Mgawanyiko bora wa chakula kwa afya yako

Mgawanyiko bora wa chakula kwa afya yako

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
1553133629382.jpeg


Kama utaweza kula mkate wa kahawia badala ya mkate mweupe, mkate wa kahawia una fibre ambazo husaidia kusafisha utumbo mkubwa na kurahisisha upatikanaji wa choo.

Punguza ulaji wa nyama nyekundu na kuongeza ulaji wa kuku na samaki. Ukiweza tumia mafuta ya nazi au mafuta ya mzeituni (olive oil).

Kama ukijijengea tabia ya kula baadhi ya mboga bila kupika ni tabia nzuri sana. Unaweza kuanza na carrot moja kwa siku, unaweza kujikuta unakula tango, hoho, carrot kila siku. Ukifikia stage hii utawashangaa wanaolalamika kutokupata choo kila siku.
Kunywa maji ni muhimu, hata kama una uwezo wa kununua soda kusindikizia chakula, unaweza kuamua kunywa maji badala yake. Soda iwe ni kiburudisho cha nadra mara mbili au tatu kwa wiki.

Hasa kwa wale wanaoendesha magari. Hakikisha unafanya mazoezi angalau masaa mawili kwa wiki. Safari fupi unaweza kutembea. Kwa wale wa TZA 111 tunafanya sana mazoezi hasa tunapopungukiwa nauli ya mwendo kasi.

Punguza unywaji wa pombe, kunywa bia moja kila baada ya siku moja si mbaya. Ikiwezekana acha kuvuta sigara.
 
Back
Top Bottom