Mganga wa diamond aibuka na jipya baada tuzo 7 za diamond.

Mganga wa diamond aibuka na jipya baada tuzo 7 za diamond.

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Yule mganga maarufu wa mastaa nchini ambae
aliwahi kutangaza kuwa amekuwa na ukaribu na
mwanamuziki Diamond ameibuka na kusema
kuwa tuzo hizo saba alizozipata zinamaana
kubwa sana kwenye kazi zake anazozifanya.

alisema" Niliongea na Diamond wiki moja kabla
ya shoo nikamueleza kuwa atapokea tuzo nyingi
sana mwaka huu na hizo tuzo ni ishara tosha ya
kudumu kwenye game kwa miaka kama hiyo ya
tuzo zake kwa maana ya miaka saba mbele yote
nyota yake itaendelea kung'ara" Alisema Dokta
Kamdege
Aidha Mganga huyo aliendelea kusema" Unajuwa
haya mambo ya maagano yapo muziki na miti
shamba zinaendana kwani kwenye dunia hii ya
leo maadui ni wengi kuliko marafiki kwani wapo
watakaokuchukia bila sababu za msingi hivyo ni
vyema ukalijua mapema hilo na kujikinga kama
ilivyo kwa Diamond" Alisema mganga huyo
mwenyeji wHa Mkoa wa Tabora
Hata hivyo mganga huyo aliendelea kuto uwito
kwa watanzania popote walipo duniani
waendelee kupata huduma zake kwani hii ni
kama baraka kwa taifa la Tanzania.
Dokta Kamdege amekuwa akitumiwa sana na
vigogo wa Serikali, wasanii na watu mbalimbali
duniani kufanikisha mambo yao kwa kuwapatia
baraka kupitia miti shamba.
 
Hapa nimeshtuka kitu, huyo nganga ndo wewe na hapa unajipromo ili wasanii wengine waje, na wanasiasa kama ulivyosema. Sawa bwana tumesikia
 
Bila shaka iman yake ina mruhusu! "Tembea na wanawake wengi na uwaimbe ktk nyimbo zako" ndio masharti yake
 
Hapa nimeshtuka kitu, huyo nganga ndo wewe na hapa unajipromo ili wasanii wengine waje, na wanasiasa kama ulivyosema. Sawa bwana tumesikia

Duh wengine wanasema mm msanii , wewe unasema mimi mganga kila mtu anaongea lake kuhusu Mimi, mwisho wa siku hayo yatabaki kuwa mawazo yako tu hakuna ukweli wowote
 
Duh wengine wanasema mm msanii , wewe unasema mimi mganga kila mtu anaongea lake kuhusu Mimi, mwisho wa siku hayo yatabaki kuwa mawazo yako tu hakuna ukweli wowote
Bro usijali ni mitazamo yetu tu.
 
Huyu si alisema dai ataporomoka kimuzikiii imekuajeee
 
Back
Top Bottom