Mfunze Mwanao kujiajiri, mwambie maisha hayaanzi akiajiriwa, wasomi wakiwa wengi ajira zinakuwa chache

Mfunze Mwanao kujiajiri, mwambie maisha hayaanzi akiajiriwa, wasomi wakiwa wengi ajira zinakuwa chache

Haha napata point yako ila sio entrepreneurship hiyo, wanasema mfundishe mtu kuvua samaki sio kumpa samaki, kama wanataka ideas kuna thread moja humu mtua alipost idea zaidi ya 10 ambazo nyingi ukifanyia kazi unatengeneza mamilioni, in short kuna idea moja alitaja ambayo hata mimi nilikua nshaanza kuifanyia kazi.

Kua entrepreneur mzuri solution ni moja tu, angalia tatizo ambalo lipo kwenye mazingira yako, tafuta solution yake na solution iwe ambayo watu wanaweza kulipia, alafu solve hilo tatizo watu wakupe hela. Kila biashara ndivyo ilivyo.

Sasa bongo matatizo mbona yamejaa mno? Na kama mtu hana capital akianza kuimplement idea hata kwa hela kidogo anaweza fika sehemu akaomba investment makampuni yapo mengi yanatafuta watu wanaojaribu kitu kipya wainvest, hata mimi mwenyewe ukija na kitu kipya na kinaweza tengeneza hela kweli umeanza kuexecute vizuri investment naweza toa mapema kabisa, just don’t come with an idea, njoo ukiwa umeishaanza kuexecute, napenda sana execution kuliko maneno tu.

Na nishapata jengo kubwa soon nitafungua incubator Dar es salaam ya technology kuleta startup companies mbalimbali bongo nawapa ofisi bure kabisa wakae waimplement wanachotaka, nawapa na msaada wa marketing kwenye sns, mabango ya barabarani ikihitajika au technical experties maana nina miaka zaidi ya 10 kwenye utengenezaji wa software.

Naomba vijana wa kitanzania muamke, acheni lawama, acheni excuses, hakuna mtu atakaa awasikilize, amka anza kupiga kazi, huna direction kaa uliza watu, kaa tafuta connection, tafuta like minded people, kila mtu ana strength zake na weakness zake, tafuta mtu opposite na wewe anayeweza kukupa nguvu aple ambapo una mapungufu, entrepreneurship una challenge zake kibao ila trust me ukihit ni biashara moja tu unachomoka kabisa unasahau umasikini.
Mtu wa mwisho kumsoma akiandika vitu kama hivi alikuwa ONTARIO
 
Ila Vile vitabu vya Motivation vinatuaribia Sana Taifa.
We need Experts in this country for Christ's Sake.

Na hatuezi kufika huko kama mtu unasoma uengineer alafu 80% ya mawazo yako yanawaza shamba La matikiti uliloacha mkuranga baada ya kuiskiliza ushauri Wa Shigongo. Huo muda wa kuwaza jinsi ya kujenga daraja kuanzia Dsm hadi Znz utautoa Wapi? Unakuwa Katikati.

Siyo kila mtu Anaeza Akawa Entrepreneur. Mbona ni Obvious na mtoa Mada umekiri Ujasiriamali unaitaji Muda Na maarifa.

Mna discourage Sana Vijana hamjui tu. We kama umeamua kulima matikiti lima tu mkuu.

Corona imeingia Sasa hivi Hao wasomi (madaktari) mnaowatukanaga na kuwaambia WAJIAJIRI wangefuata ushauri wenu na wakaingia kwenye calling Yenu kwa Sasa mngewapata Wapi? Au nyie wenzangu mkiumwa Mnapelekwa Kwa WAJASIRIAMALI?

Hizo taarifa za Corona mngetoa Wapi bila millard, em imagine na mwenyewe angeingia kwenye Ujasiriamali?

Inaezekana Nimetoka Nje ya Mada ila bottom Line ni kwamba Acheni Vijana Wasome in Peace, wafanye WALICHOSOMEA wawe the Best. TUNATEGEMEANA. Nchi haiendeshwi na wajasiriamali pekee.
 
Twende practical... Mfano uyo jamaa wa law anahitaji kujiajiri ila iyo biashara unahitaji 100K na iyo K hana, unasemaje anawaza kuajiriwa tu.

Hawezi kosa mtaji wa 100K


Mi dadake nipo na mamake yupo.

Alishapewa duka la 12M limemshinda.

Akipewa leo 500k kesho hana anakuomba buku ya supu.

Ila vitu vingine haviihitaji mtaji.

Mfano lawyer sio lazima aanze na ofisi au mtaji watu wanahitaji huduma ya kisheria anaweza saidia na akapata hela. Eg kuandika mikataba ya nyumba, kuwasaidia watu wanaoenda Mahakamani nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unavyoelezea unaonesha kama ulienda shule, kama kweli basi ni wazi shule uliyoenda ilikunyima kuelimika ikakujaza ujinga.
Usisahau na wewe ndio ulikua head prefect wa shule tuliyokua tunajazwa ujinga.
 
ninauelewa na hizo mambo kuliko yeye, pia nna vifaa vinavyohusu mambo hayo.so namuongoza. sijui nimeeleweka??
Mshauri wa dj mkuuu kivipi?

When your toddler was learning to walk, you’d encourage her to get back up after she fell down,Parents should practice that approach as their children get older.
 
Hawezi kosa mtaji wa 100K


Mi dadake nipo na mamake yupo.

Alishapewa duka la 12M limemshinda.

Akipewa leo 500k kesho hana anakuomba buku ya supu.

Ila vitu vingine haviihitaji mtaji.

Mfano lawyer sio lazima aanze na ofisi au mtaji watu wanahitaji huduma ya kisheria anaweza saidia na akapata hela. Eg kuandika mikataba ya nyumba, kuwasaidia watu wanaoenda Mahakamani nk

Sent using Jamii Forums mobile app
Duu kumbe ndio hivyo.
 
Sasa kila mtu akiwa mjasiriamali itakuwaje?

Ujasiriamali wenyewe wa kuuza nyanya!

Hebu tuwe serious watanganyika!

Ujasiriamali ni kipaji ambacho sio wote wako nacho! Ujasiriamali ni taaluma!

Kila mtu atembeze tenga la nyanya patatosha kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani, maana huwez kukosoa kwenye vitu vidogo vidogo hivyoo.Kwani umesikia hapa anafanyiwa usahili mpaka umtake kuandika vizuri??

When your toddler was learning to walk, you’d encourage her to get back up after she fell down,Parents should practice that approach as their children get older.
Amezidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nunua maharage kilo mbili na cement mifuko mitatu kisha jenga mgahawa. Baada ya miezi saba utakuwa na five star hotel na zaidi ya bilion mia tatu benki!

Alisikika motivational speaker kwenye viunga vya stendi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahah na motivational speaker huyo aliongea maneno hayo huku akijifuta uso wake kwa mikono baada ya leso aliyokua akitumia kua imeloa jasho chapa chapa sababu ya kutembea kwa miguu kutoka kutoka Bunju mpk hapa Mwenge kwny huu mkutano.
 
Mnhhh nyie mliotoboa mna mambo!

Confidence ni muhimu kitu cha kum coach mwanao..hakikisha unamjengea kujiamini ku face anything

i think mmeshindwa kutambua kwamba ...sio swala la mzazi peke yake ku'mwambia' tu mtoto asiwe na ndoto ya kuajiriwa..

Mimi naona ni kitu kinachokua reinforced katika jamii,parents,teachers,peers wanajamiii wote wanachangia kumshape mtu through daily experiences...hivyo basi kama tunataka kulimaliza tatizo la ajira,we must not look at individuals bali at societal level..
 
Hahahah na motivational speaker huyo aliongea maneno hayo huku akijifuta uso wake kwa mikono baada ya leso aliyokua akitumia kua imeloa jasho chapa chapa sababu ya kutembea kwa miguu kutoka kutoka Bunju mpk hapa Mwenge kwny huu mkutano.
Mnaokaa kwenye viyoyozi mna maneno sana. Tuacheni tuuze nyanya na matikiti,kupanga ni kuchagua.
 
Back
Top Bottom