sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,745
- 1,171
Friedrich Nietzsche anatuambia kuwa A politician divides mankind into two classes: tools and enemies.
Pia kuna msemo usemao divide and rule.
Nauona mshikamano na umoja wa kitaifa ukipangaranyika siku hadi siku.
Ombwe kubwa la umoja wa kitaifa limesababishwa na wanasiasa, wanao pingana kisera katika kutaka madaraka ya kutawala na kuwaongoza wananchi.
Hapo ndipo dhana ya Friedrich Nietzsche
inapo jidhihirisha kuwa wanasiasa huwagawa wananchi katika makundi mawili,zana na adui.
Zana, ni wananchi wanao tumika kama nyenzo ya wanasiasa kupandia jukwaa la kusaka uongozi, wakati huo huo uadui unajengwa katika misingi ya kundi linalo hasimiana na malengo ya wanasiasa hao.
Hapo ndipo wanasiasa waliopata dhamana ya kiuongozi wanapo tumia njia ya kutugawa ili watutawale.
Ikifikia hali hii, mshikamano na umoja wa kitaifa unapoteza mwelekeo.
Katika nchi yetu dhana zote mbili yaani zana na uadui umetamalaki, hali inayo mnufaisha mtawala kutawala atakavyo kwa kuwa ana tumia kundi la zana ya kukubalika kwake ili kurahisisha mambo yake.
Lakini zana hiyo ina tengeneza uadui miongoni mwa wasio kubaliana na matakwa ya mtawala, hapo ndipo shida inatokea.
Hapo ndipo yanapo ibuka makundi ya wafuasi wakijiita wana harakati wanao mtetea mtawala na wanaharakati wanao tetea maslahi ya umma(wanyonge).
Ifike mahala tujiulize kama sisi ni Watanzania na Tanzania ni nchi yetu,kwanini tuna tengeneza matabaka ya wenye haki na wasio na haki ndani ya taifa moja.
Taifa lililo tumia nguvu ya hoja kuunganisha mshikamano na umoja wa kitaifa,bila kubaguana.
Leo tuna baguana kutafuta ushawishi na utashi wa kuongoza dola.
Kuna ulazima wa kujiuliza mambo yafuatayo.;
√√ Kwanini tuna tengeneza uhasama na chuki miongoni mwetu na kusababisha majeraha na vidonda visivyo tibika kwa sababu ya kuyalinda madaraka.
√√ Madaraka haya yana nini kinacho sababisha watawala kuvaa miwani ya mbao, inayo wazuia kuona utengano, uadui na maovu yanayo tendeka kwa dhana ya ufuasi wa kumlinda fulani (tools).
√√ Tukisha tumika kama zana ya kuwanufaisha wanao jiona wana haki na Tanzania kwa kuwajengea uadui unao wamaliza kwa viashiria vya kutekana, kutishana, kunyimana haki, nini kitafuata.
Wenzetu mathalani jirani zetu hapa Kenya, wamevuka mstari wa ubinafsi ulio taka kuliangamiza taifa lao. Wameondokana na nadharia ya Friedrich Nietzsche,wanasaka umoja na mshikamano wa kitaifa.
Wamegundua kabla ya vyama vya siasa kulikuwa na nchi yao, ambayo wote wamezaliwa ndani yake kwa maana ya Mama mmoja,Kenya.
Utengano wa watoto wa mama Kenya kwenye maslahi ya nyenzo ya vyama vya Siasa,usiwagawe kwenye misingi ya umoja wao, zana(tools) Kwa maana ya vyama vya siasa iwe ni njia ya kushindana kisera kutafuta utashi wa kuongoza bila kuathiri mshikamano wa wana wa Kenya.
Kwa mantiki hiyo BBI imezinduliwa rasmi kama mkakati wa maridhiano kwa usalama wa Taifa lao.
Tanzania ni ya Watanzania, hakuna wenye miliki na nchi hii zaidi ya Watanzania, kwa utashi huo kila Mtanzania ana haki na nchi hii bila kujali tofauti zetu za kiitikadi kuliongoza Taifa letu,bila kulazimisha kwa utashi wa matwaka yake pasi na ridhaa ya Watanzania.
Tukilijua hili, utete wa usalama wetu hautakuwa mashakani.
Mihimili yote ifanye kazi kwa misingi na matakwa ya wananchi, hapo ndipo dhana ya sovereignty state itakapo kuwa na mashiko.
Viva Tanzania viva