Mfunze Mwanao kujiajiri, mwambie maisha hayaanzi akiajiriwa, wasomi wakiwa wengi ajira zinakuwa chache

Mfunze Mwanao kujiajiri, mwambie maisha hayaanzi akiajiriwa, wasomi wakiwa wengi ajira zinakuwa chache

Ujasiriamali siyo kitu rahisi hata kidogo na ndiyo maana uchumi kama wa Marekani unadhibitiwa na watu wasiofikia kumi. Kama ni kusoma ama kuona fursa unajiuliza hivi mtu wa Marekani na Tanzania kwa uwiano kupi kuna wasomi na waona fursa wengi!?

Ni kweli ni lazima vijana wajifunze kufanya kazi ili wajitegemee lakini si kweli kwamba kila mtu kwenye kila jamii atafanikiwa kuwa sawa na wengine waliofanikiwa. Tatizo hao "Motivational/Inspirational speakers" huwa mafundisho yao yanaonesha kufanikiwa kupo kwa kila mtu na wasiofanikiwa ni kwa kuwa hawajajaribu ama kuthubu.

Kuwa na mali na kufanya kile unachokipenda na kukiamini ni vitu viwili tofauti. Tatizo kwenye jamii yetu maskini ni wengi sana kiasi kwamba akitokea mtu na porojo za kufanikiwa wengi hupata kichaa cha kujilamu kuchelewa au kujiona wana ujinga wa kutokujuja mambo na kuamini kuwa wana hofu ya kuthubutu kuyatafuta mafanikio.

Hao magwiji wa kuhamasisha wenyewe ukiwachunguza sana ni wakwepaji wakubwa sana wa kodi. Hivi yale makongamano na semina wanazoziendesha huwa wanalipa kodi kweli??
 
Sasa hivi sio watoto tu wanaolalamika kuwa hakuna ajira bali mpaka wazazi wa watoto hao wanalalamika ajira hakuna jambo ambalo linafanya familia nzima inalaumu tu mwanzo mwisho na hakuna anaezinduka hapo.

Ni bora aliyejiajiri akawa anapitia magumu wakati huu kuliko yule ambaye hana ajira kabisa wakati huu can you imagine the situation?

Hii ni kwa sababu mzazi alimjenga mwanawe tokea zamani kuwa soma upate ajira,soma upate ajira mwanangu.

Hii ni sumu mbaya sana kwa watoto mwisho wa siku mtoto anaona kuwa bado hajaanza maisha mpaka apate ajira kwanza,wakati maisha yanaanza unapojitambua na kuwa na malengo yako.

Kwa ambao wana ajira wakomae na ajira zao.

Mwambie mwanao sasa hivi wasomi wengi sana na ajira zinakuwa chache mno hasa katika mambo ambayo wengi wanasomea, kumbuka ukisoma H.R kuna mamia huko nyuma wamesoma kwa hiyo usitegemee kuwa wewe ni mtu muhimu sana uajiriwe wewe peke ako,pengine ukakosa jipange kisaikolojia.

Kiukweli maisha yanakoenda inaonekana kuwa watu wanashida sana na ajira kuliko hiyo ajira ilivyokuwa na shida na watu.

Bwana einsten aliwahi kusema kuwa : where there is a difficult,there is an opportunitiy.

usitake mambo rahisi rahisi tu alafu mafanikio yaje simple kana kwamba unafanya peke yako jambo hilo.

Watu ni wengi,wasomi ni wengi ajira ni chache sana.serikali yenye akili haiwezi kuwaajiri watu ambao hawana shida nao,haiwezi kuajiri watu ambao hata wasipokuwepo kazi zitaenda bila shida.hata wewe upo hivyo.

Mwambie mwanao maisha yanaanza akijitambua na kuwa na malengo na maisha hayaanzi akiajiriwa,mwambie hata akiwa shule ana haki ya kujiajiri na kuwa mjasiriamali.

Mtoto harithi ajira ya baba,mtoto anarithi biashara tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
sio kwamba ajira hazipp ila ni upatikanaji wa mishahara ya kuwalipa ila mahitaji ya watu kuhudumiwa ni weni sana hasa kwa nchi kama tanzania maana katika taasisi sio tu za kiselikali hata za binafis kuna upungufu mkubwa wa watoa huduma kwa kila aina ya nyanja nakupa mfano madaktari na manurse na ma midwife ni watu muhimu sana wapo mitaani ila huko kweneye vituo vya kazi ni wachache sana ukianalia ma accountats pia ukiangalia ukienda mabank mengi pamoja na taasisi wapo wachche sana na kusababisha folenina upotezaji mkubwa wa muda vile vile kwa ma engeneers hasa a umeme kila siku tanesco watu wanakatiwa umeme kupata hiyo huduma mpaka baada ya wiki angalia mabarabara kila siku yanaharibika na ni watu wanahitjaika angalia kesi mahakamani zipi nyingi sana ila mahakimu ni wachache kwahiyo sio kwamba kazi hazipo ila ni rasilimali za kuwezesha hao wasomi ili wapate kulitumiki taifa nahisi ndio bado hazijaangaliwa ndo maana ..
 
Lakini yote ni sababu ya pesa.

Laiti ingekuwa kitu kinachoitwa pesa hakuna basi kuna mambo yangeenda vizuri ila ni ngumu sana hicho kitu kwa dunia ya leo.

Mwalimu wa mtaani analalamika hakuna ajira kwa sababu anajua akiajiriwa atapata pesa.

Unadhani tukiondoa kupata pesa kwa mwalimu aple anaoajiriwa je unadhani kuna kingine ambacho kitamfanya mwalimu adai kuajiriwa na kulaumu kukosa ajira ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusio na kazi jamani tupambane tuuze hata mihogo au maji ya kandoro kitaa huko ilaniwambie ukweli ile bongo ya kuuza nyanya hadi kumiliki mabasi ya mkoa au hoteli kihalali iliisha miaka hiyooooo leo 2020 ukiuza mtumba au kandoro au mahindi utauza hivo maisha yako yote hutoki bila magumashi na hayo magari hata vitz utayaona kwa wenzako tu....

Kabisa mkuu.

Bora kihangaika na karanga barabarani , kuliko kuhangaika na cheti mfukoni bila mafanikio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila Watanzania huwa tunapenda sana sifa. Unakuta mtu Mungu kamjaria katoboa kweli afu anakuja kutujaza ujinga hapa kuwa tujijiari. Ukweli ni kwamba kuajiriwa kutaendelea kuwepo na kujijiari pia kutakuwepo milele.

Imagine mtu kasomea education afu leo hii unamtia presha et akalime matikiti au akafungue mgahawa au awe mbunifu katima technology wakati kasoma masomo ya sanaa! Tusidanganyane kujiajiri n bonge la kipaji na mtaji. Huo ubunifu wa Technology unahitaji heavy Capital tuache kulishana matango poli hapa.

Unataka kutwambia mtu katokea familia ambayo hata umeme wa solar ya D-ligth hawana leo hii awe mbunifu wa technology!? Ili ufanye vitu vya kueleweka katika jamii lazima uwe na mtaji wa kueleweka tuache kudanganyana hapa.

Nitoe ushuhuda wangu kipindi nimemaliza kidato cha sita nilipitia app fulan hivi ufugaji aisee nikaona kufuga kuku wa kienyeji kwa laki 3. Nikapa morali nikaingia nikanunua vifaa vya kutengenezea banda kweli nikaanza kupiga ufugaji ila baada ya miezi miwili huwez amin kuku wangu walikufa nikaaza kidogo.

In short kwangu mimi nitaendelea kupambana mtaani lkn kweli ajiri ikitoka na nikaajiriwa serikalini naenda tena napiga kazii. Ajira ni tamu sana
 
Mimi ninatoa rai kwa serikali na private sectors kuwekeza kwenye Vocational Trainings Centres zenye wataalam na Miundombinu ya kisasa zinazoendana na dunia ya teknologia na uhitaji wa duniani. Tukifanya hivi ni dhahiri kwamba tutapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira kwani vijana watapata skills ambazo wataziapply moja kwa moja na kujipatia kipato. Pia skills zikiwa ni za kujitosheleza wanaweza kucompete regionalwise na globally. My five cents!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo kwenye technology, mainly online shopping ila biashara kibao, sibagui kazi as long as inaingiza hela

Unajua laiti vijana wengi wangejua fursa zilizopo kwenye upande huo wa technology hasa upande wa internet na computer technology kwa ujumla nadhani wengi wangebadilisha maisha yao na kupiga hatua japo kidogo. Ila shida inakuja wengi wanaamini hiyo technology ni kwaajili ya waliosoma IT tu, na wengine wanaamini hayo mambo kama ya Online Shopping ni utapeli tu, at the end of the day unakuta watu wanaishia kulialia tu na kutafuta mchawi, basi unaamua kuacha tu kila mtu apambane na hali yake.

Unajua kuna watu wengine hapa hapa jamiiforums ukiwa unalia lia kuhusu ajira na kukosa pesa huwa wanashangaa sana , ni kweli hata mm ni mmoja wapo huwa nashangaa sana, nadhani kuna kitu hakipo sawa miongoni mwa wahitimu wengi wa vyuo vikuu.
 
Lkn mkuu ninyi mnaongelea vijana ambo tayari wana mitaji! Jaribuni kugusa vijamba ambao hata kutapa 100k kwa ajiri ya mtaji huo uwezo hawana na anatamni sana kufanya hivyo. Mi naona mnaongelea watu wa maisha kati lkn wengine tunajaribu kupata hata njia tu lkn inashindikana mkuu.

Naomba kama hutojari unisaidie kwa hilo
 
Kijana mwezangu, maisha siyo rahisi , but ni rahisi kwa wale wanaothubutu na kutoka nje ya comfort zone. Alafu usipende sana kutaka kuhurumiwa tena hasa unapokuwa mtoto wa kiume, ni hatari sana. Alafu usiwe unajiaminisha maisha unayopitia wewe basi wengine hawayajui au hawajayapitia, wanayapitia ila wanapambana na changamoto zilizo mbele yao na kuzishinda, na hiki ndiyo kipimo cha elimu uliyoipata huko chuo kiku.

Kwahiyo ww unaamini kila mwenye mtaji ni lazima atoke kwenye daraja la maisha ya kati? Unazungumzia 100k? Toka nje ya Comfort Zone utaipata tu hiyo 100k, usianze kuangalia wanaokuzunguka watakuonaje au watakuchukuliaje, believe me or not ukifika stage hiyo utaipata hiyo 100K. Hata sisi tulipitia huko.

NOTE: LIFE BEGINS AT THE END OF YOUR COMFORT ZONE
 
Nipo kwenye technology, mainly online shopping ila biashara kibao, sibagui kazi as long as inaingiza hela
Unajua laiti vijana wengi wangejua fursa zilizopo kwenye upande huo wa technology hasa upande wa internet na computer technology kwa ujumla nadhani wengi wangebadilisha maisha yao na kupiga hatua japo kidogo. Ila shida inakuja wengi wanaamini hiyo technology ni kwaajili ya waliosoma IT tu, na wengine wanaamini hayo mambo kama ya Online Shopping ni utapeli tu, at the end of the day unakuta watu wanaishia kulialia tu na kutafuta mchawi, basi unaamua kuacha tu kila mtu apambane na hali yake.

Unajua kuna watu wengine hapa hapa jamiiforums ukiwa unalia lia kuhusu ajira na kukosa pesa huwa wanashangaa sana , ni kweli hata mm ni mmoja wapo huwa nashangaa sana, nadhani kuna kitu hakipo sawa miongoni mwa wahitimu wengi wa vyuo vikuu.
Lkn mkuu ninyi mnaongelea vijana ambo tayari wana mitaji! Jaribuni kugusa vijamba ambao hata kutapa 100k kwa ajiri ya mtaji huo uwezo hawana na anatamni sana kufanya hivyo. Mi naona mnaongelea watu wa maisha kati lkn wengine tunajaribu kupata hata njia tu lkn inashindikana mkuu.

Naomba kama hutojari unisaidie kwa hilo
Jamaa Umomi umejibu umeandika hoja mzuri sana hapa, mimi mmoja wapo nazifuatilia na nataka nianze hizi Online Hustle hata leo ila sio suala la eti huna hata Tzs 50 uwamue kufanya tu unafanya ni uwongo.

Hivi mambo zinahitaji uwe na kipato kwanza amini most of them unahitaji Smartphone nzuri, PC nzuri, Some Startup Capital kuanza tu kitu kama Freelauncer au Upwork bika kutoa Cent 5 ni uwongo, Kuanza Drop shipping bila kutoa Cent 5 uwongo, FX ndio kabisa usiseme.

Haya mambo yanahitaji Skills sindogo ambayo kuipata inakubudi uwekezeze muda wako na pesa ndio uje ku Earn something delicious, sasa kwa ambaye 50,000/= Cash ya pamoja inamshinda anawezaje.

Hizi Biashara nitakuja kufanya sana nutawekeza kilakitu huko najua potential yake ila kwasasa ku-accumulate 40,000/= still nightmare for me ngoja nikomae na kusaka vibarua na vibarua vigumu Time will prove a point.
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] we jamaa kweli umeona mbali ...Ajira n tamu pale ukipata sector nyeti ...ndo utafurahia ... Wanaotoa ushauri tujiajiri wao wanakula Ac 24/7 ...maisha mazuri ....

One love
Eeh mkuu kuna sector ukiwekwa kumenya ni akili kumkichwa tu. Unaeza hisi watu wanaosema maisha magumu kama wanakupigia kelele tu maana we hata mshahara huangaiki nao.

Kizazaa zaa ni siku utakayoondolewa ama kuhamishwa kitengo.
 
Mkuu wewe ukipata kitengo cha aina hio itakuwa balaa!
Hahahahah acha kabisa mkuu, kuna watu wamekabidhiwa vipande hao ndio ambao wengine wameegamia kwenye praise team.

Ukiwa ofisini kipupwe, ukiwa nje ya ofisi kipupwe, ukiwa home kipupwe tu! Kama mtoto kipenzi DAB anavyomenya tu downtown enzi zile ilikuwa Rizi kila upande now kijiti ni cha DAB. Ana switch whips tu like nobodys business! Wapo ambao wame laylow mi na wewe hatuwajui.
 
Tatizo la sisi waafrika tunakuwa kwy umasikini wa kutupa tunajua kwamba kuwa na watoto ndio utajiri, kumbe ni mawazo ya kimasikini kuwa na watoto alafu kutokufatilia mwenendo wao, bila mzazi kuwa na idadi ndogo ya watoto ambao tutaweza kuifatilia tutaendelea kuteseka na umasikini ktk maisha yetu yote wenzetu China walinyanyuka baada ya kupiga marufuku ya kuzaaa zaaa ovyo bila kufata uzazi wa mpango na kurejesha akili kwy ufanyaji wa kazi. Ukishakuwa busy na kazi huna muda wa kukaaa na family. Matokeo ya kutokukaaa na family watoto wanaharibikiwa kwa sababu wanakosa ile muda thabiti na mwisho kuharibikiwa. Watoto wawili mpaka watatu wanatosha zaidi ya apo ni shida tuuu hata kama unayo pesa muda wa kulea family unakuwa huna

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo development model yako sio ya kweli........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahah acha kabisa mkuu, kuna watu wamekabidhiwa vipande hao ndio ambao wengine wameegamia kwenye praise team.

Ukiwa ofisini kipupwe, ukiwa nje ya ofisi kipupwe, ukiwa home kipupwe tu! Kama mtoto kipenzi DAB anavyomenya tu downtown enzi zile ilikuwa Rizi kila upande now kijiti ni cha DAB. Ana switch whips tu like nobodys business! Wapo ambao wame laylow mi na wewe hatuwajui.

For Ordinary Civilians especially from Ordinary familia, ni ngumu ×1000kupata position nzuri ya ajira ila rahisi atleast kupata position nzuri kidogo kwenye biashara.

Unahitaji Hustle kupata position nzuri ya ajira kuliko ku-position Biashara yako kuwa nzuri.
 
Kweli mkuu, ila vyote viko mkononi mwako. Competition is way ahead of in both so unachagua bega tu!
 
Kweli mkuu, ila vyote viko mkononi mwako. Competition is way ahead of in both so unachagua bega tu!
For me is better to put all in Business, sioni mafanikio kwenye nilichosomea sijawai kuona mwalimu mwenye maisha ninayoyahitaji mimi.

Naitaka ajira leo kesho ila kuna kitu ajira itani Offer...Sijawai ona Position nzuri kwenye Carrier ya uwalimu.

Unapokuwa mdaharo wa Ajira Vs kujiajiri/Biashara kwanza iangalie ajira gani.
 
Hiki ndio wengi hawakiongelei. Kuna ajira zina mishahara na bonus kubwa balaa.
 
For me is better to put all in Business, sioni mafanikio kwenye nilichosomea sijawai kuona mwalimu mwenye maisha ninayoyahitaji mimi.

Naitaka ajira leo kesho ila kuna kitu ajira itani Offer...Sijawai ona Position nzuri kwenye Carrier ya uwalimu.

Unapokuwa mdaharo wa Ajira Vs kujiajiri/Biashara kwanza iangalie ajira gani.
Yeah kwa ualimu ni mtihani...naona wengi wameegamia kwenye business na wamenyoosha life wamesahau vumbi la chaki.
 
Back
Top Bottom