Mganga wa DIAMOND Ajitokeza

We Diamond, usijifanye chizi! wasanii wooote hutegemea tunguri kuvuta nyota lakini huu ndio mwisho wako!

kwa hiyo furaha yako jamaa afike mwisgi???kakukosea nn kwan??daah tanzania bhana
WATU WANGU WANABAK MASKIN SABABU YA WIVU NA CHUK
 
Duh wewe una akili sana.
 
Kumbe Ustaadh inatumika hata kwenye uganga...
 
We Diamond, usijifanye chizi! wasanii wooote hutegemea tunguri kuvuta nyota lakini huu ndio mwisho wako!

Naona una illusions mpaka umeanza niita diamond. Achilia mbali kuwa mimi si diamond pia hata hiyo kazi anayofanya si kati ya kazi ambazo naweza fanya na umri wake na wa kwangu tumepishana sana.
 
Mganga huyu ameniacha kitu kimoja,ametaja kuwa mizimu yake itamuadhibu Diamond,huku akisema pia alikuwa akimswalia kwa Mwenyezi,mbona anakufuru?hapa huwa pana nipa shida sana ustadhi ni mshirikina wakati shiriki imekatazwa kabisa,Hili limekaaje ndugu zangu Waislamu?
 
Kumbe Ustaadh inatumika hata kwenye uganga...

Mi mwenyewe huwa natatizwa ninapokutana na waganga wa kienyeji wanaojitanabaisha kuwa maustaadhi
 
Mi mwenyewe huwa natatizwa ninapokutana na waganga wa kienyeji wanaojitanabaisha kuwa maustaadhi

hiyo ni lugha tu ya kiarabu maana yake ni mwalimu so labda yeye mwalimu wa ulozi.
 
huyu jamaa anatafuta watu wa kuwatapeli.....
 
Kama ni kweli ulimshirikisha huyo jamaa basi Diamond unahitaji kutubu na kumrudia Mungu kwani huo ni ukosefu wa akili na kutojiamini. Pili ninachojiuliza hivi mchango wa huyo bwana kwa muziki wa Diamond ni upi ? Kuandika mashairi ? Kuboresha sauti ? Kutengeneza beat nzuri ? ama ? Huyu bwana anatafuta promo kupitia Diamond kama ni kweli Diamond amewahi kumshirikisha kwenye shughuli zake basi iwe ni fundisho kwa wengine. Na yeyote atakayeenda kwa huyu bwana ajue imekula kwake atakuja kudhalilishwa. Na je katika ufanyaji wake wa hizo kazi amewasaidia wangapi ambao wamefanikiwa kufikia level ya Diamond ? Ni kumaanisha kuwa amebahatisha ? Sitaki kuamoni ujinga wa aina hii. Ila Diamond hili liwe ni fundisho, Muamini Mungu na mambo yako yatakuwa sawa daima hakuna zaidi ya Mungu.(ungelikuwa mkristu ningekuambia yesu ndiye njia ya kweli na uzima)
 
Kwani kuamini mungu na kuamini mganga tofauti ya msingi ni nini?
 
tofaut ipo kbwa 2 mungu ni 1 na ukmuamini atkusaidia,lkni wganga ni wengi utaamini wangapi?
 
tofaut ipo kbwa 2 mungu ni 1 na ukmuamini atkusaidia,lkni wganga ni wengi utaamini wangapi?

mkuu usianzishe ligi ya izo vitu na Kiranga...maana haoni vibaya kumtusi Mungu wetu kipenzi,akaturushia stimu waamini.
 
Last edited by a moderator:
tofaut ipo kbwa 2 mungu ni 1 na ukmuamini atkusaidia,lkni wganga ni wengi utaamini wangapi?

Kasema nani? Unajuaje kama mungu ni mmoja? Ushawauliza Wahindu? Kwa nini wewe na imani yako muwe sawa na Wahindu wanaoamini miungu wengi wasiwe sahihi? Kwa sababu wewe umeikuta dini yako kwenu tu?

Na kama wewe unaamini mungu, na Diamond anaamini mganga, wote wawili mnaamini, kimsingi tofauti ni nini kama wote mnaamini?

Kama kuamini kuna tatizo kuna tofauti gani kati ya anayeamini mungu na anayeamini mganga?

Mungu huyo mmoja unayesema unamuamini unamjua historia yake? Kafikaje mpaka ukapata kumuamini wewe? Na kabla yake kiliaminiwa nini na mababu zako?

Anayeamini mganga anaweza kuwa afadhali hata ya anayeamini mungu, maana anayeamini mgamnga anamuona mganga, na dawa isipofanya kazi anaweza kwenda kumdai mganga.

Wewe unayeamini mungu usiyemuona je?
 
mkuu usianzishe ligi ya izo vitu na Kiranga...maana haoni vibaya kumtusi Mungu wetu kipenzi,akaturushia stimu waamini.

Mungu ni deal la watu kuwakandamiza wengine, kuwafariji pale faraja inapokosekana (kama kwenye msiba) etc.

Lakini habari za mungu hazina uthibitisho na ukichunguza sana utaona uzushi tu.

All things supernatural are characterized by human ignorance, intentional obfuscation or wishful thinking. Possibly all combined.
 
mkuu usitafute ban, jf hairuhusu plagarism..........
 
sasa wewe mpagani kamawe unaamini ma-theory yaliyobuniwa na wazungu...acha kudhiaki iman za watu,wewe si umetokana na evolution basi endelea kumdhiaki aliyehasisi evolution eti sababu haumuoni kuna siku utaipata flesh.
 
Mpagani ni nani?

Nani kakwakmbia mimi naamini ma theory? Ya wazungu nonetheless? Nani kakwambia nimedhihaki imani za watu?

Kuhasisi ni kitu gani? "Haumuoni" ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…