Mgao wa umeme uliotangazwa na TANESCO kwa ajili ya ukame. Je, tutegemee mgao zaidi hata litakapokamilika bwawa la Nyerere?

Kama na lenyewe linatumia maji ya mvua kama mabwawa mengine uliyoyataja hapo juu, basi nalo litakuwa prone to draught. Ukame ni ukame. Kisichokauka kwa ukame ni bahari tu...
 
Kama na lenyewe linatumia maji kama mabwawa mengine uliyoyataja hapo juu, basi nalo litakuwa prone to draught. Ukame ni ukame. Kisichokauka kwa ukame ni bahari tu...
Absolutely true👏👏👏
 
Mto Ruaha maji yamepungua sana
Yamepungua kuanzia eneo gani? mwanzoni mwa oktoba nimepita barabara ya Iringa -Mikumi kupita milima ya udzungwa maji yanatiririka kwa kasi utafikiri ni wakati wa masika. Labda kama waliyafungulia kwa makusudi huko mtera.
 
Yamepungua kuanzia eneo gani? mwanzoni mwa oktoba nimepita barabara ya Iringa -Mikumi kupita milima ya udzungwa maji yanatiririka kwa kasi utafikiri ni wakati wa masika. Labda kama waliyafungulia kwa makusudi huko mtera.
Nilikuwa Ruaha National park Mto una maji machache sana
 
Niko huku masaka panya rodi huu mradi hahuitaji umeme,pole huko.
 
Hakuna Cha ukame hii ni Ile staili ya kugungulia mabwawa ili watu wapige ela hapa naona harufu ya iptl kurudi nakumbuka magu alisema kulikua na wajanja wachache wanaotengeneza ukame Kwa faida yao hatujasahau hayo bado
Acha kujitoa ufahamu, kwani mvua hunyesha kwa kificho kusema watu watajua kuwa mvua zipo za kutosha ama la? Unashangaza
 
Kama hakuna mvua waziri aseme nini? Walipoanza mradi wa bwawa la Nyerere viongozi walijua kabisa kuwa mabadiliko ya tabia nchi yapo, na mvua hazitabiliki- wao hawakuamini wataalamu ila wakatumia utashi wao.
Kwa miaka 60 unatumia hydropower plant...kusingekuwa na uchepushwaji na hujuma maji yanatosha sana. Nyerere dam bado ni mradi sahihi na litakuwa na reserve kubwa sana kukabiliana na ukama kuanzia kuutunza umeme mpaka maji.
 
Hiv hawa Wafanyakazi wa Tanesco hakuna mzalendo hata mmoja akatoa siri nn kinafanyika huko? Kweli maji yamekauka au watu wanafungua mabwawa ili upigaji uendelee?
 
Kama kutakuwa na Ukame mgao utakuwepo
 
Hiv hawa Wafanyakazi wa Tanesco hakuna mzalendo hata mmoja akatoa siri nn kinafanyika huko? Kweli maji yamekauka au watu wanafungua mabwawa ili upigaji uendelee?
Ni vyema tukaelezwa ukweli.

Rais wa awamu ya 5, Hayati Magufuli alitoa tuhuma nzito kuwa watendaji wa mabwawa hayo huwa wanayafungulia mabwawa hayo na kuyamwaga Maji, Ili walete "artificial" mgao Ili waendeleze "dili" zao za kuuza jenereta😎

Tunaomba watendaji wa TANESCO wajitokeze hadharani waweze kuyakanusha au kuyakubali maelezo hayo ya Hayati Magufuli
 
Hakuna sababu za maana za kututesa wananchi na kutuletea mgao wa Umeme baada ya miaka 61 ya uhuru, badala yake ninauona mgao huu kama "dili" ya watendaji wetu wakuu wa wizara ya nishati, ya kuuza majenereta yao😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…