Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Mgeni siku ya kwanza
mpe mchele na panza;
mtilie kifuani,
mkaribishe mgeni.
Mgeni siku ya pili
mpe ziwa na samli;
mahaba yakizidia,
mzidishie mgeni.
Mgeni siku ya tatu
jumbani hamuna kitu.
mna zibaba zitatu,
pika ule na mgeni.
Mgeni siku ya nne
mpe jembe akalime.
akirudi muagane,
aende kwao mgeni,
Mgeni siku ya tano
mwembamba kama sindano,
hayeshi masengenyano,
asengenywayo mgeni.
Mgeni siku ya sita;
mkila mnajificha;
mwaingia vipembeni
afichwaye ni mgeni.
Mgeni siku ya saba,
si mgeni ana baa.
hata moto mapaani
katia yeye mgeni,
Mgeni siku ya nane;
njoo ndani tuonane.
atapotokea nje,
natuagane mgeni,
Mgeni siku ya kenda;
enenda mwana kwenenda!
usirudi nyuma nenda,
utokomee mgeni.
Mgeni siku ya kumi
kwa mateke na magumi.
hapana afukuzwaye,
Ila ni yeye mgeni.
mpe mchele na panza;
mtilie kifuani,
mkaribishe mgeni.
Mgeni siku ya pili
mpe ziwa na samli;
mahaba yakizidia,
mzidishie mgeni.
Mgeni siku ya tatu
jumbani hamuna kitu.
mna zibaba zitatu,
pika ule na mgeni.
Mgeni siku ya nne
mpe jembe akalime.
akirudi muagane,
aende kwao mgeni,
Mgeni siku ya tano
mwembamba kama sindano,
hayeshi masengenyano,
asengenywayo mgeni.
Mgeni siku ya sita;
mkila mnajificha;
mwaingia vipembeni
afichwaye ni mgeni.
Mgeni siku ya saba,
si mgeni ana baa.
hata moto mapaani
katia yeye mgeni,
Mgeni siku ya nane;
njoo ndani tuonane.
atapotokea nje,
natuagane mgeni,
Mgeni siku ya kenda;
enenda mwana kwenenda!
usirudi nyuma nenda,
utokomee mgeni.
Mgeni siku ya kumi
kwa mateke na magumi.
hapana afukuzwaye,
Ila ni yeye mgeni.