Mgodi wa dhahabu wa wajerumani uliosahaulika

Mgodi wa dhahabu wa wajerumani uliosahaulika

Katika tafiti zangu za hapa na pale kuna mgodi mmoja mpk leo naona kama vile umesahauliwa kabisa ....mgodi huu upo Afrika mashariki , katika nchi ya Tanzania

Mgodi huu unasadikika kuwa ni mgodi wa kwanza kwa Tanganyika ambapo wajerumani baada ya kuanza kutawala Tanganyika mwaka 1885 , katika ukanda wa kanda ya ziwa hakukuwa na upinzani mkubwa

Kutokana na kauli ya viongozi wa kisukuma kwa kuwaogopa wajerumani na kubaki na slogani ya KAYA YA NGOBA NAYO KAYA ( WAKIWA NA MAANA NYUMBA YA MUOGA NAYO NI NYUMBA)

Mgodi huo unapatikana katika eneo la busega katika kijiji ...kimoja kinaitwa NGASAMO ...

Kijiji hicho ndipo wakolini wa kijerumani ..walianzisha mgodi wa dhahabu ambao ulikuwa ukitoa dhahabu nyingi kutoka na maelezo ya

Bibi kizaa bibi Mzaa mama yangu ambaye alifariki mwaka 2010 akiwa na umri wa miaka 120 ...hiyo ni neema nilipata na lilikuwa mdadisi sana kutokana na kijijini hapo mimi ndiyo nilikulia hapo !! Kuna eneo lilikuwa limezungushwa vizuri liliitwa NYAMAGANA pembeni kukiwa na magofu ya nyumba za wakoloni


Katika mgodi huo ambao ulikuwa na njia nne za kuingia na kutokea mgodini ...ambao mgodi huo wajerumani walifanikiwa kuchima zaidi ya Futi 60 na zaid kwenda chini na kuchonga njia mbali mbali kwa ajili ya viberenge vya kubebea mchanga kutoa mgodini

Hivyo kuoelekea eneo kubwa la mji wa ngasamo na maeneo yanayozunguka mpk ,dutwa ,gasuma kuwa juu huku ndani kukiwa na njia pamoja na taaa na maisha yalikuwa yakiendelea

Na wajerumani walifanikiwa kuwa na vibarua wengi ndani ya mgodi huo tatizo amabao walikuwa ni mamia kwa mamia walikuwa wakipishana kwa shift

Bac ilifika mwaka 1918 baada ya wajerumani kuanza kuhisi kishindwa kwa vita kuu ya kwanza baada ya kupata redio call ambayo ilikuwepo pale mgodini kutoka kwa Gavana wao

Kuna Mwingereza anaonekana kupata ushindi ...wakaona haitawezekana kubeba shehena ya mali amabayo yalikuwa ni masanduku makubwa sana

Amabayo yalikuwa na madini ya dhahabu na madini ya blue sample moja mpk leo ipo nitakuja kuuplood picha ili watu waone ....

Wakaamua kutoboa mwamba kwa kuwapa ....maagizo wale ma formen wa kiafrika walipotoboa mwamba ule haikupita hata robo saaa yalitokea maji ya ajabu sana ambayo yalifunika wote na wote waliokuwa ndani ya mgodi maisha yaliishia mle ndio maana mpk leo panaitwa NYAMAGANA maana yake (mamia )

Baada ya kuondoka kuja waingereza kuanza kutawala Tanganyika hawakutaka kabisa kujihusisha na mgodi ule na kupaoona kama hapakuwa na mali yoyote zaidi ya kisima kikikubwa cha maji

Kuna miaka nakumbuka ya 90 walikuja magiologist pale kijini ila kwa tulivyokuwa tunahisi walikuwa wajerumani maana walikuwa na ramani na kuna bikoni zilizoachwa na wajerumani wa mwanzo walikuwa wakizifatilia

Baadae kuna wachimbaji wadogo wadogo miaka ya 2000 walivamia pale kijijini na kuanza kufanikiwa kuingia kwenye mgodi kupitia njia za nyuma ya mlima amabzo ilikuwa inachukua km dk 30 kutembea ndani kwa ndani mpk kufika kwenye kitovu cha mgodi

Walifunaga mashine na kuanza kufanya shughuli za uchimbaji na maji ya pale mgodini walitumia kuoshea dhahabu mpk pakakauka na kufanikiwa kuuziba mwamba kwa cement maalum

Njia zikawa wazi ...ila ngazi nyingi za kuteremka mle nyingi zilikuwa zimeozeshwa na maji hivyo wenye roho ngumu wakawa wanaingia wanabetua yale masanduku wanachukua mzigo ndani wanaofanikiwa wanatoa kuna baadhi ya vijana mpk leo pale walifanikiwa kutoka na vitoafali wapo vizuri

....kwa leo naomba nikomeee hapo next time nita uplood picha za mgodi kuanzia juu hadi ndani nilifanikiwa kuingia hadi kwenye korido za mwanzo mwamzo

Hadi leo naona kama umesahaulika hauna mwenyewe tukutane next time
f







Sent using Jamii Forums mobile app
UPDATES.

Huo mgodi watu washaanza Kuchimba Na wanapata Sana Dhahabu
Hata Mimi nipo hapa hapa Mgodini.

Sehem iko katika wilaya mbili yaan Bariadi na Busega mkoan Simiyu
 
Back
Top Bottom