Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Kwa mbwembwe nimeingia, salamu nawatakia
Za watoto nawaitikia, wakubwa naamkia,
Swali nawaulizia, natumai mtajibia,
Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia?
Mgeni akikujia, kutoka maili mamia,
Hata jirani na njia, hodi akakupigia,
Nawe ukamlakia, huku ukimkumbatia,
Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia?
Ndipo ukamwandikia, chakula cha kunukia,
Kumbe njaa kazuia, chakula kakipania,
Akala akigunia, utamu ukimwingia
Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia?
Mwisho alipofikia, sahani akaachia,
Chakula kikabakia, ni wali na mboga pia,
Ndipo ukaulizia, 'vipi hujafurahia'
Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia?
Mgeni kakuambia, siku ya kwanza nabakishia,
Ya pili ikiingia, ntakula utakimbia,
Ndipo swali kuingia, ni mila ya kuachilia,
Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia!
Tamati nimefikia, na miye nawakimbia,
Ugeni umenijia, chakula naandalia,
Kesho nitawaambia, kama alibakishia,
Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia!
Na. M. M.Mwanakiiji (Sauti ya Kijiji)