Mgao wa umeme unaivua nguo Serikali

Hivi 'Dipiweldi' hawadili na umeme pia, ili tuwape tu hili shirika letu? Au mnasemaje ndugu zangu?
Hili dude tuliwahi kuipa kampuni moja toka kwa Madiba ili iliendeshe. Matokeo yake ikaleta matatizo makubwa na ubabaishaji hadi Serikali ikaamua kuwatolea nje. DPW tuwaache tu waendelee kutuliza huko mwaloni.
 
Kwakweli huyu mama Hana uwezo kabisa wa uongozi, kila Kona wahuni wanapiga hujuma yeye Wala haelewi kitu
 
Mwaka jana wamelalamika mvua hamna,mwaka huu mvua zimenyesha sana.Sasa sijui watakuja na ngojera gani.

Bi Mkubwa akae akijua wahuni sio wa kucheka nao, mara vituo na miundo mbinu chakavu havifanyiwi mantainance, Bi Mkubwa kawapa hela mwaka umepita hamna kitu.
 
Huyo Mmama tunayemlalamikia Nahisi hata Unit moja Ya umeme Hajui ina cost shingapi

I agree 400%. Hajui unit ya umeme shiing ngapi. There is no way anajua.

Wakati LUKU zinaanzishwa Samia alikuwa mlamba asali tayari, Samia hajawahi maishani kwenda kibanda cha wakala kununua LUKU.

Na hapa ndio tunakosea, tunachagua watu ambao sio wenzetu, hawajawahi kuishi shida zetu.

Tuko kwenye depression, umeme hakuna, dollar hakuna, maji hakuna, petroli na diesel hazishikiki, familia zinalala njaa, absolute economic catastophe, Rais yuko busy kununua magoli ya wacheza mpira. Heartless kleptocrats.
 
Niko mtela bwawa la maji yamepungua sana hata kama Magufuli angekuwepo labda ange kojelea bwawa likajaa hili mgao uishe
 
Niko mtela bwawa la maji yamepungua sana hata kama Magufuli angekuwepo labda ange kojelea bwawa likajaa hili mgao uishe
Maji yameenda wapi? Au ngombe wamekunywa? Hivi jenereta bei gani
 
Niko mtela bwawa la maji yamepungua sana hata kama Magufuli angekuwepo labda ange kojelea bwawa likajaa hili mgao uishe


Angekuja na mbadala wa ufumbuzi wa tatizo.

Asingepata usingizi hadi ufumbuzi wa tatizo la kukosekana Kwa Umeme na maji lipatikane.
 
Watanzania mlishazoea mgao...endeleeni kusema mama anaupiga mwingi..magufuli alisema iko siku mtamkumbuka...yaani Magufuli asafishe halafu mama awarudishe kazini wapiga dili wakiongozwa na makamba unategemea nini.Mgao wa umeme Tanzania ni COOKED fully stop. .Biteko ndio kwanza kaingia hana kosa kijana wa watu ila anakazi kubwa ya kusafisha ufisadi na madudu ya mtangulizi wake
 
Wacha mama aupige mwingi,tutanyooka tu!
 
Shirika wazawa kuliendesha limetushinda heri libinashishwe waje wazungu tu waliendeshe kwa mwendo huu hapana
 
Sasa viongozi wanafanya nini kama wameshindwa kutatua tatizo dogo tu la umeme? Huko si kuvuliwa nguo hadharani?
Ukiwauliza watakujibu kirahisi tu.
'atafutwe muwekezaji kutoka Dubai'
Watu wamekalia viti kufikiri hawataki. Wanataka muarabu aje awafikirie na kuwapa rushwa.
 
Kama Nchi inabidi Ifike mahali Tukubali tu Kwamba Kiongozi wa Nchi Hii Nchi imemzidi Nguvu hebu 2025 akae Kando Tu Kupisha Aibu ndogo ndog Kam hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…