A
Unaweza kufanya uhuni au utapeli huo Kariakoo tena Msimbazi?Ungeweka namba ya gari tujue ni kweli ni wao halmashauri au ni wahuni tu wa mitaan
Poleni, ila na nyie suala la kufuata sheria za barabarani ni mtihani.Kuna migambo wanazunguka Kariakoo na gari aina ya Fuso wanakamata pikipiki na bajaji kisha zinapelekwa pale Lumumba kisha hutozwa fine Shilingi 50,000 na ikilala kila siku inaongezeka elfu 10.
Mimi ilinitokea nilikuwa nafunga mzigo pembezoni ya barabara yaani kwenye reserve parking ya jengo, huo mzigo ilikuwa box 2 ambazo nilikuwa nazitoa flour ya kwanza, migambo wakanipatia wakaniambia siruhusiwi kufungia hapo mzigo, nikawelekeza mzigo wenyewe nautoa juu floor ya kwanza walinijibu eti ningefungia huko wakaipeleka Lumumba kisha kunitoza shilingi 50,000.
Niliambiwa eti wrong parking kwamba siruhusiwi kupaki pembeni na pia bado hilo zoezi linaendelea na ukitaka uthibitisho njoo Kariakoo.
Kinachofanyika ni kwamba wanatutia hasira sana kwa maamuzi yao hayo, Kariakoo ni sehemu kubw ana kuna watu wengi, yaani mtu akisimama tu wao wanamkamata, kama wanajua kuna sheria kadhaa kwa nini wasiwe wanaeleza watu ili kama inatokea wanaleta ubishi ndio hatua nyingine zinachukuliwa?