DOKEZO Responded Mgambo na Trafiki wananyanyasa watu Kariakoo, ndio maana Rushwa haiishi!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
photo_2026-07-21_17-05-23.jpg
Mimi ni dereva bajaji, wiki iliyopita Kariakoo ilinifundisha somo chungu kuhusu uonevu ambao hauzungumzwi kwenye runinga au Media.

Ilikuwa mchana wa jua la utosi wakati naingia Kariakoo, nikiwa na abiria wangu, nilielekea kwenye duka moja ambalo mbele yake kuna eneo lililotengwa rasmi kwa ajili ya wateja kuegesha vyombo vya usafiri (Reserve Parking). Nilipunguza mwendo, nikakata usukani kuingia. Ghafla, nikasikia sauti kubwa ya ’paa!’ ikipigwa nyuma ya bajaji yangu.

Kabla sijaelewa nini kinaendelea, vijana kadhaa wa Jiji (Mgambo) waliizunguka bajaji yangu, nyuso zao zilijaa ukali wa kulazimisha. "Wewe unataka kuua watu? Umegonga askari!" alifoka mmoja wao.
photo_2026-07-21_17-05-20.jpg
Nilikumbwa na mshangao! "Nimegongaje nyuma na mimi nilikuwa nikielekea mbele, kaka zangu?" niliwauliza kwa staha nikitegemea busara, bila kunijibu, kwa mabavu na dharau, wawili kati yao walivamia na kuingia ndani ya bajaji yangu. Moja wao akaniambia "Sikiliza wewe, kwanza hapa umeweka Wrong Parking, tupe hela tukutoe la sivyo tunaenda mbele," walishinikiza kwa sauti ya chini.

Nilikataa kwa sababu nilijua sikuwa na kosa, lakini msimamo wangu uliwakasirisha, wakaiwasha bajaji na kunipeleka hadi kwa Askari Trafiki aliyekuwa karibu, wakamwambia kosa langu ni Wrong Parking, hapo ndipo nilipojifunza kuwa kilio cha mnyonge hakina mwangwi.

Yule Trafiki bila hata kupepesa macho wala kutenga sekunde moja kunisikiliza, alinyoosha mkono akachukua funguo yangu ya bajaji, akanyofoa na leseni yangu ya udereva. "Kaa hapo chini," alisema kwa kifupi, kisha akaendelea na mambo yake.

Nilibaki nimekaa kando ya barabara, nikitazama jua likisogea na muda wangu wa kazi ukipotea kwa saa mbili nikiwa kama mateka. Kila dakika iliyopita ilikuwa ni hasara kwangu; abiria wanapita, bajaji imelala, na hesabu ya bosi inanisubiri jioni.

Mwishowe, niligundua kuwa haki yangu haitapatikana kwa kusubiri. Uvumilivu ulinishinda, na njaa ya siku hiyo iliniambia nitapoteza mengi zaidi nikikaa pale. Nilisogea karibu na yule Askari kwa unyenyekevu, nikashusha sauti yangu chini kabisa.

"Boss, yaishe tu." Nilikunja noti ya buku 5 ya jasho langu, nikaidondosha mikononi mwake kiustadi. Bila kuchelewa, kana kwamba alikuwa akisubiri, alirudisha funguo na leseni yangu.

Niliondoka Kariakoo huku moyo wangu ukiwa mzito, si kwa sababu ya kupoteza buku 5 pekee, bali kwa kutambua jinsi tulivyo wadogo mbele ya mifumo ya uonevu, hiyo ndiyo Kariakoo ya wanyonge mahali ambapo sheria hainyooki hadi iwekewe mafuta.

Pia soma ~ Halmashauri ya Jiji Dar: Hatukamati Wanaoshusha au kupakia abiria bali wanaoegesha kabisa
 
Pole sana mdogo wangu, yataisha tuu,uonevu Huwa haudumu!
 
Back
Top Bottom