Mganga wa DIAMOND Ajitokeza

Mganga wa DIAMOND Ajitokeza

CompaQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2012
Posts
281
Reaction score
134
MGANGA WA DIAMOND AJITOKEZA
by Teen Newz
1 hour ago
Ustadhi Yahya Michael, mkazi wa
Dar, hivi karibuni amejitokeza na
kudai kuwa yeye ndiye mganga
aliyempaisha mwanamuziki Nasibu
Abdu ‘Diamond Platnumz’ ambaye
kwa sasa ni kinara wa Bongo Fleva,
Risasi Jumamosi lina mkanda
kamili.
MH! SIKU HIZI ANAJIFANYA
SUPASTAA
Akizungumza na gazeti hili katika
mahojiano maalum maeneo ya
Magomeni, Dar, mganga huyo
alidai kuwa pamoja na jitihada
kubwa alizofanya kumpaisha
Diamond lakini anamshangaa kwa
kuwa amesahau alikotoka na
anajifanya supastaa.
Alidai kuwa siku hizi akimpigia
simu, Diamond huwa hapokei,
tofauti na zamani alipokuwa
akihangaika kuchomoka kisanii.
Mganga huyo alifunguka kuwa
sababu ya kufanya hivyo ni baada
ya kuchukuliwa na watu
waliompeleka kwa waganga wa
Kigoma ambako anajidanganya
kuwa ndiyo wanampaisha kumbe
walimchukua akiwa
ameshampandisha kwa kumpa
dawa kali za mvuto.
ALIMPA DAWA GANI?
Alizitaja dawa alizompatia
Diamond kuwa ni mitishamba aina
ya Dubi, Ntajamasala (hii humfanya
watu wamuogope na
kumheshimu), Italigula,
Nkangacharo na Kalila Lila (ambayo
huichoma na kuoga kwa ajili ya
kuwavutia watu).
ANGUKO LA DIAMOND
Alidai kuwa Diamond amejisahau
na hajui kama anguko lake linakuja
kufuatia ahadi aliyoiweka wakati
anaanza kuimba baada ya
kumpatia dawa hivyo atapotea
kwenye muziki.
Akielezea historia ya kukutana
kwao, Ustadhi Yahya alisema yeye
na staa huyo walikutana miaka ya
2000 nyumbani kwa Papaa Misifa
ambaye alikuwa meneja wa
Diamond.
Alidai kuwa kubadilika kwa
Diamond kulikuja baada ya kutwaa
tuzo tatu za Kili mwaka 2010 ndipo
akawa anahusudu wanawake
tofauti na masharti ya dawa
japokuwa alimkanya lakini
hakumsikia.
DIAMOND ANASEMAJE?
Kama ilivyo desturi ya gazeti hili,
lilimgeukia Diamond ili kupata
mzani wa habari hiyo ambapo
alipopatikana kwa njia ya simu
alisomewa maelezo yake yote.
AMKANA
Katika maelezo yake, Diamond
alikataa kata kata kuwa
hamfahamu mtu huyo kisha
akakata simu.
“Sina msikiti nitakuwaje na
Ustadhi? Huyo mganga nasema
simfahamu,” alisema kisha akakata
simu.
source : GLOBAL PUBLISHERS
WEBSITE
 
Msanii na usanii

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
mh kazi, ila jamani watanzania tumezidi kuyaendekeza haya mambo ya kishirikina, maana hata bungeni mambo haya yameshika kasi sana hadi wengine kunaswa na kamera,
 
huyu atakuwa anatafuta promo apate wateja zaidi na wasanii walivyo vichwa vibovu watamiminika kwake na umaarufu hawapati.
Wamwache mtoto wa watu atambe muda wake ukiisha atapotea kama wengine wasianze tafuta sifa za kwamba wao ndio wamempaisha na wao ndio watampoteza kumbe hakuna kitu
 
Huyo mganga nae njaa yake hasemi nayo,kwani waliwekeana mkataba ukipanda usiwache? mganga kweli hajipi wana hasemi siri za mgongwa wake naende uko...
 
Tanzania hii ina watu na matukio kweli
 
Hivi kuna wasanii wasioenda kwa vigagula...hii si habari bali taarifa.
 
Kuna binadamu mwenye akili timamu ambaye anategemea source za Shigongo? Mbona aandiki kwamba Baba yake mzazi aliyekufa kwamba ameonekana Tabata? mpuuzi kabisa huyu jamaa awaache watoto wa watu wapumuwe. kama Mganga anaweza kumpa mtu pesa na mafanikio na ajipe yeye hiyo mitishamba apate pesa yeye mwenyewe.
 
huyu atakuwa anatafuta
promo apate wateja zaidi na wasanii walivyo vichwa vibovu watamiminika
kwake na umaarufu hawapati.
Wamwache mtoto wa watu atambe muda wake ukiisha atapotea kama wengine
wasianze tafuta sifa za kwamba wao ndio wamempaisha na wao ndio
watampoteza kumbe hakuna kitu

We Diamond, usijifanye chizi! wasanii wooote hutegemea tunguri kuvuta nyota lakini huu ndio mwisho wako!
 
Aiseeee.

Nilikuwa natafuta mganga wa kunitoa.

Huyu nishamfuta.
 
Lol! Atakusimanga mchana kweupeee

Si ndo hapo.

Mganga hajui hata ethics za kuweka siri za wateja wake?

Basically kawaambia wengine wote waliokuwa wanafikiria kwenda kwake kwamba wakiingia kwenye database anaweza kuwaumbua muda wowote.

Kama kamfukizia mvuto Diamond mbona yeye hana mvuto kwa Diamond.
 
Mbona wasanii underground wako kibao wanahangaika kutoka, kwanini asiwachukue hao akawapaisha kama alivyofanya wa Diamond (kama ni kweli)? Tena aandikishane nao mikataba ili wakitoka wasije wakamtosa.
 
Back
Top Bottom