TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 5,771
- 17,849
Hakuna haja ya salamu.
Unajua kuna vitu unaweza kupiga siasa, ukapiga porojo, ukatia nakshi nakshi, ukatetea nk na watu wakakuelewa. Ila inapokuja kwenye vitu ambavyo vinaonekana wazi na vinaathiri maisha ya watu MOJA KWA MOJA kunakua hakuna kiasi cha porojo, siasa, mbwembwe wala maneno matamu yanayosaidia!
Hivi ina maana nchi nzima hii ya Tanzania yenye Rais, Makamu wa rais wawili, Waziri mkuu, mawaziri, wabunge, maprofesa, mainjinia, wataalam, vyanzo vya maji vya kila aina, upepo, jua, gesi, nk yaani imeshindikana kabisa kwa miaka 60 sasa kuwa na umeme wa uhakika?
Hivi tuna kipi cha kujitetea, tuna maneno gani ya kuongea, tuna porojo zipi za kupiga kuonyesha ni sababu gani imepelekea mpaka leo hii nchi inaingia gizani? Na bila AIBU tanesco inatoa ratiba ya mgao wa umeme, as if ni kitu cha kawaida tu wala hakuna tatizo lolote.