SoC01 Mfungwa sio mnyama, alipwe, alipe kodi

SoC01 Mfungwa sio mnyama, alipwe, alipe kodi

Stories of Change - 2021 Competition

Kamamaa

Member
Joined
Feb 12, 2010
Posts
15
Reaction score
4
Mfungwa anapomaliza kifungo na kurudi uraiani anakuwa kama mtoto. Hana kazi, hana mali na wakati mwingine hata utu wake huonekana tofauti. Anaweza kuonekana kama mhalifu kama wengine wengi ambao wakitoka jela huwa na sura za kutisha.

Huonekana si kitu. Hana mbele wala nyuma na waswahili husema mkono mtupu haulambwi. Si marafiki tu, hata ndugu husumikiliza na kumthamini yule mwenye nacho sasa huyu mwenzangu na mimi nani atamjali.

Anachoweza kuambulia ni pole halafu kila mtu ataendelea na hamsini zake.
Kama akiwa jela ataandaliwa vyema kwa kuwezeshwa ili atokapo asianze upya, hatakuwa tofauti na wengine. Atakuwa na mpangilio wa maisha yake na hatakuwa tegemezi.

Hili litawezekana iwapo utawekwa mfumo wa kuwalipa wafungwa na kuwahifadhia fedha kidogo wanazopata pale wanapofanya kazi wakiwa wafungwa.

Shughuli zote wanazofanya wafungwa kama vile kilimo, ujenzi au ufundi zinaweza kuwekewa mfumo wa kisasa ambao utalinufaisha jeshi la magereza, Taifa na mfungwa mmoja mmoja.

Fedha hizi zitahifadhiwa na mfungwa atakabidhiwa wakati akitoka. Hii itamfanya kwanza afanye kazi kwa bidii na kuwa na matuamaini ya maisha ya nje baada ya kumaliza kuitumikia adhabu yake.

Lakini si kwamba itakuwa na tija kwa mfungwa tu, hata kwa Taifa, kama mgungwa atalipwa basi atapaswa kulipa kodi pia.

Pia mfumo huo unaweza kuboreshwa kwa kumfanya mfungwa aweze kuisaidia familia yake kama kuwalipia karo watoto wake. Hii itarudisha utu wake.

Mfumo wetu wa magereza uangaliwe
‘Jehanamu ndogo duniani ni magereza hasa upande huu wa dunia ya kwetu’. Yametengenezwa kukomaza wahalifu na pia yakilalamikiwa kuwa chanzo cha vitendo vya ushoga na usagaji. Wachache huzungumza unyama wanaokutana nao wakiwa chini ya himaya hiyo. Iwe ni mahabusu au wafungwa. Yote haya huchochewa na msongamano.

Moja ya rai alizotoa Hayati Rais John Magufuli mwezi mmoja kabla ya kufikwa na umauti ni kuhakikisha mrundikano magereza unapungua kwa manufaa ya Taifa.

Akiwa mjini Dodoma katika maadhimisho ya Siku ya Sheria, Rais Magufuli alisema: Natoa rai kwa waheshimiwa Majaji kuruhusu dhamana na kutoa adhabu mbadala kila inapostahili. Hii sio tu itapunguza mrundikano wa wafungwa kwenye magereza yetu, lakini pia itaipunguzia Serikali mzigo wa kuhudumia wafungwa.

Pamoja na kuwa Serikali ia mpango madhubuti wa kupunguza idadi ya wafungwa kama wale ambao hupata msamaha wa Rais katika sherehe za Muungano na Uhuru, bado magereza zimeendelea kufurika kwa kuwa wengi hurudi tena jela.

Hapa ndipo inapokuja kulazimu kutafakari, ni kwa nini magereza zetu zinatengeneza jamii ya namna hii. Jibu ni kwamba haziwaandai kuwa raia wema mara tu wanapokutana na uhuru.

Maisha yale yamewageuza kutoona tofatuti ya mtu huru na aliyefungiwa kama mnyama. Hayamuandai kujitegemea mara tu atakapomaliza muda wake.

Kwa wengi anapoingia jela, maisha yake huanza upya. Hupoteza mali, kazi, biashara, marafiki na wakati mwingine hata ndugu humtelekeza.

Ni Kama hupoteza dira na mwelekeo kabisa wa maisha yake. Atakaa ndani ambako atapambana na ‘wababe’, huenda naye akabadilika kama liingia akiwa mtu mwema. Ili kuishi atalazimika kufanya mambo mengine ambayo nje hakuwahi kuyafanya.

Kama ana nguvu itabidi azitumie la kama hana basi afanye anayoelekezwa na ‘wababe wa vita’ ili aweze kuishi akisubiri siku yake ya kutoka.

Kesi zisomwe kwa wakati
Mwezi uliopita Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Hamza Chilo alitangaza kuwa Serikali imeandaa mpango maalumu wa kupunguza mahabusu nchini. Ni hatua nzuri kwa kuanzia.

Ikumbukwe ni wiki chache zimepita tangu iliporipotiwa kuwa Gereza la Mpanda lenye uwezo wa kubeba wafungwa 100, sasa linahifadhi wafungwa 400. Hali iko hivi karibu magereza yote nchini. Yanabeba idadi kubwa ya wafungwa kuliko uwezo wake.

Athari yake mbali na kuchochea tabia za kihalifu, pia husasababisha magonjwa ya mlipuko, magonjwa ya ngozi, magonjwa ya mfupo wa upumuaji, uhalifu na unyanyasaji baina ya wafungwa.

Kinachopaswa kufanyika sasa ni kutowakamata watu kabla uchunguzi haujakamilika kwa baadhi ya makosa. Huu huwa uonevu kwani wakati mwingine huwalazimisha wachunguzi kuwabambikia watu vidhibiti hasa pale wanapokumbwa na shinikizo la kukamilisha uchunguzi.

Itungwe sheria ya kuwawajibisha polisi pale inapogundulika kuwa mtuhumiwa hakuwa na hatia ili afidiwe muda na maumivu aliyopata Katika kipindi chote cha kesi.
 
Upvote 2
Apo labda tu fidia kama hana kosa ila sijui kuajiriwa ngumu maana mtaani penyewe hamna ajira leo hii watu wasikie ajira zipo ukiwa gerzani itasababisha watu tufanye makosa twende uko tule na tulale bure baada ya apo tunafanya kazi tunalipwa.. au labda kuna nchi inasheria hzo unazosema kuwa mfungwa analipwa Kwny kazi anazofanya jela???
 
Apo labda tu fidia kama hana kosa ila sijui kuajiriwa ngumu maana mtaani penyewe hamna ajira leo hii watu wasikie ajira zipo ukiwa gerzani itasababisha watu tufanye makosa twende uko tule na tulale bure baada ya apo tunafanya kazi tunalipwa.. au labda kuna nchi inasheria hzo unazosema kuwa mfungwa analipwa Kwny kazi anazofanya jela???
Kuajiriwa inawezekana na ipo nchi nyingi duniani. Hulipwa mishahara na fedha huifadhiwa katika akaunti maalumu. Pia ni walipa kodi katika mataifa hayo.
 
Back
Top Bottom