Mgao ujao wa umeme…

Mgao ujao wa umeme…

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Inadaiwa mgao wa umeme unakuja. Inadaiwa unaanza tarehe 1 mwezi ujao wa Februari.

Sababu ya huo mgao eti ni matengenezo ya mitambo yao ya wapi wapi huko sijui…

Sasa kwa akili zangu hizi za kidato cha nne, ni kama vile sielewi elewi.

Mbona nchi zingine huwa hakuna migao inayosababishwa na matengenezo ya mitambo ya umeme?

Au zipo? Kama zipo, basi sawa. Ila kwa nchi nizijuazo mimi, kamwe hata mara moja sijawahi sikia eti kutakuwepo na mgao au migao ya umeme kwa sababu mitambo ya kuzalisha au kusambaza umeme inafanyiwa ukarabati.

Hao wenzetu wao mitambo yao huwa haihitaji ukarabati? Kama huwa inahitaji ukarabati, wanawezaje kuepuka migao ya umeme?

Kwa nini sisi kila mitambo inapohitaji ukarabati [ kama ni kweli inahitaji huo ukarabati] basi kunakuwepo na mgao?

Manake hili si jambo geni. Limekuwepo siku zote. Sasa miaka yote hii hawa watu hawajaweza tu kubuni namna ya kuikarabati hiyo mitambo bila kuleta usumbufu wa migao?

Tanesco….and whoever else involved….seriously????

NB: Halafu nani anaamini huu mgao utakuwa ni wa siku 10 tu????? Mimi siamini….
 
Huu mgao mpya utaanza lini kwa maana tayari tuna mgao kuanzia siku ile january Makamba alipoteuliwa kuwa waziri wa nishati badala ya Kalemani.
 
Tutamkumbuka Sana uncle Magu chini yake hakukuwa na tatizo la umeme wala maji aliwapiga beat Tanesco hata kabla yakuingia madarakani, kiufupi tunarudi kwenye maisha tuliyoyazoea hii nchi inatakiwa impate raisi ambaye ni mkali asiyependa masiala na mwenye maamuzi magumu sasa huyu Raisi wasasa anaendeshwa kwasababu ni mpole na hana maamuzi magumu so watu watamchezea wanavyotaka.Ukali wa Magu ulisaidia hii kunyooka kulikuwa na taarifa eti maji ya kidatu kupunguza Mara kwa Mara kipindi Cha kikwete lakini tangu aingie Magu Huu upuuzi ulikuwa haupo.
Nyani Ngabu
 
R.I.P JPM hii yote ni kufanya jambo kwa kumuwaza JPM asimgekufa ina maana kuna siku umeme ungekatika.

Hawa wanataka kubadili mfumo wa kupokea pesa hawataki pesa wazikose kama kipindi kileee saivi wapo serious kushirikilia kila sehemu vibaki kwa ajili ya vizazi na vizazi vyao .

hii nchi ni yetu sote sio ya watoto wa vigogo mbona nyerere hajatufanyia hivi ila wao wanataka kushika kila kitu huyu aridhi,huyu habari ili kuzuia na kuelekeza propaganda huyu mwingine anapiga msumali matrillioni yakae ndani mwao.
 
Tusubiri tuone labda kuna umuhimu wa kufanya hivyo na halikwepeki.
Na kama sivyo ni hatari kwa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya mtu mmoja-mmoja.
May be it's business as usual and subjection to a vicious cycle (Watcha You Gonna Do !!?? That's Why !!!!)
 
Inadaiwa mgao wa umeme unakuja. Inadaiwa unaanza tarehe 1 mwezi ujao wa Februari.

Sababu ya huo mgao eti ni matengenezo ya mitambo yao ya wapi wapi huko sijui…

Sasa kwa akili zangu hizi za kidato cha nne, ni kama vile sielewi elewi.

Mbona nchi zingine huwa hakuna migao inayosababishwa na matengenezo ya mitambo ya umeme?

Au zipo? Kama zipo, basi sawa. Ila kwa nchi nizijuazo mimi, kamwe hata mara moja sijawahi sikia eti kutakuwepo na mgao au migao ya umeme kwa sababu mitambo ya kuzalisha au kusambaza umeme inafanyiwa ukarabati.

Hao wenzetu wao mitambo yao huwa haihitaji ukarabati? Kama huwa inahitaji ukarabati, wanawezaje kuepuka migao ya umeme?

Kwa nini sisi kila mitambo inapohitaji ukarabati [ kama ni kweli inahitaji huo ukarabati] basi kunakuwepo na mgao?

Manake hili si jambo geni. Limekuwepo siku zote. Sasa miaka yote hii hawa watu hawajaweza tu kubuni namna ya kuikarabati hiyo mitambo bila kuleta usumbufu wa migao?

Tanesco….and whoever else involved….seriously????
Mkuu inaonekana umerudi bongo tuisome namba kwa pamoja

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom