Mganga amuua Mteja wake na kufukia Mwili Shimoni, Pwani

Mganga amuua Mteja wake na kufukia Mwili Shimoni, Pwani

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia kijana mmoja aitwaye Ally Juma Shaban, Miaka 29, Mganga wa tiba asilia na Mkazi wa Makazi Mapya, Mlandizi kwa tuhuma za mauaji ya Juma Yoram Nyambihira, Miaka 58, Mkazi wa Makazi Mapya Mlandizi.

Inaelezwa mnamo Tarehe 29.08.2025 Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani katika kituo cha Polisi Mlandizi lilipokea taarifa kutoka kwa ndugu wa Juma Nyambihira wakieleza kupotea kwa ndugu yao huyo tangu tarehe 17/08/2025.

Jeshi la Polisi lilifungua Jalada la Uchunguzi na kuanza ufuatiliaji ambapo walimkamata Ally Juma Shaban aliyekuwa akiishi na Juma Nyambihira ikielezwa kuwa ndiye aliyekuwa akimpatia matibabu ya tiba asilia nyumbani hapo kwani marehemu alikuwa na tatizo la uoni hafifu.

Mnamo Tarehe 03.09.2025 Jeshi la Polisi likiendelea na upelelezi walifika nyumbani alipokuwa akiishi Juma Nyambihira na mtuhumiwa kwa ajili ya upekuzi wa kina ambapo walibaini kuwepo kwa tanuri la mkaa maeneo ya karibu na nyumba hiyo huku pembeni ya tanuri hilo kukiwa na dalili ya uwepo wa shimo.

Zilifanyika jitihada za kufukua shimo hilo na kukuta mwili wa marehemu, Ambapo imeelezwa mwili huo utafanyiwa vipimo na daktari kisha kukabidhiwa kwa ndugu ili wafanye taratibu za mazishi na Mtuhumiwa wa kesi hii atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.


Screenshot_20250905-163655_Instagram.jpg



Chanzo: EATV
 
Zilifanyika jitihada za kufukua shimo hilo na kukuta mwili wa marehemu, Ambapo imeelezwa mwili huo utafanyiwa vipimo na daktari kisha kukabidhiwa kwa ndugu ili wafanye taratibu za mazishi na Mtuhumiwa wa kesi hii atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
 
Kama mgonjwa angelikuwa wa kike ningesema mganga kanyimwa papuchi na kuamua kuua kabisa.
 
Back
Top Bottom