Razorblade
JF-Expert Member
- Aug 30, 2019
- 337
- 753
Habari!
Kumekuwa na kundi kubwa la watu hasa vijana ambao wanashindwa kujua namna ipi nzuri na rahisi ya kugawa pesa zao kulingana na mahitaji yao.
Naomba nitoe ushauri na kupendekeza njia rahisi inayoweza kuwa msaada kwa wengi katika kufikia malengo.
Njia hii ambayo imeelezwa kwenye kitabu cha All Your Worth: The Ultimate Lifetime Money Plan(Published 2005) kilichoandikwa na Elizabeth Warren pamoja na binti yake Amelia Warren.
Njia hii inahusisha ugawaji wa pesa kulingana na mahitaji kwa kutumia asilimia(%) kama ifuatavyo;-
50%(Mahitaji Muhimu)
Haya ni mahitaji ya lazima kwa mtu, sehemu hii inahusisha malazi, makazi na chakula na inaweza kuhusisha usafiri pia.
30%(Mahitaji Mengineyo)
Sehemu hii inahusisha mahitaji ambayo sio ya lazima kulingana na mahitaji ya mtu husika.
20%(Akiba)
Hii ni sehemu muhimu zaidi, kila mtu anapaswa kujaribu kutenga kiasi kama akiba au uwekezaji. Hatua hii inaweza kusaidia zaidi inapojitokeza dharura au kufikia malengo fulani.
Muhimu: Njia hii inategemea na mahi taji ya mtu husika.