Mgawo wa Umeme umerudi upya baada ya kukamilika kwa Bwawa la Mwalimu Nyerere?

Waka Waka

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2024
Posts
1,333
Reaction score
2,076
Habari,

Hali ya mgawo wa umeme imerejea kwa kasi sana ni wiki tangu kuanza kwa changamoto hii. Ndani ya jiji la Dar es Salaam wilaya ya kinondoni hali sio nzuri.

Watanganyika tulijua baada ya Bwawa kukamilika ingekua ni mwarobaini tosha ya kukatika katika huku. TANESCO wilaya wametenga masaa 12 ndio warejeshe umeme kila wanapo kati umeme. Hii ni mbaya kwa uchumi wa Tanganyika hii.

Kuna tetesi pia kua Tanganyika inauza umeme Zambia huko hali yao sio poa kabisa. Kama mnauza mmeamua sisi tuteseke?

TANESCO tunaomba mtutangazie ratiba kamili kuhusu mgawo huu.

Kwa maana fupi BWAWA LA MWL NYERERE sio mkombozi kwa taifa.

ASANTE.
 
Tanesco wilaya ya kinondoni tunaomba majibu hapa. Kuhusu huu MGAO
 
Niko Kigamboni, eneo ninaloishi umeme unakatika hata mara tatu kwa siku ila hauzidi dakika 10 unarudi. Pia tulikuwa na tatizo kubwa la low voltage limeisha sasa. Sikumbuki mara ya mwisho ni lini umeme ulikatika kwa muda mrefu. Kwa mara yavkwanza naweza kusema Tanesco wanajitahidi.
 
Tanesco wilaya ya kinondoni tunaomba majibu hapa. Kuhusu huu mgao
 
Niko Kigamboni, eneo ninaloishi umeme unakatika hata mara tatu kwa siku ila hauzidi dakika 10 unarudi. Pia tulikuwa na tatizo kubwa la low voltage limeisha sasa. Sikumbuki mara ya mwisho ni lini umeme ulikatika kwa muda mrefu. Kwa mara yavkwanza naweza kusema Tanesco wanajitahidi.
Kwa kigamboni sw.lakini kinondoni wakikata ni masaa 12. Na bila taarifa kiongozi.
 
Screenshot_20240913-165615_Instagram.jpg
 
Niko Kigamboni, eneo ninaloishi umeme unakatika hata mara tatu kwa siku ila hauzidi dakika 10 unarudi. Pia tulikuwa na tatizo kubwa la low voltage limeisha sasa. Sikumbuki mara ya mwisho ni lini umeme ulikatika kwa muda mrefu. Kwa mara yavkwanza naweza kusema Tanesco wanajitahidi.

Hata ubungo hivyo. Umeme unakatika katika ila hauchukui dakika 10 unarudi fasta

Kwa miezi ya karibuni Sijawai kuona umeme umekatika masaa kazaa mfululizo
 
Hili lipo karibu nchi nzima Kwa watumiaji wa Gridi ya Taifa
 
Nilipo hakuna huo mgao wala sijausikia,kwani hilo bwawa hata kama limekamilika haiwezi kutokea hitilafu nyingine itakayosababisha umeme kukatika?
 
Habari,

Hali ya mgawo wa umeme imerejea kwa kasi sana ni wiki tangu kuanza kwa changamoto hii. Ndani ya jiji la Dar es Salaam wilaya ya kinondoni hali sio nzuri.

Watanganyika tulijua baada ya Bwawa kukamilika ingekua ni mwarobaini tosha ya kukatika katika huku. TANESCO wilaya wametenga masaa 12 ndio warejeshe umeme kila wanapo kati umeme. Hii ni mbaya kwa uchumi wa Tanganyika hii.

Kuna tetesi pia kua Tanganyika inauza umeme Zambia huko hali yao sio poa kabisa. Kama mnauza mmeamua sisi tuteseke?

TANESCO tunaomba mtutangazie ratiba kamili kuhusu mgawo huu.

Kwa maana fupi BWAWA LA MWL NYERERE sio mkombozi kwa taifa.

ASANTE.
Hii tabia ya kupayuka mambo ya hearsay ndio Huwa Ina wa cost

Mgao uko huko kwenu tuu? Blackouts za kawaida ni mgao?
 
Kuna shida kubwa ya Low voltage,mkoa wa mbeya ususisani Jimbo la chunya!
Sasa hapo tatizo sio umeme kutokuwepo Bali njia za kusafirisha umeme na mashine umba ndio Hazina uwezo na ndio kazi ambayo Tanesco inafanya Kwa Sasa Nchi nzima kubadili nyaya na transformer ziendane na mahitaji.
 
Back
Top Bottom