Tuna report shida ya maji kila siku ila ndo hivo suluhu hamna takribani miezi 6 sasa
Habari, mimi ni mkazi wa Goba, Mtaa wa River View, nahudumiwa na DAWASA Makongo lakini mtaani kwetu imekuwa ni desturi sasa maji hayatoki miezi sasa! Japo ratiba yetu ya mgao ni Alhamis na Jumatatu lakini hata katika siku hizo maji hawayafungui makusudi! Tumepiga simu sana lakini DAWASA hawana msaada badala yake tunauziwa maji ya tank kwa 40,000! Hii inatuhumiza saanaa.
Tangu 2025 wanatuambia kuwa mgao wetu ni Jumatatu na Alhamis lakini cha ajabu Jumatatu maji hayatoki na wala Alhamis maji hayatoki huku kwetu maji yanaweza kukaa hata miezi miwili hayatoki
Tume-report DAWASA kwa viongozi, tumeripoti kwa Bwire CEO mpaka sasa hamna kilichofanyika kila siku maji hamna, tunauziwa maji ya tank elfu 40, je Mtanzania wa kawaida anaweza nunua maji ya elfu 40 kila wiki?
Tusaidie kupaza sauti maana tume-report toka mwaka 2025 mwezi wa 8 hakuna kilichofanywa mara tuambiwe TANESCO wamekata umeme wameshindwa washa mtambo, naandika kwa hisia kali kwa sababu wanakeraaa, lengo ni kukata maji tuuziwe maji ya tank?
======
Nimerejea hapa Oktoba 2026, bado ni changamoto, na wala hakuna dalili ya kutatua, tunapigwa Kiswahili kila siku mara wingi wa watu mara sijui presha ndogo ila mwaka 2025 hali haikuwa hivyo.
Pia soma ~ DAWASA yaelezea sababu ya kuyumba kwa huduma ya maji Goba River view