Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Nimeona vigogo wa TANESCO wakitutahadharisha watanzania kuwa kutokana na ukame uliolikumba Taifa letu, kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, wamelazimika wao TANESCO kuanzisha mgao wa umeme nchi nzima, kutokana na mabwawa ya Kihansi, Mtera na Kidatu, kupungukiwa maji ya kuyajaza mabwawa hayo kutokana na ukame na hivyo kulazimika kuizima mitambo hiyo uliosababishwa na tabia nchi.
Ndipo hapo ninapojiuliza, hivi pamoja na kutumia matrillioni kadhaa ya pesa, kwa ajili ya kujenga bwawa la Nyerere, ambalo watawala wetu wamekuwa wakilipigia "promo" kubwa Sana, kuwa ndilo litakalokuwa "muarobaini" wa tatizo letu la umeme nchini, kwani litakuwa linazalisha umeme usiopungua Megawatts 2,000 hivi kwa mwenendo tunaokwenda nao wa ukame unaosababishwa na kile kinachoitwa mabadiliko ya tabia nchi, ambapo inategemea kudra ya Mwenyezi Mungu kuendelea kuileta mvua itayojaza mabwawa hayo, je mgao huu wa umeme utaendelea kuwepo nchini, hata pale tutakapoufungua mradi huo mkubwa wa umeme wa bwawa la Nyerere?
Swali lingine ambalo ningependa kuwauliza hao TANESCO, hivi hii miradi ya uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia yetu tuliyoivumbua huko Mtwara, ambayo nayo imeligharimu Taifa letu matrillioni ya pesa, ina maana nayo ni white elephant projects?
Kama kawaida ya watawala wetu, kutuona watanzania wote ni wajinga wa kupitiliza, tunaoweza kudanganywa wakati wote!
Naomba hayo maswali machache nijibiwe na hao wataalamu wetu wa TANESCO