Katikati ya mjadala unaoendelea kuhusu wageni wanaofanya kazi na biashara nchini Kenya, swali moja muhimu limejitokeza: Mgeni anapata wapi ruhusa ya kufanya kazi Kenya, na anahitaji nini?
Kwanza, kuruhusiwa kuingia Kenya hakumaanishi moja kwa moja kwamba mtu ameruhusiwa kufanya kazi au biashara. Directorate of Immigration Services inaeleza kuwa mgeni anayetarajia kuajiriwa, kufanya biashara, consultancy au taaluma fulani lazima awe na permit au pass inayolingana na shughuli anayofanya.
Baada ya maombi kukubaliwa na permit kutolewa, mwombaji anaweza kuichapisha kutoka eFNS na kuiwasilisha katika ofisi ya Immigration kwa endorsement. Makao makuu ya huduma hizi yako Nyayo House, Nairobi. Immigration pia ina ofisi za kikanda katika maeneo kama Mombasa, Kisumu, Nakuru, Eldoret, Embu, Kisii na Kericho.
Kwa hivyo permit hainunuliwi kutoka kwa agent, polisi au Huduma Centre; inatolewa na Directorate of Immigration Services kupitia mfumo rasmi wa eFNS.
Class G – Trade, Business or Consultancy: Hii inalenga wageni wanaotaka kufanya biashara, consultancy au shughuli maalum za kibiashara nchini. Masharti yanajumuisha uthibitisho wa biashara, mtaji unaohitajika pamoja na nyaraka nyingine za kisheria kulingana na shughuli.
Class R – Raia wa East African Community: Raia wa nchi wanachama wa EAC wanaotaka kuishi, kuajiriwa, kufanya biashara au taaluma nchini Kenya wanaweza kuomba Class R Permit. Wanahitaji passport, picha, barua kutoka kwa mwajiri au shirika, usajili wa biashara na vyeti vya kitaaluma pale vinapohitajika.
Immigration pia inaonya wazi kuwa kufanya kazi au biashara bila permit au pass inayohitajika ni kosa chini ya sheria za Kenya
Kwa mtu anayetaka kuthibitisha masharti au kuomba permit, sehemu rasmi ya kuanzia ni Directorate of Immigration Services kupitia eFNS, huku huduma za endorsement zikipatikana kupitia Immigration, ikiwemo Nyayo House, Nairobi.
Kwanza, kuruhusiwa kuingia Kenya hakumaanishi moja kwa moja kwamba mtu ameruhusiwa kufanya kazi au biashara. Directorate of Immigration Services inaeleza kuwa mgeni anayetarajia kuajiriwa, kufanya biashara, consultancy au taaluma fulani lazima awe na permit au pass inayolingana na shughuli anayofanya.
Work Permit Inapatikana Wapi?
Maombi yote yanaanza online kupitia Foreign Nationals Services (eFNS) Portal, ambayo inasimamiwa na Directorate of Immigration Services. Mwombaji anafungua akaunti, anachagua aina ya permit, anajaza fomu na kupakia nyaraka zinazohitajika.Baada ya maombi kukubaliwa na permit kutolewa, mwombaji anaweza kuichapisha kutoka eFNS na kuiwasilisha katika ofisi ya Immigration kwa endorsement. Makao makuu ya huduma hizi yako Nyayo House, Nairobi. Immigration pia ina ofisi za kikanda katika maeneo kama Mombasa, Kisumu, Nakuru, Eldoret, Embu, Kisii na Kericho.
Kwa hivyo permit hainunuliwi kutoka kwa agent, polisi au Huduma Centre; inatolewa na Directorate of Immigration Services kupitia mfumo rasmi wa eFNS.
Kuna Aina Gani za Permit?
Class D – Employment Permit: Hii ni kwa mgeni aliyepewa ajira maalum nchini Kenya. Mwajiri anatakiwa kutoa maelezo kuhusu nafasi hiyo, qualifications za mwombaji na, katika baadhi ya mazingira, kueleza kwa nini nafasi hiyo haiwezi kujazwa mara moja na Mkenya. Kwa sasa processing fee iliyoorodheshwa na Immigration ni Sh20,000, huku issuance ya Class D kwa wasio raia wa EAC ikiwa Sh500,000 kwa mwaka.Class G – Trade, Business or Consultancy: Hii inalenga wageni wanaotaka kufanya biashara, consultancy au shughuli maalum za kibiashara nchini. Masharti yanajumuisha uthibitisho wa biashara, mtaji unaohitajika pamoja na nyaraka nyingine za kisheria kulingana na shughuli.
Class R – Raia wa East African Community: Raia wa nchi wanachama wa EAC wanaotaka kuishi, kuajiriwa, kufanya biashara au taaluma nchini Kenya wanaweza kuomba Class R Permit. Wanahitaji passport, picha, barua kutoka kwa mwajiri au shirika, usajili wa biashara na vyeti vya kitaaluma pale vinapohitajika.
Unafuata Hatua Gani?
Mwombaji anatakiwa kufungua akaunti ya Government of Kenya Single Sign-On, kuingia eFNS, kuchagua Permit Issuance/Renewal, kujaza application, kupakia nyaraka na kulipa ada inayohitajika. Mfumo unatuma taarifa kuhusu hatua ambayo maombi yamefikia kupitia account na email.Immigration pia inaonya wazi kuwa kufanya kazi au biashara bila permit au pass inayohitajika ni kosa chini ya sheria za Kenya