Mgahawa wa akina Joti gumzo Sabasaba!

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
MGAHAWA wa wasanii wa vichekesho wa Kundi la Orijino Komedi (OK), umejipatia umaarufu mkubwa na kujizolea idadi kubwa ya watu, wanaohudhuria Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam ‘Sabasaba' yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Tanzania Daima ambalo lilitembelea katika viwanja hivyo, lilikuta watu wakipigana vikumbo kuingia katika mgahawa huo kupata huduma mbalimbali, huku watoto wakionekana kuvutiwa zaidi.

Akizungumza na Tanzania Daima, mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo, Lucas Mhuvile ‘Joti', alisema wamebuni biashara hiyo kama moja ya njia za kuliingizia kundi hilo kipato na kingine kuweza kukutana na mashabiki wao ambao wamekuwa wakiwaona tu kwenye runinga.

Katika shughuli hiyo, Joti alisema wamegawana majukumu ambapo yeye yupo upande wa kushika fedha (mhasibu), wakati upande wa mapokezi yupo Alex Chalamila ‘Mc Regan', huku Mjuni Silvery ‘Mpoki' na Emmanuel Mgaya ‘Masanja' wakiwa katika idara ya upishi.

Kwa mujibu wa Joti, wanajisikia faraja wananchi wanapokwenda katika mgahawa huo kupata huduma na kufurahi nao pamoja, jambo linalowafanya watambue kwamba bado wanakubalika na Watanzania, licha ya kuwepo kwa makundi mengi ya uchekeshaji nchini.

Joti alitumia fursa hiyo kuwataka mashabiki wake kumuunga mkono katika kununua filamu yake ya ‘Kapu la Babu' aliyoiachia sokoni mwezi uliopita, ambayo pia inapatikana katika mgahawa wao huo.

Kutokana na ubunifu mkubwa alioufanya katika kutengeneza filamu hiyo, alisema mtu atakayeinunua hatajutia hela yake.

Source:Tanzania Daima
 
Acha vijana wajitafutie hela

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nimependa huo ubunifu!
 
We chaki haupo msibani ninii
 
Last edited by a moderator:
nimependa ubunifu wa OK wasani wa kibongo wana majina makubwa lakini hawajui jinsi ya kuyatumia ili yawaingizie kipato
 
unapata muda na kuanzisha thread kweli wanadam tunatofautiana.

Watu tonatofautiana mkuu, kwa wakati huu sina mtu wa kubadilishana naye mawazo, kila mtu yupo Stressed.

Kuwepo kwango Jf siyo kwa Leisure bali saa nyingine napata Relief kidogo ya Jambo lililotokea.

Kumbuka Jambo likishatokea hakuna namna tena ya ku-reverse.

Kuanzisha thread mbona ni Copy and Paste tu hai-consume chochote mkuu?

Anyway ahsante kwa kuwa concerned kwa hilo.

Kumbuka hii nilipost kabla sijapata taarifa za msiba.

Ahsante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…