Tetesi: Mgodi wa Bulyankulu kufungwa

mtanzania1989

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2010
Posts
4,068
Reaction score
6,758
Kuna tetesi Acacia wameamua kuanza kufunga mgodi wa Bulyankulu week 5 kuanzia sasa. Acacia wana miliki migodi mitatu Tz ( North Mara, Buzwagi na Bulyankuli).
Kutokana na maelezo yao, Bulyankuli ulikuwa ufungwe 2019 na ni miongoni mwa migodi iliyokuwa inazalisha makinikia mengi na kutegemea mapato ya makinikia kama sehemu muhimu ya faida yake, kutokana na zuio la makinikia wanaamini hauna faida tena kwa sasa. Serikali ya Tz mpaka sasa bado wapo katika meza ya majadiliano na Barrick.

Wito: GoT watoe taarifa rasmi kuhusu kinacho endelea, nia na kusudi la Rais na serikali ni jema ila mkiacha hizi habari tukawa tunapata kutoka kwa maadui zetu mjue zitaambatana pia na upotoshaji na propaganda zao.
 
Nyerere aliifunga na tukawa tunaishi vzr tu na kuota dhahabu juu ya ardhi baada ya mvua kunyesha na kumonyoa baadhi ya sehem ya ardhi.
Wasafiri salama
 

Acha kuleta habari ambazo hazifanyiwa uchunguzi wewe.
 
Mtoa mada;

Accacia haijawahi kumiliki Geita Gold Mine (GGM) na wala life span ya Bulyahulu si 2019 kama ulivyosema bali hadi 2035. Kwanini usenena uwongo? Nenda kaulizie zaidi nani mmiliki wa GGM.

Kuonesha wewe ni mtupu kwenye hii field ya madini; mgodi maarufa nchini kama Bulyahulu unauita Bulyankuli
 
Hatuna maadui hapo.ni kuhitikafiana tuu.walipewa bure sasa mnawatoza hawatakubali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wewe nae sijui umetokea wapi.
mgodi geita na acacia wapi na wapi.

Pili ukiingia mgodi wowote wa acacia toka siku ya kwanza hadi unaondoka hata ukikaa miaka ishirini tishio la kufungwa huwa lipo kila siku. ni vipropaganda vinavyowaweka nchini
 
Mficha uchi..............
 
Nyie hamjamuelewa mtoa mada.. alitaka tu kujua majadiliano ya serikali na barrick yanaendeleaje ila alikosa namna ya kuuliza. So akaamua kutunga habar habari ya uwongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliposoma tu kale ka kipengele kuwa Accacia wanamiliki mgodi wa Geita nikachoka kabisa. Sikua na haja ya kusoma zaidi nikaona hizi ni PROP-za-GANDA. Yule jamaa tunaempaka matope ya kukosa uzalendo huziita "professorial rubbish"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majadiliano yamechukua mwezi hadi sasa.......tunasubiri ngonjera !!!
 
Hii mambo tayari ilikuwa inasemwa kwenye baadhi ya corridor za Acacia nje ya nchi, leo ime rasmishwa kwa watanzania sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…