Wakuu natafuta eneo zuri la kufanya kikao na client, sio kikao official sana ila ni mtu ambae atujuani anakaa maeneo ya Goba.
Wanaofahamu maeneo hayo naomba suggestion za hotel au mgahawa tulivu tunaoweza pata lunch au soft drinks uku tukifanya maongezi. Iwe karibu na barabara sio pa kuelekeza sana.
Na pasiwe expensive kihivyo, sehemu nzuri tu ya hadhi ya mtu mstaarab kuwa comfortable kukaa.
Thanks in advance
Nashaur ungefika kwanza uangalie Mazingira ya hizi sehem ili ujue ipi umeridhika nayo kukaa na mteja wako:-
1. Roz Kitchen Restaurant
Ukiwa unatoka Goba center kuelekea njia nne, upande wa kushoto kuna shel kubwa ya Simba oil. Baada tu ya shel. Upande huo huo wa kushoto, kuna kituo cha bodaboda na kuna Hiyo Restaurant.
(Ni restaurant classic kuliko zote Goba ila ina makelele maana iko road kabisa na kuna magenge na kituo cha boda pemben yake).
(Ila kwa Vyakula hapa pako vizur na bei ya Kizalendo).
2. Joy Inn Hotel
Ukiwa unatokea Goba center unashuka njia ya Mbezi Beach -Massana. Utapita shel ya kwanza upande wa Kulia.(Giraffe Oil) Baada ya hapo kwa mbele kuna kituo kinaitwa Lastanza. Kuna bodaboda hapo Ulizia wakuelekeze Joy inn Hotel.
(Iko barabaran. Kituo kinaitwa Osterbay(kituo cha mbele baada ya Lastanza). Hotel ipo Kabla ya kushuka kilima cha Tripple B bar- iangalie pia na hii bar maana iko karibu na Joy in hotel ,ingawa hii haina mazingira mazur).
3. Joy es Slava
Hii ni Bar . Ila kwa nyuma ina Hotel na Restaurant.
Ukiwa unatokea Goba center. Nenda kama unaenda Mbez Magufuli. Kuna Round about (inaitwa njia nne) Nenda kulia kama unaelekea Madale.
Kwa Mbele kama 1 km mkono wako wa Kulia utaona sheli ya Olympic. Baada tu ya Sheli upande huo huo wa kulia ndio ipo Joy es Lava.
Upande wa nyuma ya Bar kuna sehem ya restaurant.
4. BR Hotel and appartment.
Ukiwa unatokea Goba center.. fika round about ya Njia nne. Kata kushoto kama unaenda Matosa.
Upande wa kushoto kama 500m utaona Kiure Engineering .
Upande huo huo kushoto kwa mbele kidogo kuna tuta na kuna kituo cha daladala na kuna kibao cha BR hotel. Ingia na hiyo rough road mita 200 utaona hiyo BR.
Hizi zote ziko ndan ya Radius ya 3 - 4 km.
Ukiwa na gar ni ndan ya dk 20 unazikagua zote na kuona ipi inakufaa.
Pia Google Map kwa msaada zaid wa Picha na mazingira.