ni sawa na SMG, iko mikononi mwa mtandao wa wahalifu na watu wabaya.
Alisema kama haitapatikana haraka, silaha hiyo itaendelea kusumbua na kuhatarisha usalama wa maisha ya wananchi na mali zao na hata wanyama katika hifadhi za wanyama pori.
Kutokana na utata huo, Kamanda Msangi alisema wanafanya uchunguzi wa kina ili kubaini sababu za kuachiwa na kuwa huru kwa mfungwa huyo hatari aliyepatikana na hatia ya kupatikana na silaha na kuhukumiwa na Mahakama adhabu ya kifungo cha miaka 15 jela mwaka 2010.
Maisha ya askari
''Mimi kinachonisikitisha zaidi ni jinsi baadhi ya watu wanavyohatarisha usalama kwa kuwaachia huru wahalifu sugu na hatari kama huyo. Wakati sisi polisi hatulali na tunauza roho zetu kupambana na uhalifu hasa wa kutumia silaha nzito kama hizo, baadhi ya watu wanakwamisha jitihada zetu kwa kuwaachia huru wahalifu hao katika mazingira ya kutatanisha.
"Lakini hili la safari hii hatutalifumbia macho mpaka wale wote walioshirikiana naye wabainike na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria, mimi nimekula kiapo sintakubali kurudi nyuma,'' alionya.