Mganga wa kienyeji ahukumiwa miaka 20 jela na viboko 12 kwa kosa la kufuga fisi.

20 haitoshi angetakiwa afugwe miaka 50 pamoja na kulipa fidia. Ili iwe fundisho hasa huko kanda ya ziwa ndiyo wanapenda sana.
 
Watanzania hatupendani tuna chuki binafsi mioyoni mwetu,miaka20 jela na viboko juu kumfuga fisi, ukute alikaokota kakiwa kadogo
 
Mwafrika badala afuge kuku,bata,kanga au mbuzi ambao atauzs apate faida ndani kwake kafungia fisi.Fisi anamsaidia nini haijulikani na faida anayopata kwa kumiliki fisi pia haijulikani
 
Adhabu kubwa kuliko kosa, angemuua angeitwa muwindaji haramu, angalau inge make sense, ila kumfuga tu pasipo kumdhuru sioni kama anastahili adhabu kubwa kiasi hicho, mbona kuna hawa wanaotembea na mijoka mikubwa kwenye maonyesho yao hawakamatwi?
Wataalamu wa Wildlife Act wakuje watupe dondoo tujazie nyama kuhusu hii hukumu
 
Lakini unafuga li fisi la kazi gani wajameni..kwanza ni nyara ya serikali pili likidhuru watu kesi kwako, tatu huna uhuru nalo kutembea nalo mtaani ,nne ni gharama kulihudumia. Ila kudumisha uafrika ni kazi sana
 
Sasa mbona fisi anacheka hivyoo? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Au anafurahia kifungo cha boss wake! Wangemfunga nao ili awe anawatunza ha ha ha
 
Y viboko tena kwa baba wa watu πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Utuwekee na pic yake huyo mfugaji isije kuwa anafanana na huyo fisi anayechekaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ni tapeli, sio mganga, angekuwa mganga wa kweli fisi hangeonekana. Wengi wanafuga ila hayaonekani kwa macho.
 
Waganga wanaowachinjia watoto au kutaka viungo vya albino kwa nafasi zao awakamatwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…