Mgao ujao wa umeme…

Mgao ujao wa umeme…

Ila kuwa kiongozi bongo ni raha sana,unaangalia tu watu wanavyobweka mitandaoni huku yako yanaenda kama ulivyopanga.
 
Kwani taarifa ya Tanesco inasema ni matengenezo ya mitambo au bomba la gas? Rejea taarifa ya Tanesco then tuendelee kujadili.
Ni bomba la gesi boss...nilichanganya ma-file....samahani
 
Kila hitilafu ikitokea inakuwa oh...fulani angekewepo isingetokea!!
Hata mashine zinachoka na kuhitaji ukarabati...
"Mpaka mvua ikichelewa kunyesha itasemwa kwa kuwa fulani hayupo.."
Tusubiri wahusika watujulishe sababu ya mgao na sio kuangalia nani yupo nani kaondoka...
Miaka sita ya magu hakukuwa na huo ukarabati? Mbona umeme ulikuwepo?
 
Hadi mwaka jana, inakadiriwa kuwa uzalishaji wa umeme kwenye gridi ya taifa ulikuwa 1,604MW, huku mahitaji kwenye grid yalikuwa 1,180MW...

Sasa ikitokea chanzo kimoja kikubwa kimezimwa, ndipo hapo upungufu unapojitokeza...

Kitu ambacho nadhani Waafrika kimekuwa kikitukwamisha, ni kutojua au kutilia maanani vipaumbele...

1604MW, kiwango hiki ni chini ya matarajio ya sera ya nishati, ambayo ilikadiria kuwa hadi kufikia 2020, Tanzania ingekuwa ikizalisha si chini ya 5,000MW za umeme kwenye gridi ya taifa, hasa baada ya ugunduzi wa gesi asilia...

Huu ndio ule wakati Waziri Muhongo na wanasiasa wengine walijigamba kuwa mgao wa umeme kuwa historia Tanzania...

Kwa mujibu wa takwimu, matumizi ya bomba kubwa la gesi lile la (Mtwara <> Dar) ni asilimia 6 tu, huku asilimia 94 zikiwa hazitumiki...

Iwapo bomba hilo lingetumika kwa uwezo wake kwa angalau asilimia 50 tu, lingesaidia kuongeza umeme wa uhakika...
Ni kwanini hiyo asilimia 94 haitumiki?
 
Hapa kwenye umeme likiendekea hivi basi ni suala la muda tu hata tunaomsapoti na kuyavumilia mapungufu hatutamuelewa.
 
KOREA KUSINI!!!!!!!!!!!!!!!.................................
Unafananisha kifo na usingizi, wanatumia umeme wa mabwaha??? Korea Kusini ina viwanda 14 vilivyo kwenye Fortune Global 500.

Soma hapo kuhusu Korea Kusina:

Electricity generation in the country mainly comes from conventional thermal power, which accounts for more than two thirds of production, and from nuclear power. .
Uko sahihi. Je, umeme huo hauna mtambo wowote ule ambao unahitaji matengenezo kwa miaka zaidi ya 30.?
 
Safi sana!

Mama anafungua nchi!

Tuliaonewa sana kwa miaka 5!

Tunapumua!

Push Gang Mtapata tabu sana!!!

Watu wanajenga sana mtaani , mzunguko mkubwa!! Enzi za mtu wenu hali ilikuwa mbaya sana unaweza ukatembea umbali wa 2km hauoni ujenzi ukiendelea ila sasa kila mita 100 unaona watu wanaporomosha mijengo.
 
Basi utakuwa dogo sana wewe.

Mgao wa umeme upo tokea utawala wa Mwinyi.
Kwa kutaja miaka hiyo sio justification ya kusema mimi ni mdogo , miundombinu ya utawala wa mwinyi haikua imara kihivyo nimetoa mfano hai kwa miaka ambayo hata awareness kubwa kwa watanzania ilianza kuwepo ndio hiyo miaka mgao wa kukumbukwa sana zama za karibuni ni 2006 & 2007
 
Kwa kutaja miaka hiyo sio justification ya kusema mimi ni mdogo , miundombinu ya utawala wa mwinyi haikua imara kihivyo nimetoa mfano hai kwa miaka ambayo hata awareness kubwa kwa watanzania ilianza kuwepo ndio hiyo miaka mgao wa kukumbukwa sana zama za karibuni ni 2006 & 2007
Mimi naikumbuka sana migao ya miaka ya 80 mwishoni na miaka ya 90!
 
Inadaiwa mgao wa umeme unakuja. Inadaiwa unaanza tarehe 1 mwezi ujao wa Februari.

Sababu ya huo mgao eti ni matengenezo ya mitambo yao ya wapi wapi huko sijui…

Sasa kwa akili zangu hizi za kidato cha nne, ni kama vile sielewi elewi.

Mbona nchi zingine huwa hakuna migao inayosababishwa na matengenezo ya mitambo ya umeme?

Au zipo? Kama zipo, basi sawa. Ila kwa nchi nizijuazo mimi, kamwe hata mara moja sijawahi sikia eti kutakuwepo na mgao au migao ya umeme kwa sababu mitambo ya kuzalisha au kusambaza umeme inafanyiwa ukarabati.

Hao wenzetu wao mitambo yao huwa haihitaji ukarabati? Kama huwa inahitaji ukarabati, wanawezaje kuepuka migao ya umeme?

Kwa nini sisi kila mitambo inapohitaji ukarabati [ kama ni kweli inahitaji huo ukarabati] basi kunakuwepo na mgao?

Manake hili si jambo geni. Limekuwepo siku zote. Sasa miaka yote hii hawa watu hawajaweza tu kubuni namna ya kuikarabati hiyo mitambo bila kuleta usumbufu wa migao?

Tanesco….and whoever else involved….seriously????

NB: Halafu nani anaamini huu mgao utakuwa ni wa siku 10 tu????? Mimi siamini….
Ile reshuffle ya Bodi ya Tanesco plus safari ya UAE zinaanza kutoa majibu
 
Uko sahihi. Je, umeme huo hauna mtambo wowote ule ambao unahitaji matengenezo kwa miaka zaidi ya 30.?
Nchi zilizoendelea zinatumia vyanzo tofauti na sisi kupata umeme..na zina "back up" ya uhakika wanapokarabati mitambo yao..hivi umesika kinu cha nyuklia cha kuzalisha umeme? Sisi bado sana...wacha tukarabati kwanza hivi vya mabwawa.
 
Back
Top Bottom