Mganga wa kienyeji Pemba ahukumiwa Miaka 30 kwa kumbaka mteja wake

Mganga wa kienyeji Pemba ahukumiwa Miaka 30 kwa kumbaka mteja wake

G-Mdadisi

Senior Member
Joined
Feb 15, 2018
Posts
165
Reaction score
100
Mahakama ya Mkoa Chake Chake imemuhukumu Mshitakiwa Issa Abdalla Haji mwenye umri wa miaka 41 mkaazi wa shehia ya Wawi Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 30 pamoja na kulipa fidia ya shillingi millioni moja za Kitanzania baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kubaka.

Hukumu hiyo imetolewa jana Oktoba 20 na hakimu wa mahakama ya Mkoa Chake Chake Luciano Makoye Nyengo baada ya mtuhumiwa kukiri kutenda kosa.

Mbele ya hakimu wa Mahakama hiyo imeeelezwa na mwendesha mashtaka Ali Amour Makame kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka kwamba mshitakiwa alidaiwa kumbaka mwanamama mmoja mwenye umri wa miaka 39 jina limehifadhiwa Oktoba 11 mwaka huu wakati mshitakiwa alipomtaka mama huyo wafanye mapenzi ikiwa ni miongoni mwa masharti ya dawa itakayoweza kumtoa mume wake rumande ambako anashikiliwa kwa tuhuma ya kesi ya jinai ndipo mganga huyo alipombaka mama huyo jambo ambalo ni kosa kisheria kwa mujibu wa sheria za Zanzibar ya mwaka, sheria No. 6 YA 2018 kifungu cha 108 kifungu kidogo cha 1, kifungu kidogo cha 3, mabano (b) sheria ya makosa na adhabu Zanzibar.

Mshitakiwa alipotakiwa kujibu shitaka hilo bila ya kupepepsa macho alikiri kutenda kosa hilo, ndipo hakimu wa mahakama hiyo Luciano Makoye Nyengo alipomuamuru mshitakiwa huyo kutumikia miaka 30 chuo cha mafunzo na kumlipa mlalamikaji fidia ya shilling milioni moja ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama hizo.

‘’kwa mujibu wa sheria No. 6 ya mwaka 2018 kifungu cha 108 kifungu kidogo cha 1, kifungu kidogo cha 3, mabano (b) sheria ya makosa na adhabu Zanzibar nakuhumu kwenda chuo cha mafunzo miaka 30 pamoja na kulipa fidia ya shilling millioni moja ili iwe fundisho kwako na kwa wengine wenye tabia kama hizi’’ alieleza hakimu huyo.

Ikumbukwe kuwa mganga huyo alikuwa nje kwa dhamana ambapo anakabiliwa shitaka la tuhuma ya wizi.
 
mshitakiwa alipomtaka mama huyo wafanye mapenzi ikiwa ni miongoni mwa masharti ya dawa itakayoweza kumtoa mume wake rumande ambako anashikiliwa kwa tuhuma ya kesi ya jinai ndipo mganga huyo alipombaka mbaka mama huyo
kwani maza angeikataa dawa ya mnana hiyo ingekuwaje? maana sharti la kwanza kwa mganga ni ukubali ama ukatae masharti - uamuzi huwa ni wa wako.... maza wee sema ukweli...
 
Jamaa kwa akili zake alidhani kwamba atapewa muda wa kuelezea ni kivipi kumuingilia huyo mama kungesaidia mume wa huyo mama kuepuka jela[emoji23][emoji23]

Kumbe hakujua mahakamani ukikiri tuu hakimu hapotezi muda anakulamba hukumu palepale[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Unaweza kuta mteja alikuwa kajaaliwa kidogo ule upande wa nyuma basi Mh Mganga akaone naye ajipoze maisha yaendelee mbele....

Lakini pia inaweza kuwa ndio tekniki ya Mganga kwenda kumtoa mme wa mama huko jela..hahahaha
 
kwani maza angeikataa dawa ya mnana hiyo ingekuwaje? maana sharti la kwanza kwa mganga ni ukubali ama ukatae masharti - uamuzi huwa ni wa wako.... maza wee sema ukweli.
Ni kwamba huoni kosa la mganga? Kama ulivyosema , ukipewa masharti unakubali au kukataa. Siielewi umesoma aje, Ila imeelezwa wazi kuwa alikataa, ndio akabakwa.
 
Back
Top Bottom