Abdalah Abdulrahman
JF-Expert Member
- Aug 29, 2019
- 223
- 202
Dini, kabila, kanda, rangi na asili ya mtu ni sehemu muhimu ya utambulisho na maisha ya watu wengi. Tofauti hizi zimekuwa na nafasi kubwa katika kujenga maadili, tamaduni, mshikamano, huruma na uwajibikaji ndani ya jamii. Tanzania ni taifa lenye utajiri mkubwa wa utofauti wa kijamii na kitamaduni, likiwa na waumini wa dini mbili kubwa (Waislam na Wakristo), makabila zaidi ya 100, wananchi wenye asili ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, pamoja na watu wanaotoka katika kanda mbalimbali za nchi, ikiwemo Kaskazini, Ziwa, Kati, Kusini na Pwani. Pamoja na utofauti huo, Watanzania wamejenga kwa muda mrefu utamaduni wa kuishi kwa amani, kuheshimiana, kusaidiana na kushirikiana bila kuruhusu tofauti za dini, kabila, kanda, rangi au asili kuwa kikwazo cha umoja na mshikamano wa kitaifa.
Hata hivyo, tofauti hizi zinapogeuzwa kuwa chombo cha kuwagawa wananchi, inaweza kutoka katika nafasi yake ya kujenga jamii na kutumiwa kama silaha ya kisiasa, kijamii au kiitikadi. Hatari kubwa si uwepo wa tofauti hizi, bali ni namna tofauti hizo zinavyoweza kutumiwa kuwajenga watu katika makundi yanayopingana vizazi na vizazi.
Swali la msingi tunalopaswa kujiuliza ni hili: Nani anafaidika Watanzania wanapogawanywa kwa misingi ya dini, kabila, kanda au asili, na ninani anayebeba gharama za mgawanyiko huo?
Katika dunia ya leo, vita vingi havipiganwi kwa silaha pekee; ni vita vya matumizi makubwa ya akili, taarifa na ushawishi. Teknolojia ya mtandao imefanya iwezekane kwa mtu au kundi lililo maelfu ya kilomita kutoka Tanzania kutumia mitandao ya kijamii kuwafikia na kuwashawishi kwa muda mfupi mamia au hata maelfu ya vijana, na kuwaelekeza kushiriki katika vitendo vya vurugu, ikiwemo kuharibu miundombinu na mali za umma. Hatari kubwa zaidi ni kwamba ujumbe unaochochea chuki, hofu na hasira unaweza kusambaa kwa kasi kuliko ujumbe unaohimiza utulivu, maridhiano na amani. Katika mazingira haya, uwezo wa wananchi hasa vijana wa kuchambua taarifa, kutambua propaganda na kujiuliza “Nani anafaidika na mimi kufanya hivi?” ni sehemu muhimu ya ulinzi wa amani na usalama wa taifa.
Kutokana na mazingira haya , naona hatari kwa baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini kutumia tofauti zilizopo katika jamii kama nyenzo ya kujenga ushawishi, kuendeleza mgawanyiko au kuimarisha maslahi ya kundi dogo badala ya kutanguliza maslahi mapana ya taifa. Ni katika mazingira haya, tunashuhudia juhudi za maridhiano zinazofanywa na Serikali kugeuzwa kuwa sehemu ya ushindani wa kisiasa badala ya kuwa fursa ya kurejesha mshikamano wa kitaifa. Hivi kweli katika mazingira ya utayari wa Serikali na wadau wengine kuanzisha mchakato wa maridhiano tunapaswa kuipa sharti la kumuachilia mtu mmoja ambaye yuko kizuizini au kujikita katika masuala mapana zaidi yanayogusa haki, amani, utawala bora na mustakabali wa wananchi wote. Uhai wa taifa, amani ya Watanzania na mshikamano wa kitaifa haupaswi kufanywa utegemezi wa hatma ya mtu mmoja, chama kimoja au kundi moja. Kiongozi mmoja akibaki au kuondoka, hilo pekee halipaswi kuwa kipimo cha kama Watanzania wataendelea kuishi kwa amani au katika mgawanyiko na migogoro. Maridhiano ya kweli yanapaswa kujenga mfumo ambao unaendelea kuwa imara hata pale watu na viongozi wanapobadilika, kwa sababu msingi wake ni maslahi ya taifa, si hatma ya mtu mmoja au kikundi cha watu flani.
Maridhiano ya kweli hayawezi kujengwa kwa kumfanya mtu mmoja kuwa kiini cha amani ya taifa, wala kwa kuendeleza mtazamo kwamba mustakabali wa Tanzania unategemea hatma ya kiongozi au kundi fulani. Maridhiano yanapaswa kuwa mchakato mpana wa kitaifa unaolenga kurejesha uaminifu, kuondoa chuki, kusikiliza malalamiko halali, kuheshimu haki na kujenga mazingira ambayo kila Mtanzania anaona kuwa ana nafasi na thamani sawa katika taifa lake. Serikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini, taasisi za kiraia, wasomi, vyombo vya habari na wananchi wote wana wajibu wa kujenga mazingira hayo. Tofauti za kisiasa zinapaswa kushughulikiwa kupitia mazungumzo, sheria na taasisi halali, badala ya kuchochea hisia za kidini, kikabila, kikanda au za asili. Taifa linapoweka maslahi ya pamoja mbele ya maslahi ya mtu au kundi, ndipo maridhiano yanapoweza kuwa msingi wa amani endelevu na maendeleo ya kweli.