MR.NOMA
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 339
- 505
Habari za Leo ndugu zangu, Nimeumizwa na kusononeshwa Sana na tukio lililotokea Leo Majira ya saa 5-6 mchana Jijini Dar - Mtaa wa Kimara Mavurunza, mita chache tu ukitoka kimara DAWASCO kuelekea Kimara Mavurunza.
Vijana wapatao watano wakiwa wamevalia magwanda ya kijani ambapo inasadikiwa kuwa ni migambo waliotumwa na Serikali ya mtaa walivamia nyumba kadhaa katika mtaa huo na kuwaeleza wenye nyumba kuwa wanakagua usafi wa mazingira badae walikuwa wakali Huku wakitishia kuwapeleka watu polisi na waliwaambia watu kuwa Bora watoe Hela elf 50 la sivyo wakienda polisi watatoa zaidi ya laki 2 ili kuwa huru.
Bahati nzuri hakuna mtu aliyetoa pesa yeyote baada ya hapo mgambo hao walikamata watu kadhaaa wasio na hatia ambao pia walishindwa kuwakimbia wakimwemo Ma house girl.
Taarifa nilizonazo ni kuwa watu hawa walienda wakafungiwa katika ofic za mtaa huo na mashahidi wakiwemo vijana waliokamatwa wanasema Wanasema kuwa Walipokuwa kwenye chumba walichohifadhiwa walisikia mgambo na viongozi wa mtaa wakizozana juu ya kuwa wamekamata watu wasio na maana hivyo hawataweza fanikisha Nia Yao. Kiukweli na laani sana tukio hili na nimekwazika sana kwa kilichotokea.
Naomba uongozi wa kata ya saranga Kimara na wilaya ya Ubungo hasa Mkuu wa wilaya utusaidie kufatilia na kuwawajibisha kikundi hiki haramu ambacho kimeleta tafrani na usumbufu kwa raia kwa kutaka kujipatia fedha isivyo halali.
Mgambo Gani Hana kitambulisho na Wala hajaongozana na uongozi wa mtaa.Anatofauti Gani na jambazi?