Mgeni siku ya kwanza - kula na kubakisha?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Kwa mbwembwe nimeingia, salamu nawatakia
Za watoto nawaitikia, wakubwa naamkia,
Swali nawaulizia, natumai mtajibia,
Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia?

Mgeni akikujia, kutoka maili mamia,
Hata jirani na njia, hodi akakupigia,
Nawe ukamlakia, huku ukimkumbatia,
Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia?

Ndipo ukamwandikia, chakula cha kunukia,
Kumbe njaa kazuia, chakula kakipania,
Akala akigunia, utamu ukimwingia
Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia?

Mwisho alipofikia, sahani akaachia,
Chakula kikabakia, ni wali na mboga pia,
Ndipo ukaulizia, 'vipi hujafurahia'
Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia?

Mgeni kakuambia, siku ya kwanza nabakishia,
Ya pili ikiingia, ntakula utakimbia,
Ndipo swali kuingia, ni mila ya kuachilia,
Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia!

Tamati nimefikia, na miye nawakimbia,
Ugeni umenijia, chakula naandalia,
Kesho nitawaambia, kama alibakishia,
Mgeni siku ya kwanza, ale na kubakishia!

Na. M. M.Mwanakiiji (Sauti ya Kijiji)
 
Ngoja kwanza nijaribu kumjibu Mzee Mwanakijiji...

Kila mgeni akila, lazima kubakishia
Ikiwa kamalizia, Aaonekana kapupia
Shangazi yangu Aisha, somoni alinambia:
Bila kula mara mia, Usile ukamalizia

Ugenini waingia, kwa njaa waumia
Mwiko na safuria kulamba watamania
Mwanangu wewe tulia, jaribu kuvumilia
Bila kula mara mia, Usile ukamalizia

Kuna wanawake pia wanashindwa kuangalia
Mlo wa kumalizia na ule wa kubakishia
Kwa mlo wa kukaribia, wanasafisha sinia
Bila kula mara mia, Usile ukamalizia

Ila hili lakumalizia, au tena kubakishia
Manyingi hutegemea umri pia jinsia
Kijana akimalizia anaonekana Kadhamiria
Kijana akibakishia, huonekana hana afia

Wengi wao hutumia sifa hiyokama Njia,
ya kutafuta pa kufikia, au hata kuhamia
wenyeji hufurahia vijana wakimalizia
Kijana akibakishia, huonekana hana afia
 
Last edited by a moderator:
Umenikumbusha story ya my late bro!
Aliksribishwa lunch, na mdada alikuwa anamfukuzia (lsevya Tbr); kaenda na mshkaji wake. My bro was starving n the food was mmwah! Kwa wanaowajua wadada wa kinyamwezi wa enzi zile (sio kina sisi) watakuwa wanaelewa nikisema the food was mmwah!

So, mdada wa watu (sijui ndio mila) akawaacha wale; yeye kaenda uani kuendelea na shughuli zake. My bro kafukumia lile punga na kuku wa kienyeji, akafuta. His buddy, hakuwa mlaji sana, alibakisha chakula. So my brother baada ya kusikia movement sign ya mshori kuja; akanadilisha plate. Yake iliyo clean kaisogeza kwa mshikaji na ya mshikaji yenye mabaki akaiweka kwake!

Mdada alivyoanza kutoa vyombo; akamuuliza buddy wa bro "shemeji nikuongeze chakula?".
You can imagine nini kilichotokea baada ya my bro na buddy wake kurudi ufisini!
 

mh! Dada Ngorongoro a
ni wapi hiyo?
 
sidhani chakula kiongelewacho ni cha kwenye masinia, someni kati kati, chini na juu ya mistari.
 
sidhani chakula kiongelewacho ni cha kwenye masinia, someni kati kati, chini na juu ya mistari.

Kongosho nishaelewa siku nyingi! Lkn nimeikumbuka tu hiyo story!

Na kwangu mimi, mgeni akimaliza chakula Siku ya kwanza nafurahi; kwani inaonesha kafurahia! Na ni kwa maana zote!
 
Kula ni kula jamani,mbaya kukomba mboga utaonekana hujatulia,mlafi nk. Ni vizuri siku ya kwanza ukala chakula chote na mchuzi ukanywa wote ili mwenyeji apange bajeti nzuri siku nyingine!
 
Mgeni kafakamia, aibu kajipatia,
Tonge lamkwamia, kooni kujipitia,
Style hakuitumia, kuanza maji pitia,
Sasa anaumia, pia anajutia
 
Pilau ziko za aina nyingi. Kuna pilau maua, pilau maharagwe, pilau samaki, pilau ng'ombe, pilau bata, pilau soseji,pilau mbuzi, na hiyo pilau kuku.
King'asti, pia kuna pilaw za vegetarians
Pilau njegere, pilau maharage, pilau soja nk
Kuna pilau for all tastes, hata pilau kavu ipo.
 
Mgeni siku ya kwanza???????????usijifanye mjuaji......
Pembeni kuangalia, kila dakika macho chini.....
Tabasamu tupilia.lakini liwe la mbali.....
Mgeni siku ya kwanza...usijifanye mjuaji.....
Nina ugeni mahali leo
thax kwa tips..........
 
king'asti, pia kuna pilaw za vegetarians
pilau njegere, pilau maharage, pilau soja nk
kuna pilau for all tastes, hata pilau kavu ipo.
mwali naona upo bussy na ugeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…